anko akiwa vekesheni bilila lodge kempinski, serengeti. hii imetajwa kuwa hoteli bora kuliko zote afrika mashariki n kati
sehemu ya presidential suite katika bilila lodge kempinski
bafuni
chumbani
chumba cha kukaa mandhari kwa nje. bwawa la mbele huja tembo kibao kunywa maji
chumba cha kawaida
lounge
bwawani
tovuti yake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. Must read from NY Times

    African Wealth and African Style at a Glamorous Juncture

    http://www.nytimes.com/2009/10/05/business/media/05magazine.html


    BG

    ReplyDelete
  2. MIMI SINA MAKENGEZA, PICHA YA CHUMBANI NA YA CHUMBA CHA KAWAIDA MBONA NI ILEILE AU INATEGEMEA NA WAKATI.

    ReplyDelete
  3. Anko nanhii, mie naomba kuuliza, hiyo hotel ndio bora kwa vigezo vipi?
    Kwa Mfano; kuna vitu kama idadi ya vyumba, ukubwa wa eneo la hotel, location, huduma zitolewazo, umahili na uwezo wa wafanyakazi, na je ipo katika nyota ngapi ?

    ReplyDelete
  4. Hivi rais huwa anaoga mwenyewe au anaoshwa?

    ReplyDelete
  5. Kitu Kimetulia! Aibu!! Hiyo ni Bilila au Bilali? Nani Mmiliki wa kitu hiki kizuri? Hata kama atakuwa ni fisadi anastahili pongezi kwa kuwekeza nchini!!

    ReplyDelete
  6. Hii hoteli kwakweli ni nzuri sana, bongo tambarareeeeeeeee duh! hivi kaka nanihii nani anamiliki hii hoteli?

    ReplyDelete
  7. Anko nanihii mbona unakuwaga mwenyewe mwenyewe tu?

    ReplyDelete
  8. Michuzi naona unakula kijivekesheni kwa kutumia kijiko kikubwa. duh! lakini ni kuzuri huko uliko. Paulo Kamau au Ze Shemeji

    ReplyDelete
  9. Napenda kuuliza, Je hii hotel ni ya nani?? Ni Ya mtu binafsi??Na ya Serikali?? Je Mkoa wa Mara na Wilaya ya Serengeti zinafaidikaje??

    Watz kwa hii hotel kuingia huwezi kama si fisadi maana per day ni Tsh $900??
    We need investigation, Wengine wanasema ni ya JK wengine ya Mke wa JK?? Je ni kweli?? Au Maneno ya watu kwa kuwa aliifungua mama salama na Mh.

    Maoni yangu yenu je??Inaweza kuwa kweli au si kweli??

    Michuzi niwekee hii

    ReplyDelete
  10. Hii kweli ni Balaa, Bipe bei zake au kwenye website yake zinapatikana ngoja nione.

    Hii kiboko,Watu wa serengeti kazi kwao sisi wamakndemhhhhhhhh

    ReplyDelete
  11. Mmmmmmh! unahela wewe? kalale Bilila lodge Kempiski, Serengeti.

    ReplyDelete
  12. jamani tupeni bei basi tukatembee kama vijisenti vitakubali

    ReplyDelete
  13. Paul kabewaOctober 06, 2009

    kaka naona kweli hiyo hoteli ni ya ukweli ulikosa hatamtu wa kukuphotoa ukaamua ujiphotoe mwenyewe ili mradi tu wadau wako tusikose uhondo hahaaaaaaaaa thank you sana

    ReplyDelete
  14. UTANDAWAZI AU UTANDAWIZI? HIVI KEMPINSKI MMILIKI WAKE NANI?? HILO BWAWA MAJI YAKE HAYANA CHLORINE?? YASIJE YAKADHURU WANYAMA WETU!HAKUNA RATE ZA WAZAWA?? LOL!

    ReplyDelete
  15. Wadau hii ngoma sio ya viwango vya wabongo!! Yaani hata bei zao ziko kwa EUR na ya chini saaana EUR 500 per Rm kwa siku!! Sasa mbongo akitaka kwenda hadi akanunue EUR au inakuwaje???Kazi kwenu mafidadi wa Bongo!

    ReplyDelete
  16. Anko nanii ulikosa kabisa mtu wa kukupiga picha!!!!!???

    ReplyDelete
  17. Alafu si mbali sana na hapo serengeti ukienda wanakoishi wa masai kumekauka Maji, Watu wamekauka njaa tupu sasa sielewi pesa wanazowasaidia wanakijiji zinaenda wapi? wanakijiji wanajisaidia vipi? Nimuda sasa Tanzania wakiwasaidia Wananchi vijijini lazima wawafundishe nakutumia na kuweka vitu ambavyo vitawasaidia Mbele.

    ReplyDelete
  18. Hi Michuzi hebu tuambie malazi ni kiasi gani ikibidi na sisi wa kawaida twende au ndio mambo ya $USD tu ??au kama kuna mdao anauzoefu tafadhali chumba ni shilingi ngapi hapo ??

    ReplyDelete
  19. mjomba michudhi nruche na changazyi nae.

    ReplyDelete
  20. Tunaomba bei!

    ReplyDelete
  21. Balozi wa Nanihii

    Huuu ushabiki mwingine kwa sio tulioenda skuli kidogo tunaustukia.

    Hii Hoteli imefunguliwa na JK chini ya miezi 3 iliyopita. Sasa hebu tuelimishe hiyo REKODI YA UBORA kuliko Hoel zote Africa Mashariki imejipatia lini??!!!

    Au ndio yale yale ya kuzungumzia Majengo na kuona ni bora...bila kuangalia huduma, usafi, chakula n.k

    ReplyDelete
  22. Kiwango ni 101%. Inavutia haswaaa!

    ReplyDelete
  23. umevaa jezi za constraction

    ReplyDelete
  24. mambo ya kujifoto

    ReplyDelete
  25. Ndugu watanzania wenzangu hiki kitendo cha kujenga hoteli ndani ya mbuga ni uhujumu uchumi.hii ninaweza kusema ni wildlife genocide.Kila mtu sasa atataka kujenga hoteli ndani ya mbuga ,hivi kweli hii ni busara.kwa kweli hatutendi haki mbeli ya viumbe wengine.Ambao wanatuletea faida.Future ya watoto wetu watakuwa masikini kabisa.kwani Wanyama wote watapotea.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  26. Naona bongo tuna maeneo mazuri sana ya matanuzi, sasa itabidi umepeleke mama mithupu kwa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa! Au vipi mkulu?

    ReplyDelete
  27. WATANZANIA TUNATAKIWA KUSEMA SASA NI MWISHO WA WATU WACHACHE WAMBAO TUMEWAPA MADARAKA NA WANATUMIA VIBAYA KATIKA KUHARIBU UCHUMI WA NCHI.TUNAISHAURI SERIKALI MAPEMA KUWA KIDENDO CHA KUJENGA HOTELI NDANI YA MBUGA NI KUHARIBU UCHUMI WA NCHI.HAO MAJENGO ATALALA NANI HAPO BAADAYE.KWANI WATU WANAKUJA KUONA WANAYAMA.KAMA WANYAMA WOTE WAMEKWISHA.TUSIMAME WATANZANIA HII SIO SUSTAINABLE ECONOMY.HOTELI ZOTE ZITOLEWE KWA FAIDA YETU NA YA WATOTO WETU.HATUTAKI WATOTO WETU WAENDE ULAYA KUANGALIA SIMBA HAPO BAADAYE."HATUTAKI KUANZISHA JIJI JIPYA NDANI YA MBUGA" "SERENGETI CITY"


    THE INSTITUTE OF RESEARCH AND ENVIRONMENTAL QUALITY[IREQ]
    www.ireq-tanzania.com

    ReplyDelete
  28. Kweli inaonekana hi hoteli nzuri sana. Natumaini na huduma zao zitakuwa ni motomoto. Isije ikawa ni hoteli nzuri kwa majengo lakini huduma zikawa za "kiswahili"

    Vipi kuhusu bei zao kwa chumba cha kawaida kwa mbeba maboksi kama mimi? Nimeangalia katika tovuti yao sijaona cho chote. Asante.

    ReplyDelete
  29. Ni sehemu nzuri sana ila nilikuwa ninaangalia bei kwa nite moja mmhh ni kisu kirefu kwa mtanzania wa kawaida sidhani kama anamudu labda awe fisadi! Bei yake ni sawa na ujenzi wa darasa moja au madawati 100! Naona na hata kwa wageni ni wale walio na pesa sio watalii wanaokuja kwa groups kama kawaida yao. Nimeona watalii wengi wa nchi za magharibi huwa wanajiandaa kwa zaidi ya miaka 5 kuja kutalii Africa na wanachanga kwa groups ili kupunguza gharama. I like the place I can come and spend at least three nites. Nice place.
    Mdau USA

    ReplyDelete
  30. Yote ubatili mtupu

    ReplyDelete
  31. shilingi ngapi kulala humo?

    ReplyDelete
  32. vekesheni kila siku mwenywe. si umeoa weye?

    sasa inakuwaje unakuwa mchuma asilimia 99 au ni kizazi wasema vekesheni?

    ReplyDelete
  33. uncle hukua na mtu wa kukupiga picha

    ReplyDelete
  34. Mheshimiwa Michu inaonekana ulikuwa unajitaswira mwenyewe maana yake kofia ulivyoweka, macho ulivyoyalegeza na mkono wa kushoto umekakamaa. Lakini umetoka bomba. Inaonyesha siku hiyo kulikuwa hakuna hata watalii, akina MIchu wala wafanyakazi si ungeomba wakutaswire.

    ReplyDelete
  35. hiyo ni lodge, siyo hotel. kuna tofauti kati ya hizo facility mbili.hotel ni kama Kilimanjaro au Movenpick

    ReplyDelete
  36. Sasa nimeamini maneno ninayosikia mtaani kwamba na wewe Anko ni fisadi.

    Hivi hela ya kutanua kwenye hotel kubwa kubwa kama hizi unazipata wapi? Kwenye hii glopu? Sorry, hii Globe? Ah, samahani bwana, hii Blog?

    Mbaya zaidi siku zote upo bila shemeji yetu kwenye haya matanuzi ya kufa mtu. Siyo fresh Anko.

    ReplyDelete
  37. Enzi za Mwalimu watu walikuwa wanasema waweke hoteli za kitalii kama hiyo ili wageni waje! Wazungu walisema wanataka sehemu ya kulala ambayo ni safi, kina choo safi, kina simu ambayo mzungu ataweza kupiga Ulaya na kusema, 'I'm calling you from the middle of a wildlife park...just saw a lion!' Naona tumefika sasa. Ila hiyo bei! Duh!

    ReplyDelete
  38. jibu basi!!!!!! shi ngapi kulala? watu tushabeba box misuli imetutoka ka mapawa vile, tunajua hukulala humo ulikuwa unapita tu lakini we mtoto wa mjini lazima uliuliza bei shing ngapi?

    ReplyDelete
  39. KUTOKANA NA MACHO YENU HUKO BONGO NI WACHOVU NDIYO MAANA MNAONA HIYO HOTEL BABU KUBWA...HUKU MAMTONI HIYO NI SAWA NA REST AREA ON FREEWAY ...KIZULI NINI NA INANYOTA NGAPI...10...TEMBEENI MUONE. MDAU MONEY UK.

    ReplyDelete
  40. Wadau mnaoulizia bei ya kulala hapo, kwa siku ni kama shilingi milioni moja. Picha zinaonyesha mandari nzuri, panafaa kufanyia semina elekezi.

    ReplyDelete
  41. Wakubwa, mbona hakuna anayeweza kujibu swali langu? Je mheshimiwa rais anaoshwa au huwa anaoga mwenyewe? Na kama anaonshwa, nani anamwosha? Yule mpambe wake?

    ReplyDelete
  42. Bei ni hii kwa chumba kimoja kwa siku ni Euro 500 na pia kuna chumba cha Euro 2800 kwa siku nadhani hiyo ni kwa wale wenye vijisenti.manake ni kama milioni tano za tz.So kama unampango wa wa kutulia hapo kwa wiki inabidi uwe na kama milioni 10 flani duuuuh! ukitoka hapo ni mwendo wa mihogo na maharage mwaka mzima.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...