Francis Cheka (kulia) akirusha makombora kwa Japhet Kaseba
Bondia Francis Cheka wa Mji Kasoro Bahari amesema anataka kucheza tena na Japhet Kaseba katika Kick Boxing ili kumaliza kabisa ubishi kwamba kama ilivyokuwa enzi zile za Stanley Mabesi, basi yeye ndiye mfalme wa ulingo kwa sasa nchini.
Kaeba hakuweza kupatikana mara moja kwa majibu, ila endapo kama pambano la Cheka na Kaeba litafanyika, itakuwa ni historia ya pekee nchini, Sfrica na duniani kwa jumla kwa mabondia wawili kumenyana katika tasni mbili tofauti.
Katika mpambano uliopita ukiofanyika neshno ya zamani na kushuhudiwa na umati mkubwa, mambo hayakuwa mambo kwa Japhet Kaseba baaada ya Francis Cheka kushinda pambano lao hilo lenye raundi 12 la uzani wa welter weight kwa KO ya raundi ya tisa.
Japhet Kaseba akihesabiwa akiwa nje ya ulingo katika raundi ya tisa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Mbese vipi tena babu unatuangusha. Gangamara mwana..ila next time nujua utashinda.

    ReplyDelete
  2. nice one....sikuzote mdomo ndio unaokiponza kichwa

    ReplyDelete
  3. Looks like boxing not kickboxing.The Gears suggest it was boxing.Boxing and kickboxing are two different games.

    ReplyDelete
  4. kweli iyo ni boxing kwani kuna mtu amesema iyo ni kick boxing??labda nikusaidie, Francis Cheka na Japhet kaseba walipigana kwenye boxing na Cheka kuibuka mshindi, sasa Cheka anataka apambane na kaseba kwenye Kick boxing pia ili aonyeshe umwamba wake.Kumbuka kuwa Kaseba kabla ya kuingia kwenye boxing alikuwa bingwa kwenye kick boxing na hakuwa na mpinzani..Sasa cheka anataka ampige kwenye michezo yote miwili..

    ReplyDelete
  5. Lakini Mdogo wangu nilimwonya kuwa asipalamie fani za watu BOXING. Ndio nakubali kwa KICKBOXING yeye ni mfalme. Pia asitake masifa ya kijinga kwa haraka haraka mara fani hii mara ile. Kwanza komaa na hii iliyokupa huu umaarufu. ONA SASA!!! AIBU HII, KO!! MIGUU JUU KA MENDE. UTULIAGE ACHA MAPEPE.

    ReplyDelete
  6. UNAONA SASA; HIZO KAMBA ZA ULINGONI NI ZA KUTOKA CHINA. WEWE UMEONA WAPI KAMBA ZA ULINGO ZINAKUWA LEGEVU NAMNA HIYO.

    HAWA WACHINA HAWA...

    ReplyDelete
  7. JAPHET.

    KAKA NI KAKA TU, NAKUJUA VIZURI UFANYAJI MAZOEZI WAKO, MDA MREFU SANA KTK GYM YA BMK, LONGTIME TABIA YAKO, UNAPENDA KUJIONYESHA UNAWEZA ZOEZI, ILA WEWE ILIKUWA BADO SANA KUCHEZA BOX, MAANA BOX HAITAKI UTOTO, FATILIA AKINA TYSON, AU MWOMBE CHEKA AKUFUNDISHE KAMA UKO INTREST, ILA PIA SIO ULINGONI JIFUNZIE MITAANI NA UMLIPE, KUOMBA PAMBANO SIO KUJIFUNZA UZA PIKIPIKI ULIPE ADA KWA CHEKA BOX INAPESA SANA, ITALIPA ILA USIDANDIE GARI KWA MBELE KASOMEE, ONA UMEZIDIWA HUELEWI KUWEKA MIKONO JUU LEFARII ATAJUAJE? INAONYESHA HATA KIDOGO HUJUI BOX ILA NGUVU UNAZO ILA SIO ZA KUMSUMBUA CHEKA UWEZO WA CHEKA NI KAMA LENOX LEWIS WEWE HUWEZI KAMA UNAPESA MPOROMOTI AENDE MBELE ILA UKIOMBA PAMBANO ATAHARIBU UBONGO WAKO BURE, SI UNAONA MUHAMAD ALLY NICHIZI NGUMI UIMUDU ILA SIO NZURI SANA KAMA HUWEZI UTAKUFA. job.

    ReplyDelete
  8. Du!balaaaaaaaaaaaa! watu wanatoa dozi!

    ReplyDelete
  9. raila odingaaaaaaaaaaOctober 08, 2009

    I know Japhet very well, yeye X factor yake ni kwenye Miguu.Angalia mechi zake za kick boxing, anaanza kumpiga mpinzani miguuni kwa wingi.Mguu wake ni chuma, na unalegeza uwezo wa miguu ya mpinzani kubeba mwili.Nilimkataza asiingie boxing, nguvu za mikono hana
    Japhet kumbuka enzi zetu Coloseum, pole

    ReplyDelete
  10. Cheka akirogwa kupigana na Kaseba katika kick boxing, AMEKWISHA!!! Na inabidi siku hiyo washikaji wake waje na machela kwani lazima avunjwe miguu! Kaseba ana nguvu za ajabu za miguu.

    ReplyDelete
  11. sio lazima bwana anawweza akapigwa vile vile!! cheka hata akimwili tu hailingani hata kidogo.yaani kaseb anweza akapigwa tena hat kwenye kick boxing

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...