2011 Diversity Visa Lottery Program (GREEN CARD)
Starts 2nd October, 2009
The Department of State announces the opening of the registration period for the DV-2011 Diversity Visa lottery. Entries for the DV-2011 Diversity Visa lottery must be submitted electronically between noon, Eastern Daylight Time (EDT) (GMT-4), Friday, October 2, 2009, and noon, Eastern Standard Time (EST) (GMT-5), Monday, November 30, 2009.
Applicants may access the electronic Diversity Visa entry form (E-DV) at www.dvlottery.state.gov
during the registration period.
Paper entries will not be accepted. Applicants are strongly encouraged not to wait until the last week of the registration period to enter. Heavy demand may result in website delays. No entries will be accepted after noon EST on November 30, 2009.

Important Notice
No fee is charged for the electronic lottery entry in the annual DV program. The U.S. Government employs no outside consultants or private services to operate the DV program. Any intermediaries or others who offer assistance to prepare DV entries do so without the authority or consent of the U.S. Government.
Use of any outside intermediary or assistance to prepare a DV entry is entirely at the entrant’s discretion.
FOR DETAILS ON GREEN CARD
AND SCHOLARSHIPS - VISIT
MAKULILO, Jr.
San Diego, CA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 43 mpaka sasa

  1. mdau naomba ufafanuzi wa hili swala kabla sijalala, please kesho ni tarehe 2

    ReplyDelete
  2. Makulilo nakufagilia kinoma, yaani katika watu wasio na roho ya Korosho ni wewe! Mungu akusaidie kama anavyoendelea kunisaidia mimi!

    ReplyDelete
  3. hiyo ni bahati nasibu ya work and live in USA mimi ni mmojawapo ya watanzania walioshinda hiyo bahati nasibu na kwa sasa mimi na familia yangu tunaishi WASHINGTON DC ni watanzania wachache wanaoifahamu hii dv lottery nchi za wenzetu kama nigeria na cameroon kila mwaka karibu kila nchi inatoa raia zaidi ya 8000 kuja marekani wenzetu kenya wanajitahidi kwani wanatoa karibu watu 4000 kila mwaka na kupata uraia wa kudumu hpa USA

    ReplyDelete
  4. ndugu yangu hiyo ni bahati nasibu ya kuishi USA kama unaweza kimombo soma vizuri hiyo tangazo

    ReplyDelete
  5. mkuu hiyo kucheza ni bure tu

    ReplyDelete
  6. UFAFANUZI

    Mtoa maoni hapo namba moja umeuliza suala la msingi kupata ufafanuzi. Kwanza kabisa ni kwamba, kumekuwapo watu ambao wanatengeneza websites nyingi wakizifananisha na hii ya ukweli ya Green Card na wanadai hela. Hizo zote ni za uongo. Njia fupi sana ya kujua kama ni uongo, katika websites zao zote huwa zinaishia na .com, .org, .net , .uk nk.Na ukitaka kujua kama ni website ya ukweli toka serikali ya Marekani itaishia na .state.gov na full website yao ya Green Card ni www.dvlottery.state.gov

    Kitu kingine cha msingi, hakuna malipo yoyote yale, zaidi ya wewe kupiga picha inayotakiwa kwa vigezo sahihi.Nanukuu "Important Notice
    No fee is charged for the electronic lottery entry in the annual DV program. The U.S. Government employs no outside consultants or private services to operate the DV program. Any intermediaries or others who offer assistance to prepare DV entries do so without the authority or consent of the U.S. Government". Fungua link hii upate masharti yote ya Green Card na picha inatakiwaje http://www.travel.state.gov/pdf/DV-2011instructions.pdf

    Picha hiyo unaweza kujipiga kwa digital, zingatia masharti yake, na uiweke ktk vipimo vinavyotakiwa.Kama upo Dar kwa mfano na unapata usumbufu unaweza kwenda MYFAIR Plaza na kuwaambia unataka picha ya Green Card watakupiga, wao wanajua vipimo hivyo.Au unaweza kwenda any photo shop na ukishapiga backround ikiwa nyeupe, unaweza kunitumia then nikakuwekea ktk vipimo sahihi then nikakutumia tena kwenye e-mail yako ili uweze kufanya application yako mapema.

    Suala la muda wa kuanza. Lottery inaanza October 2nd, Saa 6 mchana for Eastern Time, hivyo nenda na masaa hayo, au sio lazima ufanye application hiyo 2nd, maana deadline ni hadi Nov 30, ila ni vyema ufanye mapema wiki za mwanzoni kwani hata wao (serikali) inashauri mtu kufanya application early na sio kusbiria siku za mwishoni, unaweza kushindwa kutokanana na sababu za kiufundi nk.

    Nawatakia mafanikio mema wote kwenye kinyang'anyiro hicho. Ukitaka kuona watu (idadi) ya wanaoshinda fungua links hizi mbili.

    Kwa mwaka 2009

    http://travel.state.gov/visa/immigrants/types/types_4317.html

    Na 2010 ni

    http://travel.state.gov/visa/immigrants/types/types_4574.html

    MAKULILO, Jr.
    www.makulilo.blogspot.com
    San Diego, CA

    ReplyDelete
  7. unahamasisha watanzania kuhama, siyo? hapa bongo safi tu. wala huhitaji kadi kuishi. wasomali, warundi, wanyarwanda etc etc wote wanapeta tu bila kadi. sasa mambo ya kuomba hayo makadi ya kijani ni ya nini?

    ReplyDelete
  8. Yes, tarehe 02-10-2009 kesho

    ReplyDelete
  9. wenye mausongo wa kuishii marekano jitokezenuio basi maana hio ndo njiaa pekeee ya kupewa kibali cha kuishi na kufanya kazi kwa obama.

    ReplyDelete
  10. green card inasaidia nini ukiwa nayo mtu,huu mimi nauona ni upuuzi fulani tu wa wamarekani kudhania kila mtu anatamani kupata green card yao wakati wenyewe wanachapika kishenzi na life huko nafuu ingekuwa ulaya manaake MASIKINI WA MAREKANI HAJAACHANA MBALI NA MASKINI WA BONGO MASKINI WA ULAYA SI SAWA KABISA NA MASIKINI WA MAREKANI SO WAONDOE HUO UPUUZI WAO WA GREEN CARD

    ReplyDelete
  11. hii bahati nasibu inapitia ubalozi wa marekani hivyo hakuna utapeli kila kitu utaambiwa waziwazi ok

    ReplyDelete
  12. kila mwaka serikali ya USA inatoa visa kati ya 80000 hadi 100000 kuwapa nafasi ya watu wa kutoka nchi mbalimbali duniani kuishi USA
    N;B HAKUNA UBAGUZI WA DINI,KABILA,MILA,TAMADUNI,Tanzania kila mwaka watu kama 350 hivi hushinda ila ni kwa sababu watanzania wachache ndio hucheza lakini nchi kama MISRI,ALGERIA,GHANA,MOROCO,LIBYA,NIGERIA jamaa kibao wanashinda ,mdau USA

    ReplyDelete
  13. wadau mnaopinga dv lottery na chuki binafsi na roho za korosho kwani wamarekani hawalazimishi mtu kwenda kuishi kwao ila ni hiari ya mtu ndio maana tanzania hatuendelei tumejaa umaskini wenzetu waarabu na wahindi na wachina wanacheza sana hii dv ila kuna baadhi ya watoa maoni wanajidai hawana shida

    ReplyDelete
  14. wew ambaye dv lotery haikusaidii kaa kimya usisemee na watu wengine ok

    ReplyDelete
  15. ulaya na marekani kwa sasa hakuna dili kwani wamehamishia viwanda vyote china kupata cheap labour na cheap material je utafanya kazi gani huko?

    ReplyDelete
  16. uchina ni taifa tajiri ila wamecheza hadi wamemaliza nafasi zao zote

    ReplyDelete
  17. tunashukuru mdau uliyetoa hii tangazo MINGU AKUBARIKI SANA

    ReplyDelete
  18. unayesema kuwa tanzania maisha ni sawa na usa nakuomba tembelea mjengwa blog ujifunze

    ReplyDelete
  19. tungepata wabongo 10 kama makulilo nafikiri tutapiga maendelea fulani

    ReplyDelete
  20. ILA UNATAKIWA KUWA NA MTU WA KUKUPOKEA HUKU USA KAMA UKISHINDA

    ReplyDelete
  21. unayetaka maelekezo zaidi andika neno dv 2011 katika google

    ReplyDelete
  22. Wadau, pamoja na yote, ingekuwa vizuri wale ambao hawaijui Marekani wakafahamishwa ukweli, kabla hawajaenda. Maandalizi na elimu ni muhimu. Mimi mwenyewe, kutokana na uzoefu wangu wa Marekani, ninafanya juhudi ya kuelezea ninayoyafahamu. Kwa mfano, nimechapisha kitabu, ambacho kinapatikana Dar es Salaam, simu namba 0717413073 na 0754888647 na pia mtandaoni. Bofya hapa.

    ReplyDelete
  23. JAMANI WATANZANIA ACHANANENI NA USHAMBA. MAREKANI SIKU HIZI MICHOSHO HAKUNA DILI KABISA KUMEBAKI JINA TU. MAREKANI ILIKUWA ZAMANI. WATU HAMJUI TU DILI NI BORA UUMIZE KICHWA JINSI YA KUINGIA ULAYA. USWISI, NORWAY SWEDEN, LUXERMBOURG HATA UK NDO NCHI ZA KWENDA SIO MAREKANI, MAREKANI KUMECHOKA MBAYA KUMEBAKI JINA TU, WATU WANAPIGIKA KINOMA. CLEANERS IN LUXERMBOURG NETS 2OOO POUNDS AFTER TAX, NCHI AMBAYO KIPATO CHA BINADAMU NI KKIKUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI KWA SASA NI USWISI HATA WAINGEREZA WAJANJA WENYE VYETI VYAO WANAKIMBILIA HUKO SAHIVI. NORWAY SWEDEN MAMBO MSWANO HUWEZI LINGANISHA NA US HATA CHEMBE. ANGALIENI JARIDA LA FORBES NIMUONE CURRENT RESEARCH FINDINGS MTASHANGAA, UTAFITI WA 2009 WAMETOA KUHUSU NCHI ZENYE HALI NZURI ZAIDI KIUCHUMI ZA KWENDA, MIJI BORA KIUCHUMI KUISHI KATIKA LISTI HIYO MIJI YA MAREKANI IMEONEKANA NI MIONGONI MWA INAYOLIPA KIWANGO CHA CHINI SANA TENA NA LYFE TIGHT CHICAGO UMEONEKANA NDIO MJI AMBAO WATU WAKE WANA STRESS ZAIDI KULIKO YOTE KUTOKANA NA KUWA NA FRUSTRATION ZA MAISHA MAGUMU!!! , MIJI AGHALI ZAIDI, UTASHANGAA MFAGIAJI. LUXERMBOURG ANAKULA POUND 2000. NA MAISHA HUKO YAKO CHINI KINOMA HAMNA TOFAUTI NA UBELGI9J NA UHOLANZI. HAYO MAMBO YA MAREKANI YAMEPITWA NA WAKATI KUMEBAKI JINA TU SIKU HIZI STATES HAMNA ISHU LYFE IKO TIGHT KINOMA NYIE OMBENI TU HIZO GREEN CARDS MJE MTAISHIA KUSHIKISHWA UKUTA HUKU OHOO. sanasana utajikuta unakaa huku hadi unakuwa mzee unashindwa kurudi home sababu hujazichanga fresh unabaki kuona aibu manake marafiki wote uliowaacha TZ unasikia mambo yao yako juu.
    Mkosa kazi, ATL.

    ReplyDelete
  24. msada jamani, hiyo form ya kujaza naipata wapi? au naandika hizo requirement kwenye microsoft word? halafu ndio natuma au ni vipi jinsi ya kupata form ya kujaza?

    ReplyDelete
  25. Wewe unataka nije huko Marekani kubeba mabox kama wewe. Mambo hapa hapa nyumbani mjomba.

    ReplyDelete
  26. wadau hiyo green card wamarekani wanajidai haina ubaguzi lakini tunajua ina utata. waTZ kibao waliopo Marekani na walio nje ya marekani wanacheza bila kufanikiwa.huwa nashangaa ninapoona eti Nigeria au Kenya watu 4,000 wameshinda halafu TZ watu 300 tu? sasa kama wanaruhusu wanigeria 8000 wanashindwa nini kuchukua waTZ wote waliocheza manake idadi ya waliocheza ni ndogo kuliko hiyo ya nigeria..unless watuambie vigezo ni nini ili watu wengi wachaguliwe manake kama kila nchi ina nafasi sawa then kama TZ wamecheza watu 500 then wachukuliwe wote vile idadi yao ni ndogo kuliko nchi nyingine..naomba kuwakilisha.

    ReplyDelete
  27. GREEN CARD FORM AND PHOTO REQUIREMENTS

    Ukitaka FORM fungua link hii

    http://www.dvlottery.state.gov/application.aspx

    Na kwa maelezo ya picha iweje, fungua link hii

    http://www.dvlottery.state.gov/photo.aspx

    Nawatakia bahati njema

    NOTE: Kumbuka ukishatuma application yako utapewa CONFIRMATION NUMBER, unaweza nakili namba hiyo au print page hiyo na uwe nayo, kwani 1st July, 2010 ndio majibu yanatoka, na unatakiwa kuandika namba hiyo na jina lako la ukoo pamoja na mwaka wa kuzaliwa ili kupata STATUS yako kama umepata au la.

    MAKULILO, Jr.
    www.makulilo.blogspot.com
    San Diego, CA

    ReplyDelete
  28. NI BAHATI NASIBU YA BURE UNAWEZA KUPATA AU KUKOSA UKICHEZA, NI NGUMU KUPATA LAKINI WATU WANAPATA, HAITAJI PESA LAKINI UKIPATA UNAHITAJIKA UWE NA PESA NYINGI HASA KAMA UNAENDA NA FAMILIA YAKO YOTE KWA WALE WENYE FAMILIA NA NI KUBWA, HAMNA PESA ZA BURE KULE UNATAKIWA UJITEGEMEE HADI UTAKAPO SIMAMA VIZURI NINA MAANA UKIPATA KIBARUA CHA KUBEBA MABOX, PIA USIWE NA NDOTO YA MAISHA MAZURI MARA MOJA NI KUPAMBANA SANA NA PENGINE MUNGU AKIKUJALIA UNAWEZA KUFANIKIWA LAKINI INHITAJI BIDII SANA, PIA UKIPATA KUNA PESA ZINAHITAJIWA UBALOZIINI WAKATI WA VISA PROCESS, SO IT IS FREE BUT ONCE YOU WON IT THE MONEY IS NEEDED, SO IN OTHER HAND IT COSTS A FORTUNE ONCE YOU WON IT. BUT USIWEKEE MATUMAINI SANAAAA CHEZA TU KWANI HUJUWI PAHATI YAKO NI LINI KWANI KUNA WATU WAMECHEZA EVERY YEAR FOR MORE THAN 30 YEARS NA HAWAJAPATA HADI LEO HII, BUT IT WORTH IT TRY AS INTIALLY IT DOES NOT COST THE EARTH

    ReplyDelete
  29. acheni kukatisha wenzenu tamaa kama hali ni ngumu mbona nyinyi hamrudi? all in all marekani ni pazuri sana hasa hapo new york city acheni tu maisha ni popote kuna nchi masikini watu wana hela za kufa mtu na kuna nchi tajiri watu masikini kwa sana ni hayo tuuu tena mjitokeze kwa wingi saaaaaaaaana kila la heri
    mdau canada

    ReplyDelete
  30. wewe anym hapo juu kwa nini ukakosa kazi,acha kuponda maana si wote wana maisha kama wewe hapa Usa,acha kukatisha watu tamaa.

    ReplyDelete
  31. To clarify few things: Sio lazima uwe na mtu wa kukupokea huku kama huyo anayesema hapo juu...As long ukishamaliza process zote TZ na kama unavijihela kidogo unaweza kuanza maisha mwenyewe bila kupokelewa na mtu. Noma ni kuwa siku hizi kazi hamna za kuanza maisha hivyo mpaka resume zako zikae vizuri unatakiwa uwe na hela ya kukutough up big time.

    Mimi ni mmoja wao wa walioipata hii nikiwa shuleni huku na ilinirahisishia mambo mengi sana tu.....

    MAONI YANGU kama una maisha mazuri bongo au umekula chumvi nyingi kidogo basi usijaribu hii kitu kabisa....Honesty, siku hizi kama wanahand pick watu kiwin hii kitu na sio random tena kama zamani. Yaani kila anayeipata hii siku hizi ninaona ni watu wazima sana tu na ukija huku mtu mzima eti kuanza maisha ....no good at all my friend....Utaengeza depression na heart attach juu...

    Kama wewe ni kajana na unaona havieleweki TZ na hujaoa/kuolewa this is a golden ticket. Kwa waliooa, walioolewa au una mtoto/watoto its just adding pressure to whatever load you have right now. Mpaka upate maisha uweze kutunza watoto wako bongo itakuchukua miaka mingi sio kama zamani.

    Kuna mtu nimemwona walipata hii na mke wake watu wazima lakini walijirudia nyumbani kabla hawajaadhirika na mwingine yeye aliharibu akauza vitu vyake vyote ili apate nauli ..sasa pa kurudi nyumbani hapaoni.. Professional jobs huwezi kuja huku siku hizi na kuzipata tu kirahisi kama zamani...Zamani ilikua hata hujamaliza shule unakazi yako ya maana tayari lakini sasa hivi hata wanafunzi wa huku kazi hawana hivyo ukija ujiandae kuanza na kuosha viombo, ulinzi au hata kutnza vizee siku hizi...Sasa kama TZ ulikua na kazi ya kushika briefcase, dereva na wafanyakazi wa nyumbani kibao forget about.....Utajipa ugonjwa wa moyo tu waachie wengine wa jaribu bahati yao...


    my cents

    ReplyDelete
  32. hila tufanye yote kwanini watanzania tubakimbia kwetu tatizo hasa ni nini maana wengi wanaotoa mawazo hapa wamesoma kuanzia kidato cha nne mpaka ma PHD sasa km elimu ni mkombozi kwanini tusitumie tukatengeneza tanzania km marekani kwani nao si walianza kama sisi tu
    mi nawaomba sana watanzania tujenge nchi yetu tukishikana tukatoa wale maadui wa mwalimu nyerere UJINGA,UMASKINI,NA MALAZI na kwa sasa UFISADI mi nafikiri tutafika mbali sana na tutaacha mawazo ya marekani,ulaya,uholanzi
    JAMANI WATANZANIA TUBADILIKE KIMAWAZO NA KIMTAZAMO FIKRA ZETU ZIFIKE MBALI EHEE MUNGU SAIDIA WANAWAKO WABADILIKE TUENDELEZE MAENDELEO NCHINI KWETU HILI WATOTO WETU WAJE KUFAIDI KM WANAVYOFAIDI ULAYA NA MAREKANI

    ReplyDelete
  33. PETER NALITOLELAOctober 03, 2009

    MUTAKALIA KULALAMA HAKUNA KINACHOWASAIDIYA. MIMI NAJUTA NILIKUWA CANADA NILIENDA HAPO NILIPO MALIZA MUZUMBE MULOGOLO PALE CHUO KIKUU NIKASOMA CANADA MPAKA NIKAMALIZA MASTERS SASA NIKALUDI BONGO NIKIZANI MAISHA NIMEYAPATIA LOLOLO KUMBE NIMECHEMUKA SASA NINASOTA ILE MBAYA, NAWASHAULI MUKIWEZA CHEZENI HIYO BAHATI NASIBU, MUSIJE KUJUTA KAMA MIMI,

    ReplyDelete
  34. Wabongo kwa kudanganyana bana...Nimetoka huko juzi bongo kwenyewe kumechokaaaaa watu wazeeeee wamechoka wote halafu wanakandia Marekani.Mashida yaleyale toka enzi hizo
    - MAJI NOMAA
    - UMEME MDEBWEDO
    - NZI BWELELE KILA MAHALI
    - KA MLIMANI CITY hata shopping centre ya kijiji USA ni bab kubwa
    - Last but not Least......WABONGO WAMECHOKA SIO SIRI ....WAMEPIGIKA KINOMA.
    Mdau-CHINA

    ReplyDelete
  35. WE MKOSA KAZI WA ATL USIWAKATISHE WENZAKO TAMAA....WAACHE WENZAKO WAJARIBU, WE KAMA MAISHA YAMEKUENDEA VIBAYA SIO KILA MTU....TATIZO ULIKUJA UKIWA UNAFIKIRI KUNA PESA ZINAOTA KWENYE MITI....INGIA SHULE UMALIZE, UONE KAMA MAISHA NI MABAYA HIVYO...AND IF YOU ARE NOT VERY HAPPY BADO UNAWEZA KURUDI NYUMBANI AU UKAENDEA KUFAGIA HUKO LUXENBOURG....NAONA KWAMBA KUFAGIA NDIO SKILL YAKO.....

    ReplyDelete
  36. Na sio kila mtu anabeba Box kuna watanzania wengi wamesomea mambo ya afya registered nursing ,physical therapists, dental assisting n.k na wanalipwa kuanzia 56,000 -70,000 per year na hio ni associate degree tuuu....hata kama utalipa tax lakini maendeleo utayaonahuko Tanzania Tax zenu ziko wapi? Zinashindwa hata kuwalinda ALBINO? VERY SAD.....VERY SAD.....

    ReplyDelete
  37. Maisha sasa hivi merikani magumu
    sasa,mimi nimeishi huku miaka 40
    nilikuwa na kazi nimefanya miaka 30
    sasa narudi bongo,naona kijana toka kenya, miaka 5 bado ni security guard, afadhali tuendeleze
    inchi yetu, amerika siyo kama
    ilivyokua zamani, waafrika tele
    hata pesa ya kurudi nyumbani hamna
    so think grass is always greener
    on the other side till you get there
    Good luck

    ReplyDelete
  38. SYLVIA UMEKAA USA MIAKA 40 NA UMEFANYA KAZI MIAKA 30 NI KIJEBA, UKIRUDI BONGO HUTAPAWEZA UTAPATA PRESSURE TU KAMA UNA MTAJI BASI NENDA OTHERWISE THINK DOUBLE

    ReplyDelete
  39. kila mtu ana maisha yake na mipango yake. wanaotaka kubaki Bongo, wanaotaka
    kwenda marekani au china woote ni mipango yao.

    sawa na wewe uliyahamia mjini Dar,lakini kuna nduguzo wanao amini maisha kijijini ni poa tu.

    MAISHA POPOTE .

    ReplyDelete
  40. ndoto ya mchanaOctober 04, 2009

    Wajameni vipi maisha Australia na New-Zealand yako poa huko?Naomba Watanzania wanaoishi huko watuambie maana kuna green card za kuja huko:)

    ReplyDelete
  41. baba katunzi nimekusoma mwanangu!!! mlimani city bora kashopping centre ka kijiji us teh teh teh. anyway tz vipi kwema?

    ReplyDelete
  42. Ndoto ya mchana New Zealand mambo mswano. Wanataka watu wa profession za karibu aina zote, kuanzia vet hadi nurses. Waingereza wajanja na hata wamarekani wazungu wanahamia huko. Australia nako kumekuwa kimbilio la wamarekani, maisha swafiiii wanajibwaga. Shemeji yangu mmarekani mweusi mwaka jana kakimbia US kwenda New Zealand kapata kazi nzuri na tayari keshachukua mke na watoto kwenda New Zealand.

    Mie nimeishi US, maisha ya sasa sio kama zamani nilipofika 1980s. Iwapo mtu una kazi nzuri bongo na biashara zako nzuri nakusihi usijaribu US. Kama bongo huna biashara yoyote ya maana na kazi nzuri jaribu bahati yako US. Uzuri wa bongo ukiwa na kajumba kako umejenga, na kazi yako huku vibishara vinakusukuma usijaribu kabisa kuja US hivi. Endelea hapo hapo ulipo. Kuna watu wamefika US wanajuta kuwa TZ walikuwa na kazi na biashara zenye msimamo wakati hapa maisha ni mchakamchaka hadi usiku mwisho wa mwezi ukifika pesa yote yaishia kwenye bills. Wazungu wenyewe sasa wanakimbia makwao na kwenda Asia, Caribbeans, south America & south Africa.

    ReplyDelete
  43. AnonymousJuly 12, 2015

    TAFADHALINI WALE WOTE AMBAO WAMEPATA/ WAMESHINDA DV LOTTERY TANGU IANZE WANA STORIES TOFAUTI. WAKO AMBAO WANAJUTA, NA WAKO AMBAO WAMEFAIDIKA. WALIOFAIDIKA HAWATASEMA, WATAWEKA SIRI. WALIKUJA HUKU USA WAKIWA MADAKTARI, MANESI, WALIMU, MAPROFESSOR, WASOMI WENGINE, SASA WANABEBA MABOKSI. WAKO AMBAO WAMEJIINGIZA KATIKA ULINZI SECURITY GUARDS. KAMA UMESHINDA DV LOTTERY, NA UNAMIAKA 50YRS NA KUENDELYA NA UNAFAMILIA, TAFADHALI JIREKEBISHE UWAZE, KUWA AMERICA SIYO MAHALI PA MZAHA, UTALIYA, UTAUGULIWA, NDUGU TANZANIA WATAFARIKI, WEWE UKO US HATA NAULI YA KWENDA TANZANIA HUNA....PLEASE BE CAREFUL. THIS IS AN ADVICE FROM PEOPLE WHO ARE ASHAMED TO SPEAK THE TRUTH. AMERICA NEEDS LABOUR MARKET, NURSING AIDES...UTWAOSHA WAGONJWA UKIWA NA DEGREE YA UDAKTARI. UTAENDESHA TAXI UKIWA PRFESSOR, AMERICA INAJUWA KUWA MSOMI ATAFANYA HIZI KAZI KWA UAMINIFUU NA BIDII KAMA HUKO KWAKE ANAKOTOKA AKIWA DAKTARI,MWALIMU, PROFESSOR, NESI....AMERICA KUMETAWALIWA NA WASOMI KUNDI LA "JEWS" AMBAO NI 99% KATIKA USA GOVT ADVISORY COMMITEE. HAPO KALE WATUMWA WALITIWA MINYONYORO KULETWA AMERIKA KUFANYA KAZI. LAKINI SASA UTUMWA WA HIARI BILA MINYONYORO, UTALIYA, UTAJUTA, UTATAMANI KURUDI BONGO. LAKINI HUWEZI KWANI WENZAKO WATAKUZARAU...ATI UNATOKA AMERICA, HATA GARI HUNA? WENZETU WATANZANIA AMBAO WAKO SAUDI ARABIYA, DUBAI, MUSCAT NA NCHI ZINGINE ZA ULAYA WANAENDELEYA NA WANAWEKEZA TANZANIA KUSHINDA YULE AMBAYE AMEPATA "DV LOTTERY GREEN CARD" TAFADHALI SANA, USIKIMBILIYE MILIMA AMBAYO KWA MBALI HUONEKANA KIJANI NA YENYE MAUA MAZURI, UKIFIKA KWENYE HIYO MILIMA, KUNA MASHIMO, MATOPE, MIIBA NA NJIYA YA KURUDI UMESHAPOTEZA. KWA UFUPI, AMERICA LOOKS BRIGHT, LAND OF OPPORTUNITY FROM FAR, BUT IF YOU ENTER AND SEE FOR YOURSELF, YOU WILL FEEL THE PAIN!!!!!!!!!!!!!!!!!BE CAREFULL, THOSE DAYS ARE OVER!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...