jana usiku kulikuwa na dhifa iliyoandaliwa na Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA) katika hoteli ya New Arusha ambapo kulikuwa na mnuso na dansi. Juu mjumbe toka Maldives akishukuru zawadi aliyopewa na Rais wa CPA na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samwel Sitta, baada ya kutoa burudani ya kuimba wimbo wa 'Malaika' kwa ustadi mkubwa. Shoto ni kaimu Mkurugenzi mkuu wa Consolidated Holding Corpration, Bw. Methusela Y. Mbajo ambaye ndiye aliyefadhili hafla hiyo, akifuatiwa na Mwenyekiti wa PAC tawi la Tanzania, Dk. Raphael Chegeni na Mh. Sitta.
Kiongozi wa upinzani katika bunge la Bermuda amezidi kuwa kivutio sio tu kwa pamba kali bali pia kwa kupenda kulisakata rhumba. Hapa anayarudi mangoma ya Bob Marley ya 'One Love'
meza kuu. Shoto ni Mh. Anna Abdallah ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kinamama ya PAC, Bw. Methusela Y. Mbajo, Dk. Raphael Chegeni, Mh. Sitta, na viongozi wengine wa PAC
baada ya msosi libeneke..
wajumbe wa mkutano wa 55 wa CPA katika hafla hiyo
Mwenyekiti wa CPA tawi la Tanzania Dk. Raphael Chegeni akihutubia
Mh. Chegeni akionesha moja ya zawadi ambazo CPA Tanzania ilitoa kwa kila mjumbe
wajumbe wakifurahia zawadi
baadhi ya wahudumu katika mkutano huo









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mh! namuona Anna Makinda hakauki pembeni ya mzee wa Bermuda i suspect ajuza anazimia legs za mzee kibukta.

    ReplyDelete
  2. We Michu uko kazini au uko vekesheni? mimi najua ukiwa vekesheni unapumzika hufanyi kazi!

    ReplyDelete
  3. truly tanzanian, I like the hospitality.

    ReplyDelete
  4. We mtoa maoni wa kwanza uwe na adabu! AJUZA MAMA YAKO!Ajuza mkeo!Ajuza dada yako!

    ReplyDelete
  5. looks extravagant. money would have been better spent elsewhere......anyway priority yao ni ku-impress wageni.

    ReplyDelete
  6. acha hizo wewe picha moja tu kutokea pamoja ndio unasema hakauki?!

    ReplyDelete
  7. alovaa kimasai ndo kusema anadumisha ya waziri Pinda tusivae suti za kithungu?

    ok

    ReplyDelete
  8. kila siku vikao vya kipuuzi na hakuna mabadiliko africa zaidi ya njaa na mateso...vikao vya ngono hivyo kwa wabunge.mdau money.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...