Bra Michu!!
Hapa mie nimikwama… kuhusu hili la sherehe za kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu JK Nyerere.
Hakika tunapatwa faraja kubwa sana kitaifa kwa hili la sherehe za kummbukumbu za historia ya Mwlimu JK Nyerere na siyo kwa kumbukumbu ya kifo chake.
Maana vinginevyo ingelikuwa bora na vyema zaidi kusheherekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake na si kifo chake.
Kiswahili ni lugha pana na ni tajiri wa maneno hivyo kwa msemo safi zaidi ingelikuwa ni sherehe za kumbukumbu za historia ya Mwalimu miaka kumi baada ya kifo chake.
Tunaendelea…. kwa kurudi nyuma!
NDUGU WATANZANIA, ni jambo ambalo limenishangaza, limenistaajabisha na kunisikitisha, kwamba, baada ya miaka 10 ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, badala ya kusonga mbele na kumuenzi kwa vitendo, bado tunaomboleza.
NDUGU WATANZANIA, ni jambo ambalo limenishangaza, limenistaajabisha na kunisikitisha, kwamba, baada ya miaka 10 ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, badala ya kusonga mbele na kumuenzi kwa vitendo, bado tunaomboleza.
Katika maisha yake – nasisitiza MAISHA YAKE – Mwalimu alikuwa mtu mwadilifu, aliyependa usawa, aliyepinga ubaguzi, ulaji rushwa, ubinafsi, upendeleo, na kila aina ya ufisadi ambao sasa unatukuzwa na kugeuzwa kuwa “msahafu” maalum wa Kitaifa!
Juzi, Jumatano, 14 Oktoba 2009, Watanzania walipumzika nyumbani mwao, wengine walizuru sehemu mbali mbali, baadhi walikuwa Butiama, nyumbani kwa Mwalimu, wakiadhimisha kumbukumbu ya miaka kumi ya KIFO cha Mwalimu! Walimkumbuka Mwalimu na yale yote aliyoyafanya wakati wa uhai wake – jambo zuri sana – lakini pia, walisisitiza kwamba hii ilikuwa kumbukumbu ya KIFO cha Mwalimu!
Najiuliza. Utamkumbukaje mtu muhimu kama Mwalimu, kwa yale aliyoyatenda wakati wa MAISHA yake, kwa KIFO chake? Hata kama kuna ulazima wa kumkumbuka, basi, tarehe ile ile ambayo alituaga, tuitumia kwa kukumbuka MAISHA yake, si KIFO chake! Badala ya kusema tunaadhimisha kumbukumbu ya KIFO cha Mwalimu, tuseme, tunaadhimisha kumbukumbu ya MAISHA ya Mwalimu.
Kwa mtazamo wangu, kumbukumbu ya kifo, kwa kweli si jambo zuri hata kidogo. Si jambo chanya, ni jambo hasi. Waislam huwa tunasoma Hitma, lakini si sawa na kumbukumbu, bali ni kuwaombea dua waliotangulia mbele ya haki, Mola awarehemu, awaepushe na adhabu, awalaze pema, awasamehe makosa yao. Unapokuwa unakumbuka kifo cha mtu fulani unakuwa kama hutaki kukubali kwamba, mosi, mtu huyo hayupo duniani, na pili, unakuwa bado unaomboleza, hutaki kumwacha aondoke.
Watanzania wengi bado hawajaamini kwamba Mwalimu hayuko nasi. Hawaamini kwamba – kila wanapomwona akihutubia kwenye picha za kumbukumbu kwenye runinga – hayuko hai. Wanadhani kwamba bado yu nasi.
Tukubali kwamba, mosi, Mwalimu hayuko nasi, na pili, tutamkumbuka tukiyaenzi matendo yake wakati alipokuwa HAI, na si kukumbuka au kuadhimisha KIFO chake! Haya ni makosa!
Ningependa, kuanzia sasa, tuanze kuandika kwenye mabango hayo yetu: Kumbukumbu ya Miaka Kumi na Moja ya Maisha ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mdau dRU
Botswana
Well presented, hope authorities would give it required consideration.
ReplyDeletewataka kuweko sherehe ya nyerere day ama presidents' day sawa na hali ilvyo huko marekani.
ReplyDeleteMdau wa haja ya hoja ninaomba nikusahihishe kidogo. Mwalimu hayupo nasi kimwili lakini kwa mengine kama machapisho, hotuba zake na mafundisho mengine bado yupo nasi, ndiyo maana tunazisikiliza hotuba na kusoma vitabu alivyoandika. Ingawaje viongozi wengi hawafuati aliyokuwa akiyasimamia. Wanataaluma/wanafalsafa wanaamini kuwa unapofariki hauondoki na kazi zako bali zinaendelea kusomwa na vizazi vilivyobaki, hivyo haufi kitaaluma/kifalsafa.
ReplyDeleteNami nilikuwa na mawazo haya haya ya Hoja ya Haja, lakini mwenzenu huwa nashindwa kuyapanga yakapangika na kueleweka sawasawa kama alivyofanya huyu mdau wa Botswana kwa Watswana.
ReplyDeleteSijui niwalaumu Wazazi kwa kutonipeleka shule au niilaumu nafsi yangu kwa kutoweza kupangilia hoja muhimu!!!!!!!!!!!!!!
Mdau Matari hadi umefika Ohio inatia shaka kama hujasoma-kama unavyosema. Ilaumu nafsi yako na ujilaumu mwenyewe kwa kutojishughulisha katika ufikiri wako. Na uwashukuru wazazi wako kwa kukuleta duniani hadi ukafika huko ulipo.
ReplyDeleteHii ni hoja ya akili sana na ukweli mtupu. Natamani muandishi akafanya utafiti mdogo wa jinsi ya kuwasiliana na watu wa Mwalimu Nyerere Foundation - nadhani ndo wanaweza kufanya na kusimamia badiliko hilo muhimu kwa uma na vyombo vya habari. Point nzuri sana na muhimu. Isiishie hapa kwa michuzi tu
ReplyDeleteNamuunga mkono mdau wa Botswana, kuwa Tarehe 14 ya Oktoba kila mwaka iwe Siku ya Kukumbuka Maisha ya Mwalimu JK Nyerere.
ReplyDeleteHii itaondoa 'uchama' na siku hiyo kuadhimishwa 'kiaina' wanavyopenda wale wasiopenda kusikia maono ya Mwalimu kwa vitendo.
Siku hiyo ikiwa Kumbukumbu ya Maisha ya Mwalimu, itatusaidia kutosahau dhana ya umoja wa kitaifa, taifa kujitegemea, utu, na kuwa maadui wetu mpaka sasa ni njaa, ujinga, maradhi.
Pia Kumbukumbu ya Maisha ya Mwalimu inatukumbusha pia ili Tanzania iendelee inahitaji watu(watanzania), ardhi, siasa safi na uongozi bora.
Pia Kumbukumbu ya Maisha ya Mwalimu inatukumbusha kuwa 'Rushwa ni Adui wa Haki na kuwa Sitatoa Rushwa wala Kupokea Rushwa'
Pia itatukumbusha kuwa 'Tujisahihishe ' pale ambapo tumeshindwa kupafikia.
Pia Uongozi ni Kujitolea na sio sehemu ya kujinufahisha kwa dhamana tuliyopewa na Watanzania wote.
Mungu Ibariki Afrika, Ibariki Tanzania na Watu Wake.
Mdau
Arusha
MDAU TATIZO LAKO NI HIYO HEADING AU MAAZIMISHO YENYEWE, KAMA HEADING HAINA TATIZO WALA MAADHIMISHO YENYEWE PIA HAYA TATIZO YOTE UNAYOYASEMA NDIYO YANAYOFANYIKA KATIKA SHEREHE HIZO. HATA KATIKA JAMII ZETU WATU HUFANYA MISA MAKANISANI NA SALA MISIKITINI KUWA KUMBUKA NDUGU ZETU WALIOKUFA, WATU WANPIKA NA MAPLAU KATIKA KUMBUKUMBU HIZO NA KUTOWA MAELEZO JUU YA MTU WANAMKUMBUKA, MIMI NAONA HUNA HOJA YA MSINGI KWANI YOTE ULIYOYAELEZA NDIYO YANAFANYIKA, NA KILA MTU NA HULUKA YAKE KAMA HAWAFUATI MAFUNDISHO YA MWALIMU THAT IS NONE TO DO WITH NYERERE DEATH CEREMONY
ReplyDelete09:06:00PM ACHANA NA KIINGEREZA HAKUNA KITU KAMA THAT IS NONE TO DO WITH NYERERE DEATH CEREMONY, SIJUI NA HILI UTASEMA HAKUNA TATIZO? BY THEWAY WEWE NI KANUMBA au kati ya wake mawaziri sita wenye vyeti bandia?
ReplyDeleteMimi ni Mdau wa lugha, kwanza nakupongeza mtoa hoja kwa kuliona hilo kuwa lina upungufu wa mtazamo na pili namna ambavyo tunadhani tunasheherekea kifo ambalo ni kosa. Kama ningepewa mamlaka ya kupendekeza siku hiyo tuiteje basi ningesema iwe " SIKUKUU YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE" Nimeipenda hoja yako
ReplyDelete