Jengo jipya la ituo cha sanaa na utamaduni cha Culture Heritage jijini a-taun kwa ndani. ghorofa tatu zote ni sehemu ya kuoneshea kazi za sanaa na utamaduni
mgeni akipozi mbele ya kinyago cha kimakonde ambacho ni kikubwa kuliko vyote vilivyopata kuchongwa kutoka katika shina moja la mti
madhari ndani ya kituo hiki
wageni wakishangaa kinyago cha kimakonde
sehemu ya chini ya taswira ya ngao uionayo ukipita kwa nje

bustani murua zimezunguka kituo hiki
lango kuu lenye nakshi nakshi toka zenji
sanamu za mifugo na wanyama zimezagaa kile kona
sehemu ya ndani ya jengo la zamani

Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha sanaa na utamaduni wa Mtanzania cha Culture Heritage, Saifudin Khanabahi, akiwatembeza wageni katika jengo jipya la kituo hicho lenye nafasi la mita za mraba zaidi ya 30,000 na litapofunguliwa kabla ya mwisho wa mwaka huu litakuwa ni kituo kikubwa cha sanaa na utamaduni wa Afrika bara zima, kama si dunia yote
jengo jipya la Culture Heritage lina mambo mengi mapya ikiwa ni pamoja na ukumbi wa kisasa wa sinema na maonesho ya jukwaani kwa ajili ya kuonesha utamaduni wetu kwa wageni










anko nanihii alitembelea kituo hicho leo











kituo kinavyoonekan kwa ndani














Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. weka picha zaidi maana nakiskia tu hiko kituo cha utamaduni!

    ReplyDelete
  2. ako nanihii mbona hilo sanamu lipo uchi wa mnyama?

    ReplyDelete
  3. ni ishara ya kutunza utamaduni wa mtanzania na mwafrika pia. ee bwana inapendeza kinoma, ila yaliyomo yaendane kweli na mtanzania.

    ReplyDelete
  4. Ningekuwa huyo mmasai ningekushitaki, Michuzi...

    ReplyDelete
  5. Safi Sana,

    This is what I Like To See, Sasa OWNER ni Mzawa au mgeni!?

    SzB.

    ReplyDelete
  6. Bravoooo sasa hii kitu ijengwe katika mikoa mbalimbali ili kuhifidha local mila and arts za sehemu hizo

    ReplyDelete
  7. owner ni mpakistan anaitwa seif

    ReplyDelete
  8. michuzi wahisani wanataka mkapa apelekwe mahakamani kujibu mashtaka ya ufisadi, na wewe umeanza kufanana na mkapa (kitumbo) itabidi ufuatilie!!! take that to the bank mother++f

    ReplyDelete
  9. THANK YOU BRO MICHUZI, kazi yako nzuri tunashukuru kutuonya hilo jendo zuri sana

    ReplyDelete
  10. Mjomba Uncle Nanihii, haya ndio mambo tunayotaka yaendelee Bongo, sio siasa tu. I am thrilled +) FirePower, UK

    ReplyDelete
  11. Je architecture ni mzawa au...Jina lake tungelipewa basi...jengo limetulia sana na nikikumbuka mandari ya Arusha moyo unanisisimuka

    ReplyDelete
  12. HI! Bro' nimefurahi sana kwa picha nzuri hiyo inaonyesha kiasi gani na sisi tunaweza ila tupunguze umimi na ufisadi TUIJENGE TZ yetu.
    Sasa hilo jengo ni la Serikali au Mtu binafsi au Ngo's? hapo tu sijaelewa.
    RUSHWA NI ADUI WA HAKI!

    MUNGU IBARIKI TZ
    MUNGU IBARIKI AFRIKA

    ReplyDelete
  13. This is awesome

    ReplyDelete
  14. Mannnn Kukaya muswamu ile mbaya, umenikumbusha mbali Bro. Mathupu nipigie picha za mitaani A-Tauni hasa maeneo ya sakina, majengo, ngarenaro na kijenge nataka kuona hiyo mitaa inaonekanaje kwani niliondoka miaka 15 iliyopita nina twasira tofauti kabisa kichwani mwangu! Nimefurahi sana kuona hayo maendeleo ya mji wangu wa Arusha!
    KAzi nzuri Mathupu na manyama kulaaa!

    ReplyDelete
  15. Tatizo ni kwa lazima kitakuwa under uwekezaji, maana nikiangalia tu mkurugenzi nahisi kituo ni cha wawekezaji, yaani kama ni hivyo ni aibu tupu kwa wizara ya utalii kushindwa kufanya hilo wenyewe.

    ReplyDelete
  16. Nani anamiliki?Serikali???Ama?Nanihii?

    ReplyDelete
  17. Anonymous Thu Oct 01, 11:09:00 PM

    Afadhali usimjue owner kwa sababu ukimjua utakasirika. Mambo yaliyomo umo ndani utafikiri Anthropological artifacts ya enzi za kina Magreth Mead. Upuuzi mtupu!

    ReplyDelete
  18. Michu,nataka kujua mkuu,hili jumba na vitu vyake ni mali yetu SOTE au ni la mtu mmoja????maelezo pls

    ReplyDelete
  19. Nafurahi sana kuona mambo mazuri kama haya yakifanyika nyumbani. Ni ubunifu mzuri na wa kuigwa.
    Pia ndugu zetu wahindi siku hizi wameacha kuogopa kujenga. Maana zamani walikuwa wanasema hawataki kujenga kwasababu watamjengea Nyerere.

    ReplyDelete
  20. mambo ya fwedha michuzi, naona mwendo na upigaji wa picha hapo chini mkono mfukoni.

    ReplyDelete
  21. mamaaaa culture...wow.....

    ReplyDelete
  22. mzee wa libeneke

    ebu jibu dukuduku letu umu ndani sio watangaza tuu ilhali mtu/mgeni akikuuliza who owned that?govt or a person?macho yatutoke

    MJENGO WA NANI?

    ReplyDelete
  23. Jamani eh mmiliki ni mzawa ambaye ni Mtanzania kabila lake ni mpakistani. Mimi natoka Arusha huyo jamaa anaitwa seifu. Ni mswahili na ni mtoto wa mjini Arusha. So? Let us be proud

    ReplyDelete
  24. TUWE WA KWELI KAMA JAMAA ASINGEJENGA JE NI MTU GANI ANGEFIKIRIA HIVYO KUTENGEZA SEHEMU YA KUVUTIA WATALII, ILA JAMANI TUACHE UPUMBAVU WA KUSUBURI MTU ABUNI NA KUANZA KUKOSOA SANA BILA SABABU, NA SISI TUJARIBU PIA KUBUNI VITU VYETU PIA ILI TUWEZE KUPIKU WATU MBALI MBALI NDIO MAENDLEO HAYO, TUACHE CHUKI ZISIZO JENGA ILA MUWE HURU VILE VILE KUKOSOA.

    ReplyDelete
  25. Wa TZ ttz tunapenda siasa nyingi na umbea, eti nani kajenga? ina maana hakuna vyombo vinavohusika na uwekezaji TZ kutoa kibali!! cha kwanza tungeuliza mtu wa chini anafaidika vipi na uwekezaji huo,hakuna hata mmoja aliyeuliza hilo kati ya maoni yote hapo juu!! UPEO MDOGO,HATUNA WIVU WA MAENDELEO,kwa uwelewa wangu nia mojawapo ni kutangaza na kuingiza mapato. Ajira kwa watengeneza vinyago, nk!
    1.JE MTANZANIA ANAFAIDIKA VIPI? AMA BADO UAGIZAJI WA VINYAGO KUTOKA NCHI NYINGINE UNASHAMIRI (Kenya nk).
    2.MJI WA ARUSHA UTAFAIDIKA VIPI KUPITIA BIASHARA HIYO(MAPATO), BARABARA,HOSPITAL,ELIMU(SHULE ZA MSINGI)?
    AKIMILIKI WAKUJA,AMA MZAWA,AMA SERIKALI SIO HOJA, Michuzi tufanyie utafiti plz!

    ReplyDelete
  26. Hivi mchongaji wa sanamu ya jamaa wa kimasai aliishiwa na gogo la mti wa mpingo kabla ya kumalizia kazi?

    Kama ni hivyo basi Cultural heritage waombe kibali maliasili wapate kibao cha mpigo wamalizie rubega ya jamaa yetu huyo.

    Ni vizuri kituo hiki kuhakikisha kazi zinazoonyeshwa ktk kituo hicho ni za kiwango cha juu kabisa, ili dhana ya kuwa kuvutio cha kimataifa kifikiwe.

    Mdau
    Lotagolieki Mollel.

    ReplyDelete
  27. Kwa taarifa yenu the last time President Clinton came to Arusha alifika hapo lakini jengo hili lilikuwa bado halijakamilika alinunua vinyago vya thamani ya dola 1 millioni. Wallahi sitanii. Nmzigo ulikuwa heavy haswa ukabebwa na ndege iliyokuwa inaisindikiza Airforce One. Mpaka TRA walipata kizungunzungu.

    Mwacheni Seifu bwana anaujenga uchumi wa Arusha. Na kule sehemu za njirio karibu na uwanja wa nane nane wamejenga pia a shopping centre ambayo ni kivutio kizuri cha A town. Sema tu katikati ya jiji hilo hakuna miundombinu mizuri. I wish A town was Moshi. Maana Moshi layout yake ni super

    ReplyDelete
  28. Huyu jamaa mwenye mali ni mtoto wa mjini kazaliwa na kukulia na kusomea hapo hapo Arusha nafahamu familia yake ni watu wema sana na yeye jamaa ni mchapa kazi hasa.
    I'M PROUD OF HIM

    ReplyDelete
  29. Sasa mara mpakistani...mara mtanzania...inakuwa vipi hiii????a

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...