Watu wanne wamekamatwa na polisi baada ya kukutwa wakiuza samaki wanaodhaniwa kuwa wamevuliwa kwa njia haramu za uvuvi. Mh. Mwandosya amesema wakazi wa jiji la Dar wasiwe na wasiwasi wowote na waendelee kutumia maji hayo kwani uchunguzi wa kina umefanyika na kugundua kwamba hakuna sumu yoyote ambayo imepatikana katika chanzo cha mtambo wa Ruvu juu ambako ndiyo husukuma maji kuja jijini.
Profesa Mwandosya Amesema eneo ambalo tukio hilo lilitokea ni sehemu iitwayo Kwala katika Wilaya ya Morogoro Kusini, akiongezea kwamba inaaminiwa lilitiwa sumu kwa lengo la kuvua samaki na wavuvi haramu umbali wa kilomita 70 kufikia kwenye chanzo cha mtambo wa Ruvu Juu.
Amesisitiza kwamba hakuna wasiwasi wowote wa kuwepo kwa sumu hiyo na mpaka sasa Sampuli ya maji iko kwa mkemia mkuu ili kubaini kama kuna tatizo lolote pamoja na kwamba uchunguzi wa awali umeonyesha hakuna aina yoyote ya sumu katika maji hayo.
kama ni kitu A muwe mnasema A sio ohh ta ta ta, muwe wa kweli.
ReplyDeleteHivi hiki cheo cha umwagiliaji..kuna mashamba mangapi Tanzania ya Umwagiliaji mpaka Waziri anapewa hiyo title? Mhh duniani kuna mambo...hili nalo ni mojawapo...!!
ReplyDelete