Dear Bro Michuzi,
Please msaada tutani, gari inauzwa, bei maelewano.
Description ya Gari:
Used Toyota IST recently from Japan, almost new:Engine: 1498 CC, 5 doors, TV + DVD, voice navigation, Year 2002, alloy wheel, (registered and 3rd party insured)
Call: +255 755 788 486

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Yeah, tunaona iko registered Japan.....(kuna hatari ya kununua gari ambayo iko kwenye yard Japan). "Na bado ni mpya" - ni ya 2002. Je, ya 2009 utaaitaje?

    Sema bei sasa...

    ReplyDelete
  2. Sasa si utuwekee picha ya registration ya Tz au? Na ya yard ya Tz badala ya Japan? Ninaweza kuwa imepata ajali wkt wa kisafirisha na hali yake ikawa tofauti na ya sasa. Au unataka tununue huko huko Japan ndio usafirishe?

    ReplyDelete
  3. Bei gani?

    ReplyDelete
  4. MIE NILIVYOELEWA NI RECENTLY FROM JAPAN DAT MEANS IPO TZ ...Na haina muda tangu ije kutoka Japan kisichoeleweka ni nini???..hivi kweli utanunua gari bila kwenda Fundi wa kukuchekia engine na kila kitu??? hata kama gari imetoka 1990 kama haijawahi kutumika unaiita ni mpya bado amemaanisha mpya kwa mtazamo huo...2002 Ni mwaka ambao
    imetoka hiyo gari .....Weka bei kwanza hapa hapa maelewano ndo nikupigie.

    ReplyDelete
  5. Wewe anony wa Tarehe Sun Oct 04, 01:16:00 PM,

    Ni wewe mwenye gari nini? Hiyo tafsiri yako ya mpya nayo ni mpya. Gari ya 2002 imezeeka hata kama haijawahi kuingia barabarani. Huna habari kuwa gari ni vyuma ambavyo vinazeeka kadri muda unavyopita. Tena bora inayopashwa moto kuliko inayokaa tu.

    Pili, number plate hiyo ni Japan (ukibisha labda hujawahi kufika Japan). Bahati mabaya siyaoni maandishi ya juu ya namba kwenye kibao. Ningeyaona ningekwambia ni prefecture gani Japan iko registered. Km gari ina registration ya Tz kwa nini tusiwekewe ya Tz? Something fishy...kalagabao.

    ReplyDelete
  6. Hiyo voice navigation utaitumia mitaa ya sinza kweli?

    ReplyDelete
  7. we muuza gari naona unataka kutuuzia mbuzi ndani ya gunia !!! kama huna cha kuficha kwanini usituambie hiyo bei yako ? Halafu kama ni maelewano basi yafuate baadaye...kama hujuwi jinsi ya kutangaza bidhaa yako mtandaoni basi nadhani ungewatafuta wanaojua wakufahamishe vizuri.Good luck!!

    ReplyDelete
  8. Gari huwa haisafirishwi kwenda nchi nyingine ikiwa na namba za nchi nyingine. Km iko Tz basi weka picha yenye namba za Tz... Simple! Sasa unasema iko registered Tz halafu unatuonyesha registration number ya Japan. Wapi na wapi hiyo...

    ReplyDelete
  9. BISHOTE WICHITAOctober 04, 2009

    SASA WEWE MUDAU HAPO JUU KAMA UNAELEWA IPO DAR UNATOA COMMENTI YA NINI? YAANI VICHWA VINGINE SIJUI MADUDU GANI YAPO KICHWANI YAANI KILA KUKICHA YANAANDIKA PUMBA TU. SIJUI YAMEISHIA KIDATO CHA PILI CHA FORM TWO FAILURE TUSEMEGE?

    ReplyDelete
  10. weka bei tuangalie uwezekano wa kununua au kuongezea kidogo pesa, sasa tufanya makubaliano kivipi wakati bei sijui, nikisema nina million 2 utakubali?

    ReplyDelete
  11. Poleni wadau kwa usumbuvu bei mya gari ni million 4 tu. haya mnasemaje?

    ReplyDelete
  12. Nimepunguza sasa. Million 3. Mnasemaje sasa?

    Wenu muuzaji (Haji)

    ReplyDelete
  13. dah inaelekea hiyo gari si nzima,ndani ya masaa mawili imepungua bei.....kadanganye wengine humu hupati mtu!!!

    ReplyDelete
  14. Voice navigation Kariakoo?????

    ReplyDelete
  15. Bei ya jumanne.. Milioni 2 za kizimbabwe.. Haya mnasemaje sasa?

    ReplyDelete
  16. Hiyo navigation yako hapa bongo haifanyi kazi. Kwa bei hiyo humpati mtu ng'ooo.... kanyaboya ndani ya gunia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...