KIGODA CHA TAALUMA CHA MWALIMU NYERERE
CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
MBONGI (PALAVER) WA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
MADA: MIPASUKO [FAULT LINES] KATIKA JAMII YETU
CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
MBONGI (PALAVER) WA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
MADA: MIPASUKO [FAULT LINES] KATIKA JAMII YETU
TAREHE: 13 OKTOBA 2009
MAHALI: UKUMBI WA NKRUMAH,
CHUO KIKUU MLIMANI
SAA: KUANZIA 9.00 MCHANA
WOTE MNAKARIBISHWA
___________________________________________
Katika vyombo vya habari, mijadala mbalimbali na hata maongezi ya kawaida, wananchi wanahisi na wanasema kwamba mshikamano wa kitaifa na wa kijamii umepungua sana katika nchi yetu, haswa katika miaka ya hivi karibuni.
Ni dhahiri kwamba hisia hizo sio za kubuni bali ni dalili za hali halisi. Au ni hisia tu? Ishara moja wapo ya mipasuko hii ni malumbano ambayo tumeanza kushuhudia kila siku katika magazeti yetu na hoja na misimamo mbalimbali ya kisiasia na wanasiasa. Au hayo sio malumbano bali ni mijadala tu ambayo ni muhimu iwepo katika mfumo wa kidemokrasia?
Tumeshuhudia malumbano kuhusu muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hii ni dalili mojawapo ya mpasuko wa ki-nchi na wa kitaifa. Je, ni kweli, kwa sababu matatizo ya muungano ni ya muda mrefu tu?
Tumesoma na kusikia malumbano ya kidini na pia tumeshuhudia baadhi ya wasomi, wanahabari na wanasiasa wakijenga hoja zao kwa kuegemea dini.
Au hii ni sehemu ya uhuru wa kimawazo tu kwa hivyo haina ubaya wowote?
Au, kwa vyovyote vile, si jambo geni kwa sababu huko nyuma mawazo kama haya yalikuwepo bali hayakuzungumziwa kwa uwazi? Tumekuta baadhi ya wanasiasa wakitumia ukanda kuwashawishi wananchi.
Na pia tumesikia wengine wakitumia tofauti za kabila na ubaguzi wa rangi kama kisingizio cha kujitafutia mashabiki. Ukweli ni kwamba ule mshikimano wa kitaifa na kijamii ambao tulizoea katika miongo miwili ya baada ya uhuru umedidimia kwa kiasi kikubwa.
Au hoja hizi ni za watu wachache amabo ni wafuasi tu wa mfumo wa uhodhi (monopoly) wa kiasiasa na kimawazo?
Lengo la Mbongi huu ni kujadili masuala haya kwa uwazi, ufasaha na kwa undani ili kubainisha vyanzo na chimbuko la mipasuko hii. Kama ilivyo kawaida katika mijadala, sio washiriki wote wakubaliane. Ndio maana ya kujadili. Jukumu la Mchokozi Mkuu (chief interlocutor) ni kuibua masuala mbalimbali ili kuchochea mijadala.
Je, ni kweli kwamba jamii yetu ina mipasuko au hizo ni hisia tu za watu wachache? Kwani kuna ubaya gani watu kujitambulisha kwa misingi ya dini zao, makabila yao au ukanda wao? Na kama kuna ubaya, ubaya hasa uko wapi? Katika medani ya siasa au ya kijamii? Miongoni mwa wananchi wenyewe au wanasiasia na viongozi?
Nini ni chimbuko la mifarakano hii na nani awajibike? Wapi tutafute chimbuko na vyanzo vya mipasuko? Katika mfumo wa kisiasa, kijamii au kiuchumi? Je, mipasuko hii ina uhusiano wowote na mfumo wa uchumi, hususan, mgawanyiko wa kitabaka katika mfumo wa uzalishaji? Na je kuna uhusiano wowote kati ya tunachoshuhudia katika jamii yetu na uhusiano wetu na mataifa ya nje au jinsi tulivyoingiliana na mfumo wa utandawazi?
Nini kifanyike ilituweze kuepukana na madhara ya mipasuko hii? Tuanzie wapi? Mfumo wa elimu, utamaduni au mfumo wa kisiasa? Na nani mwenye jukumu la kuchochoea utafutaji wa dira mpya itakayoleta mshikamano?
Je, unaweza ukawa na mshikamano wa kitaifa bila kujali mgawanyiko wa kitabaka? Mgawanyiko kati ya matajiri wachache na mafukura wengi?
Nini jukumu/wajibu wa wasomi na wanazuoni katika hali kama hii?
Nini jukumu/wajibu wa wasomi na wanazuoni katika hali kama hii?
MIPASUKO KATIKA JAMII YETU
TAREHE: 13 OKTOBA 2009
MAHALI: UKUMBI WA NKRUMAH,
CHUO KIKUU MLIMANI
SAA: KUANZIA 9.00 MCHANA
WOTE MNAKARIBISHWA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...