Wadau kunradhi,
Inaelekea kuna mdau aitwaye Shamsa Diwani ameshaibiwa email address yake pamoja na password, na sasa wezi hao wanawaandikia wote walio katika orodha ya mdau Shamsa kuomba msaada wa pesa.
Hii ni kanyaboya na sio kweli, kwani ukimjibu kwa kiswahili anapata kigugumizi ama hajibu. Mie nimeipokea leo nahisi ni vyema nikawatahadharisha wote wanaojuana na mdau Shamsa.
Email yao ni kama ifuatavyo hapo chini, ukiletewa ipuuze na ipige 'spam' na wewe mdau Shamsa fungua email ingine, na pia ripoti kwa wahusika wizi huo.
-Michuzi
----------------------------------------------------------------------------
Am in a hurry writing you this note,Hope you get this on time, sorry I didn't inform ,Just wanted to seek your help on something very important, you are the only person i could reach at this point, and i hope you come to my aid. Because something very terrible is happening to me now, i need a favor from you now.
I had a trip here in UK on a mission. Unfortunately for me all my money got stolen on my way to the hotel where i lodged along with my bag were my passport was ,And since then i have been without any money i am even owing the hotel here.
So i have limited access to emails for now, please i need you to lend me about 900pounds so i can make arrangements and return back please,i have spoken to the embassy here but they are not responding to the matter effectively, I will return the money back to you as soon as i get home, I am so confused right now.
I will be waiting to hear from you.
Regards
Shamsa Diwani
Shamsa Diwani
Ni kweli mimi nimepata toka kwa mtu ambaye namjua lakini sijawasiliana nae kama miaka mitano hivi. Yeye anafahamu niko hapa UK na ana-email yangu . Ameandika yupo nchi nyingine eti ana matatizo ya viza sasa nimtumie hela ya kumlipa mwanasheria anayemsaidia. Nilipomjibu kwa kiswahili pia sikupata kusikia habari zake pia. Was it a scam as well? pls be vigilant hasa inapo-involve hela.
ReplyDeleteMdau London.
SHAMSA NAOMBA UWASILIANE NA MIMI KWENYE EMAIL OLDMOSHI@GMAIL.COM AU PIGA 0716 494151 NAWEZA KUKUSAIDIA ZAIDI
ReplyDeleteHii kali. I received an identical email, mwezi uliopita, zilipita siku kadhaa kabla sijaiona basi nikaignore nikijua mwombaji atakuwa ameshasort mambo yake although i had suspicion. Jina la kiswahili, lakini email yote kiingereza. Niko london lakini anaomba nimkopeshe dollars. Besides email, hakuna namba ya simu hata ya hoteli alipo ili kama kweli amebanwa niwasiliane nae kirahisi. I didnt respond.
ReplyDeleteTrue, i also received such an email last month. guys be careful!!
ReplyDeleteJAMANI HII NI HATARI!! NAMI YALINIKUTA TENA KWA KUTUMIA E-MAIL YA MTU TUNAYEHESHIMIANA SANA KAMA IFUATAVYO:
ReplyDeleteAm sorry i didn't inform you about my urgent trip to London, i don't have much time on the pc here,so i have to brief you my present situation which requires your urgent response actually, I had a trip to London but unfortunately for me all my money got stolen at the hotel where i lodged due to a robbery incident that happened in the hotel.I had been so restless since last night because i have been without any money moreover the Hotel's telephone lines here got disconnected by the robbers and they are trying to get them fixed back i have access to only emails at the library because my mobile cant work here so i didnt bring it along,please i want you to help me with money so please can you send me 700 Pounds so when i return back i would refund it back to you as soon as i get home,I am so confused right now and dont know what to do, I had been to the embassy and they are currently looking into my case,Please you can send it through Western Union Money Transfer so i will get it immediately its sent,i want you to please help me transfer the money as soon as possible.Here is the details you need for the transfer below,
Receivers Names:MHESHIMIWA
Receivers Address: 103 Harley Street
City- London
Country- UK
Zip Code- W1G 6AJ
Please get back to me as soon as you have the money sent,once you are done with the transfer just help me to scan a copy of the receipt given to you by Western Union or help me to write out the Money Transfer Control Number(MTCN)
I will be waiting for your help. Thank you so much
Best Regards
MHESHIMIWA,
NILIISHTUKIA SIKUIJIBU NIKISUBIRI TAARIFA ZAIDI.
ACHENI UJINGA UTAMPAJE PESA MTU ANAYEKUOMBA KWENYE INTERNET WALA HUMJUWI NA HATA KAMA UNAJUWA SI MTAFUTE UMUULIZE SHIDA YAKE, HAYO NI MAMBO YA KAWAIDA HUKU KWA WATU, NI WEZI TU. WALA HAINA HAJA KU-TAKE CARE OF THAT RUBBISH THING.
ReplyDeleteHawa ni WANAGERIA. Kwani miaka yote wanafanya hivyo. Email za namna hii msiangaike kusoma.
ReplyDeleteWANAGERIA, WANAGERIA, WANAGERIA WEZI WAMETUMIA NJIA ZOTE ZA KUIBA HADI ZIMEISHA.
Mdau USA
Hii ni kweli inabidi kuwa waangalifu inaweza kuwa mtu yoyote lakini wa-Nigeria wanapractise hii sana wanaiita 419.Mtu akikuomba msaada nibora ku-comfirm kwanza,sababu unaweza kupuuzia na ukakuta ni kweli nduguyo anahitaji msaada na ukashindwa kumsaidia sababu ya upuuzi wa wa-Nigeria.
ReplyDeleteKAMA EMAIL YAKO IMEKUWA HIJACKED
ReplyDeleteKuna wale ambao email zao zimevamiwa na maharamia wa mtandao kisha kuanza kutuma emails kwa watu wengine ambao wako ndani ya contacts zao bila idhini ya mhusika mkuu
Tatizo hili limekuwa kubwa sana kwa siku za karibuni haswa kwa wale wanaotumia email za mtandao wa yahoo au ile ambayo inahusiana na yahoo kwa namna moja au nyingine .
Endapo utapatwa na sakata hili unachotakiwa kufanya ni kureport suala hili haswa kwa vyombo vya usalama vilivyo karibu yako na pia kuwapa taarifa kwa njia ya mtandao kutumia anuani nyingine watu walio kwenye contact zako pamoja na kutumia njia zingine kama simu ili kuwaataarifu na kama email yako imeunganishwa kwenye group au forum yoyote hakikisha unatoa taarifa pia kwa wanachama wengine ili wajue kuhusu tukio hilo .
Kuna wengine ambao hujaribu kufungua email hizo kwa kutumia njia mbali mbali mara kadhaa halafu kushitukia email hiyo imefungwa kwa masaa kadhaa na yahoo na ukijaribu zaidi inaweza kufungwa moja kwa moja .
Ikitokea hivyo hakikisha unasoma maelezo ya kutosha kutoka kwenye mtandao wa yahoo jinsi ya kurecover password yako kama tatizo linahusiana na password ukifuata maelezo hayo unaweza kurudisha email yako kwa mara nyingine .
Ukiweza kuirudisha hakikisha una ongeza email ya pili ambayo inaweza kutumika pindi tukio hilo likitaka kufanyika tena utapatiwa email kwenye email hiyo , pamoja maswali yako ya siri jaribu kubadilisha mara kwa mara .
Pia kwa siku za karibuni umeona unatakiwa kuongeza taarifa zaidi kuhusu accont yako ya yahoo na mitandao mengine tafadhali ongeza taarifa hizo lakini udhibitishe ni yahoo ukweli , kwa google kwa mfano wanahuduma ambayo inaweza kukutumia udhibitisho kutumia namba yako ya mkononi .
Mwisho usipenda kutuma chain emails zile ambazo watu wanaforward kwa watu mbali mbali , maharamia wengi wanatumia njia hiyo pia kwa ajili ya kukusanya emails pia njia hiyo ni rahisi kuvunja baadhi ya masuala binafsi ya mawasiliano kwa mtu kujua watu wako kwenye contact list , usipende kujisajili kwenye huduma za bure na kuacha email zako humo , unapojisajili email yako inaweza kutumika kwa shuguli zingine ambazo wewe hujaridhia .
Usiku mwema , nimeandika bandiko hili haraka haraka kwahiyo mengine nimeacha njiani au nimeeleza kwa udogo , wengine wanaweza kuendeleza zaidi kwa sababu tumezidiana katika uelewa wa vitu na mambo
__________________