waziri ally akipiga jeki wakati babu njenje akisaka spana baada ya mchuma wao kupata pancha sehemu za same wakiwa njiani kuelekea a-taun ambako leo wanatumbuiza ngurdoto kwenye kilele cha mkutano wa chama cha mabunge ya jumuiya ya madola
sehemu hii si mbali sana ambapo anko nanihii
na mkoko wake wa kuazima alikula basti. Ishukuriwe Njenje walifanikiwa kutatua tatizo na hivi sasa wanafanya sound check ngurdoto


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Tatizo ni matairi au ni barabara...mwaka huu nimesafiri mara 2 kwenda na kurudi Arusha kwa gari dogo (Carina)...nimepata pancha mara 3. Sasa naanza kujiuliza kulikoni, nilidhani ni mimi tu.

    ReplyDelete
  2. hi! Njenje taifa kubwa jamani wana ndinga yao wenyewe na wanaenda kuwazungusha mduara A-tauni,wanamziki lazima watumbuize sio wanamziki wa kisasa kazi yao bifu tuuu na umbea na kujifagilia wakati kazi hawafanyi

    ReplyDelete
  3. Magari ya kibongo kwa pancture! tatizo la matairi ya kibongo mengi ni re-thread, yamechongwa threads zake kwa fundi viatu! magari yanaposafiri mwendo mrefu kidogo tu matairi yakipata moto yanakuwa flat ndo maana ajali nyingi unasikia gurudumu la mbele limepasuka! kwa nchi zilizoendelea gurudumu likipasuka unawashti watengenezaji na wanalipa mamilioni ya dolas.

    ReplyDelete
  4. mdau wa kwanza ni kama vile umesoma mawazo yangu. yaani mimi huwa kila siku najiuliza ni kwa nini tanzania kunakuwa na ajali nyingi za magari zinazosabishwa na pancha. watu wengi wanapoteza maisha yao kwa sababu hizi nashangaa ni kwa nini hadi sasa serikali haijalifuatilia suali hili. aidha barabara ni mbovu kiasi kuwa matairi hayana uhai wa zaidi ya mwezi au madereva wanaendesha magari wakiwa na matairi vipara kabisa. Serikali inafaa kuliangalia suali hili kwa haraka sana.

    ReplyDelete
  5. Tyre za CHINA

    ReplyDelete
  6. NIMEENDESHA TOKA HOUSTON TEXAS HADI L.A CALIFONIA,MASAA 26, NIKAUNGANISHA CALI TO NEW YORK CITY MASAA 42..PIGA HESABU SIKU NGAPI HIZO NA SIJAPATA HATA PANCHA MOJA...MATAILI HAYO AMBADILI HADI LIPASUKE???ETI MWANAMUZIKI HUYO...OVYO.MDAU MONEY UK.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...