Na Sunday Shomari wa VOA
Bondia wa Tanzania anayeishi hapa Marekani huko Philadelphia Rodgers "The Tiger" Mtagwa anaingia ulingoni huko Madison Square Garden New York kuwania taji la WBO katika uzito wa Super Bantam Jumamosi 10-10-2009.
Rodgers atapambana na bingwa wa uzito huo hivi sasa Juan Lopez wa Puerto Rico ambaye pamoja na kuwa bingwa ameshukuru kwamba ndoto yake imetimia ya kupata pambano katika eneo maarufu la Madison Square Garden. Bondia huyu machachari anapigana staili ya "South Paw" maana yake nguvu yake kubwa iko kwenye mkono wake wa kushoto.
Alipozungumza kwenye mkutano wao na waandishi wa habari ameahidi pambano zuri na kusema anatambua kuwa Rodgers ni bondia hatari lakini anaahidi ushindi wa KO. Usiku huo ni mzito uliopewa jina la "Latin Fury" na mapambano hayo yataonyeshwa moja kwa moja na Pay Per View na pia kutakuwa na mapambano mengine mazuri tu ya utangulizi ambapo Yuriorkis Gamboa wa Cuba atapambana na Whyber Garcia, ambapo Gamboa atatetea taji lake la (WBA)uzito wa Feather.
Naye bondia machachari wa Marekani Jermain Taylor atatoana jasho na Arthur Abraham pambano lisilo la kutafuta mkanda wowote. Rodgers amezungumza na Sauti ya Amerika na kusema anafanya mazoezi ya bidii sana anakimbia kila siku na kupiga bag kila siku bila kuchoka na ameangalia mikanda ya video ya mpinzani wake kuangalia mbinu za ushindi Watanzania tumuombee kkeri na kumtakia ushindi.
Video zake
---------------------------------------------
Rogers Mtagwa, Mtanzania anajipanga kuingia ulingoni tarehe 10.10.09 huko mjini New York.Video hii moja inaonesha alivyomkoboa Villa raundi ya 10 na ya mwisho wa mpambano kwa TKO, alikuwa amelemewa raundi zilizopita hasa ya tisa:

Video ya pili ndo promosheni ya mpambano, itizame hadi mwisho utamwona na kumsikia Mtagwa:
Enjoy!
nukta77.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Nimependa english yako, ina accent kwa mbali saana. Unawazidi akina AY, Binamu na Kiba.

    ReplyDelete
  2. Hivi kina Matumla waliishia wapi? Najua kina Malinzi walishajikita kwenye soka.....mtu yoyote anaweza kunipa update? Kuhusu Mtagwa, nadhani nitakwenda kumshangilia. Sijui wabongo tutakuwa wangapi, nitaangaza-angaza kuwatafuta!

    ReplyDelete
  3. Rogers Mtagwa ananikumbusha bondia toka West Indies(visiwa vya karibiani) aliyelowea Uingereza Chris Eubank, wanafanana jinsi ya uzungumzaji na uhodari ulingoni.

    Mabondia wengi ikiwemo Frank Bruno wa Uingereza naye pia huchukua muda kujibu maswali ya papo kwa hapo.

    Yote kwa yote kufika hapo Madison Square garden ambapo kina Muhammad Ali, Tyson na wengine walipitia ni sifa kubwa kwako binafsi na kwa Tanzania pia.

    Tupo pamoja
    Mdau
    Bronx NYC

    ReplyDelete
  4. Dada Nukta,
    Ahsante kwa kupost hiyo habari. Ingawa mimi sio mshabiki mkubwa wa boxing, hapo uzalendo uliniingia sana. Tutafuatilia hiyo weekend tuone itakuwaje.
    Nimeangalia mapambano yake mengine, watangazaji wanamuita 'Africano'.

    Ntibadyuza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...