Rogers Mtagwa (kulia) akipozi na Juan Manuel Lopez
Hali ya uchumi iliulazimisha mwaka huu kuwa na mapambano machache saana ya kulipia (Pay Per View) na katika mwezi huu, October 17, kutakuwa na pambano moja tu ambalo katika pambano kuu (main event), anasimama nyota wa ndondi toka Tanzania Rogers "The Tiger" Mtagwa.
Rogers mwenye rekodi ya (26-12-2) na anayeshikilia nafasi ya 9 ya ubora wa ndondi kwa uzito wake katika orodha inayotambuliwa na Shirikisho la Ndondi Ulimwenguni (WBO) atapambana na Juan Manuel Lopez (49-4-1) wa Caguas, Puerto Rico katika kuwania mkanda wa Lopez katika uzito wa WBO junior featherweight. Pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa WaMu Theatre uliopo eneo maarufu la Madison Square Garden jijini New York.
Rogers na Juan wakipromoti mpambano wao
Hii ni hatua kubwa na ya kujivunia kwa Mtagwa ambaye ameonesha ujasiri na maendeleo makubwa katika ulimwengu wa ndondi kwa kutwaa ubingwa wa NABF na USBA katika uzito wa Feather na pia kwa kuonekana kuboreka kila ajapo ulingoni kiasi cha kuwafanya wengi kuliona pambano lake la mwaka jana dhidi ya Thomas Villa kama PAMBANO LA MWAKA 2008.
Katika pambano hilo lililopiganwa Tucson Arizona, Mtagwa alishinda kwa KO ya raundi ya 10.
Tazama / attach
Tujiunge kwa pamoja kumshangilia (kwa watakaoweza) na kumuombea Mtanzania mwenzetu anayefanya vema sasa katika ulimwengu wa ndondi aweze kufanikiwa.
Kuwa kwenye pambano pekee la pay per view kwa mwezi huu ni kuonesha thamani yake kwani wapo mabondia wengi wenye majina ambao wameshindwa kuweka mapambano yao kwenye hadhi hiyo.

promo za mpambano
Kumbuka kuwa nyota kama Yuriorkis Gamboa toka Cuba atapigana katika pambano la utangulizi usiku huo dhidi ya Whyber Garcia katika kuwania umiliki wa mkanda wa WBA "regular" featherweight title unaoshikiliwa na Gamboa kwa sasa.
Nyota wengine waliopata kushikilia mikanda ya dunia ambao watapigana kwenye mapambano yasiyo ya kulipia ni pamoja na Jermaine Taylor vs Arthur Abraham watakaochuana Oct 17.
Tunamtakia Rogers Mtagwa pambano jema
www.changamotoyetu.blogspot.com


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. The GrandPMCOctober 07, 2009

    at least yeye anapigana akiwa na hakika na usalama wake awapo ulingoni sio kama kina Cheka,na anatambulika na federation kubwa,it is high time kwa mabondia wetu kufikiri vitu vya akili kama hivyo,likewise boxing federation yetu hapa IMELALAAAA SANAAAA,they should wake up and smell a cup of coffeee,inakera kwa kweli

    ReplyDelete
  2. GIVE A GO SON, MTOE KAMASI HUYO MTINDIGA. NIMESHAODA TAYARI HILI PAMBANO NA HII NI SUPPORT TOSHA NDUGU YANGU, USINIANGUSHE I,LL BE TALKING YOUR NAME ALL OVER THE PLACES. YOU GOT MY SUPPORT JO!!! JO!! JO!!! BUMA YEEEH

    ReplyDelete
  3. The GrandPMC nakubaliana na wewe ila naomba ukubali marekebihso yangu. hebu tuseme 'akina Kaseba'. waliofanya fujo ni akina kaseba. tusigeneralise, tumpe haki yake Cheka kwa kumgalagaza kilimilimi wetu bongo.

    vinginevyo namtakia Mtagwa kila la heri katika pambano lake hilo gumu. gumu kwa kuwa inaonyesha mpinzani wake si haba.

    ReplyDelete
  4. Kazi ni kazi!! Lakini kazi ya ugomvi mh mh

    ReplyDelete
  5. Naweza kujitupa The Garden kumsupport. Asante kwa update.

    ReplyDelete
  6. Tupo Pamoja Rogers Mtagwa, maana huko ulipo lazima wanasikia jina la nchi yetu Tanzania kwa sana.

    Ukija Tanzania kwa vekesheni usije kimya kimya, ili usaidie kuitangaza Tanzania duniani kote.

    Mdau
    Kitongojini Mgeninani Mbagala DSM

    ReplyDelete
  7. jamani nipeni matokeo ya mpambano wa kaseba na cheka ulikuwaje nani kashinda?

    ReplyDelete
  8. Mmmmh...huyo mwana Mtagwa hiyo face inaonekana imekula ndonga kichizi...ila na yeye anaonekana ngumi jiwe ile mbaya..good luck to you Roger Mtagwa, mgonge mawe huyo mtoto aumuke kama maandazi ya zenji!

    mdau
    Ashkmatit

    ReplyDelete
  9. Hongera Mtagwa, sio pambano dogo hilo. Nakutakia mafanikio na ushindi katika fani. Ntacheki kama naonyesha mpambano huku kwangu niliagize kukuunga mkono...japo sio shabiki wa ndondi.

    ReplyDelete
  10. nimemsikia mtangazaji amemtaja kawawa big up.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...