MKUTANO WA WATANZANIA GAUTENG
TAREHE 24 OKTOBA, 2009
UBALOZI WA TANZANIA NCHINI AFRIKA KUSINI UNAPENDA KUWATANGAZIA WATANZANIA WANAOISHI KATIKA JIMBO LA GAUTENG KUWA KUTAKUWA NA MKUTANO WA WATANZANIA WANAOISHI KATIKA JIMBO HILO UTAKAOFANYIKA TAREHE 24 OKTOBA, 2009 SAA NANE NA NUSU MCHANA HADI SAA KUMI NA MOJA JIONI KATIKA UKUMBI WA PRETORIA COUNTRY CLUB,
NAMBA 241
MTAA WA SYDNEY,
WATERKLOOF,
PRETORIA.
MKUTANO HUO UNA LENGO LA KUANZISHA JUMUIYA YA WATANZANIA KATIKA JIMBO HILO. TAFADHALI TUNAOMBA KUVAA NADHIFU NA KUZINGATIA MUDA. KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NA WAFUATAO:
1. Jumanne Fhika 0762 909449
2. Faustine Ndugulile 0799 965120
3. Laurean Rugambwa 0835 566966
4. Lumbi na Ethel 012 344371/012 3425921
UBALOZI WA TANZANIA
PRETORIA
Mambo ya diaspora hayo. Leo diaspora kesho tawi la CCM.
ReplyDelete@Mkuu Michuzi,
ReplyDeleteNapenda kukushukuru kwa kutuwekea hili tangazo. Ahsante sana.
@Wadau wa Gauteng
Ningependa kuwataarifu wale wote ambao watahitaji usafiri toka Johannesburg kwenda Pretoria wanijulishe kwa kunipigia simu (0799965120)au kunitumia email (drfaustinen@aol.com)
@Anony 12:00
Mkutano huu una lengo la kuunda jumuia ya kuwaunganisha watanzania wote waishio Gauteng bila kujali itikadi.
Lakini hii haizuii watanzania wanaoishi huku kuunda matawi ya vyama kutegemea itikadi zao.
Unajua nini, its not going to work,kwa sababu hapa Rsa,watanzania wamegawanyika mara mbili ,kuna wabongo na watanzania ,watanzania ni wale ambao wamekuja hapa kwa kuletwa either wanasoma.wanafanya kazi maofisini ukijumlisha wale wanaofanya ubalozi na kwengineko,na kuna wabongo ambao hawa ndio wanaoishi RSA ,I MEAN wako street na ambao ni majority hapa kwa maana mengine ni watoto wa walalahoi ,wako hapa miaka mingi tofauti na wale wanafunzi ambao wanakaa miaka miwili mitatu wanaondoka hawa ni wahusika zaidi hapa RSA,Ambao wanabaguliwa wakienda hata huko ubalozi kwani wanaoenekana hawana maana yoyote ,ambao wamenzisha jumuia ya kuzikana hapa Pretoria tangu mwaka 1995.hakuna mbongo amezikwa hapa Pretoria unless ndugu zake wameshindwa kupatikana huko Tanzania,bila ya msaada wa ubalozi ,ambao pamoja na hayo hata karatasi za kusafiria marehemu huwa tunatozwa pesa,sasa maswali sisi wabongo ambao tunaishi Rsa permanently and we manage to organize ourself for all those years ,do we need any messiah ,especially from useless people like embassy of Tanzania ,and few student ,who they just come now ,after few years they wont be here and they dont know thing about street,nothing ? ,the answer is NO,we dont need u people cause u dont need us,sio nyinyi akija mtu mnaangalia huyu ni doctor au proffesor,au mtoto wa fulani kabla hajapata msaada,na akiuliza watanzania wanapatikana wapi mnawaambia weote watanzania walio street ni wezi au wanafanya biashara haramu,ebu nenda kaangalie pale TRA Tunduma sio sisi wabongo ndio tunaongoza kwa kulipa tax,wakati ninyi vitu vyenu vyote vinaingia tax free.Narudia watakujas watu katika mkutano wenu ,lakini ni wale wanaofanana na ninyi,sisi wabongo hamtatuona .kaka mnatafuta njia ya kuiba pesa za hapo ubalozini ibeni ,si mmezoea kuiba,andikeni walikuja watz,,wangapi ,alafu muibe ,izo pesa,because isv the only thing u know.ni mimi wa MOROGORO.
ReplyDeleteMdau wa Morogoro,
ReplyDeleteNinashukuru kwa maoni yako. Mimi ni mtanzania kama walivyo watanzania wengine ambao tumeona kuna haja ya kuwa na jumuia yetu hapa Gauteng.
Katika rasimu ya katiba mpya tuliyotengeneza makundi mbali mbali yatawakilishwa ikiwa pamoja na Wasomi, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wakinamama na vijana kwa kutaja makundi machache. Uongozi wa jumuia utakuwa na uwiano wa makundi niliyotaja hapo juu.
Siwezi kujibu kwa niaba ya ubalozi, lakini Ubalozi na Kaimu Balozi aliyopo wako mstari wa mbele kuhakikisha jumuia inaundwa na makundi niliyotaja yanawakilishwa.
Hii ni nafasi yako wewe kuja na kutoa mchango na madukuduku yako. Kukaa pembeni haitasaidia.
Jumuia hii ni yetu sote ikiwa pamoja na mimi na wewe. Kwa hiyo mchango wangu na wako unahitajika kuunda jumuia itayosaidia watanzania wote bila kujali elimu, kipato wala itikadi.
Kama maelezo zaidi au kama utataka nakala ya katiba wasiliana nami kwa email(drfaustinen@aol.com) au simu( 0799965120.
Shukrani
Faustine
Tunashukuru kwa taarifa,tutakuja. Nimefurahi kusisistizwa kuvaa nadhifu.. Ila watanzania mara zote huwa tupo nadhifu hata bila kuambiwa.
ReplyDeleteMdau aliyetoa maoni kuhusu kuwepo kwa wabongo na watanzania huko bondeni amelonga kutoka moyoni. Kutakiwa 'kuvaa nadhifu' ni dalili za kuwepo kwa tofauti hizo.
ReplyDeleteWenzenu waliopo US wameanzisha (au wameanzishiwa) jumuiya kama hii. Membe alinukuliwa na magazeti yetu kwamba kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ilikuwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM. Ondoeni tofauti zenu kwanza vinginevyo itakuwa hadithi tu.
SIJAISHI SOUTH SINA LA KUSEMA HAPO SEMA UGOMVI WANGU NI KWANINI HUYU JAMAA AWAPANGIE WATU KUVAA KWENYE KIKAO????KWELI WABONGO BADO.MDAU MONEY UK.
ReplyDeletelazima wakumbushwe kuvaa vizuri hao bila hivyo kimbembe
ReplyDeleteMsela wa Moro umesema ukweli kabisa ubalozi wetu hapa sauzi ni useless hauna msaada wa aina yeyote hasa kwa sie wabongo ndo maana nimeamua kujilipua sina deal nao labda mpaka nikifa watapata fweza ya karatasi langu la kunirudisha kwa bi mkubwa mzee wa moro karibu maza site sie wabongo kivetuvetu mikutano kama hii waachieni wenyewe watanzania wachangishane au kiufupi wamchangie mtu asafiri kwani kuna tabia ya watanzania wakishajua watahama nchi wanaanzisha jumuiya na michango ikishaanza wanapotea ooooh mie simo open you are eyez nipo sauzi hapa miaka 15 i know what am talking about from pretoria to cape town .from mamelodi to kayelisha same story
ReplyDeleteMbona aliyetoa maoni Thu Oct 08, 12:39:00 PM na wa Thu Oct 08, 11:00:00 PM inaonekana kuwa ni myu mmoja? Ukiangalia style ya namna alivyoandika, ujumbe alioutoa, na orign yake aliyoiainisha wazi (mtu wa Moro) unastukia kwamba ni mtu yule yule. Bangi mbaya sana jamani.
ReplyDeleteKwani Balozi mpya wa tanzania RSA ameisharipoti? Au atakuwa ameishafika tarehe hiyo?
ReplyDelete