Home
Unlabelled
tamasha la sanaa bagamoyo lamalizika
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
fide mti mkubwa unaona kundi lako?
ReplyDeleteMBONA REDIO ZA TANZANIA HAZIPIGI NYIMBO ZA MAKABILA YETU, AU NDIO KUONDOKANA NA UKABILA? TAIFA LIMEKUFA TUMEIGA WAMAREKANI SANA NA R&B ZAO.
ReplyDeleteNafurahi kuwa mmoja kati ya watu wa kwanza kabisa kuwa katika kundi la Shada..Nakumbuka maonesho mengi tuliofanya Bagamoyo na Dar na hadi wenzetu walioendela kwenda kufanya maonesho Ujerumani na sehem nyingine duniani. sitosahau mara ya kwanza tulipoenda kufanya onesho kwenye tamasha la sanaa la watoto pale Nkurumah hall UDSM. tulikuwa na Fide na Azimio Magehema kama waalimu na viongozi wetu...nakumbuka wimbo ambao Azimio alitufundisha siku iyo tukiwa kwenye gari...(Utamaduni hatuachi jama uliza utaambiwa).Kushiriki kwenye sanaa nikiwa na umri mdogo kumenipa ujasiri na uhodari wa kuweza kusimama mbele za watu na kujieleza ipasavyo.Nilifurahi pia kurudi Nkurumah hall kama mwanafunzi wa UDSM mwaka 2003 baada ya kuwa pale kama msanii mdogo miaka iliyopita...kwenye lile tamasha ndo ilikuwa siku ya kwanza kumuona Michuzi alitupiga picha na kututoa kwenye daily news...nawakumbuka baadhi ya memba wa shada...Adam,Doto na kulwa seif,Mrisho,Ndomoki,Hussein,Fadhili,Deo,Kelina,Sada na wengine wengi tu...salam kwa Fide Tungaraza,Azimio Magehema na wanashada wengine popote mlipo...Masimbi Jr
ReplyDeleteNasikitika kuona habari hii bwana michuzi, yaani sio siri tamasha la mwaka huu limenipita hivihivi kisa ni kukosekana kwa matangazo ya kutosha, dah! anyway natumaini mwakani nikijaaliwa uhai ntafika tena kuliona, mi nimekua mpenzi sana wa tamasha hili na niliambukizwa ugonjwa huu kpindi nasoma shule ya msingi mlimani, yaani nlikua sikosi lile tamasha la sanaa la watoto lililokua likifanyika kipindi cha mwezi august au september kalibu kabisa na mitihani ya darasa la saba, na sijui kwanini kitu kile hakuna tena siku hizi. Asante bro Michuzi kwa habari hii ambayo kwangu mie ni kama habari mbaya kwani nlichokisubiri kwa mwaka mzima sasa sitokipata tena hadi mwakani
ReplyDeleteMasimbi Jr
ReplyDeleteUmenifanya machozi yanilenge.
Mwaka 2007 nilipokuwa Bagamoyo nilikutana na Hussein Masimbi, Deo, Joana (siku hizi ni mwanamazingaombwe wa kutisha kabisa), Saada, Caroline Songoro na wanashada wengine wengi tu. Nilifurahi sana kukutana na marafiki-wanafunzi zangu wale ambao wengine wamebobea kabisa katika sanaa na wengine wapo chuoni Bagamoyo kama walimu na wengine wakisoma Diploma ya Sanaa.
Onyesho la Nkrumah Hall lilikuwa la aina yake kwa kumbukumbu. Namkumbuka Hussein na Meno katika onyesho la tatu la mchezo. Namkumbuka Deo alivyowashangaza au kuwapagaisha watazamaji kwa uchezaji wake. Nawakumbukeni nyote mlivyokuwa mmefurahi wakati wa safari ya kwenda na ya kurudi. Nawakumbukeni nyote mlivyokuwa na shauku wakati wa mazoezi na wakati wa maonyesho. Namkumbuka Deo tukiwa safarini kwenda UDSM na wimbo wake wa "We mtoto wee? Mbona hivyo wanitesa nahangaika?Nilipokuwa na Dada Mary alinipenda sana, hivi sasa kaondoka sina mwingine tena.." Nakumbuka mikono mingi ya pongezi baada ya onyesho lenu. Nakumbuka Mwalimu Juma Bakari aliponiambia baada ya onyesho "..Well done Fidelis.."
Nawakumbukeni sana na wakati mwingine huwa natamani sana tukutane tena wote, tucheze, tuimbe, tupige ala, tuigize, tuangalie video, tusimuliane hadithi kama tulivyokuwa tunafanya kila Jumatano na Jumamosi.
Nawashukuruni sana nyote mmekuwa ni sehemu ya maisha yangu. Pia namshukuru zaidi sana Mwalimu Rashid Masimbi kwa kuniamini na kuniruhusu kuwa Mwalimu wenu. Nawashukuru wanajumuiya wote wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo kwa kuendelea kuilea Shada hadi leo.
Ni mimi maridhiya,
Fidelis M Tungaraza
Fidelis,
ReplyDeleteKaka una kumbukumbu kali sana.nilishasahau huo wimbo wa Deo wa dada Mary...kwa kweli ni siku nyingi sana zimepita na Shada ni moja kati ya vitu ulivyovianzisha na kufanikiwa na unahitaji pongezi kubwa sana..Naamini mafanikio ya shada leo yanatokana na juhudi zako wakati kuianzisha.Watu wengi wengi waliokuwa shada sasa wamekuwa wasanii waliobobea kabisa na hayo ni matunda ya shada.Siku moja tunaweza tukaandaa kaproduction hata ka dakika kumi na tukakaonyesha kwenye tamasha. wanashada wengi wapo na inawezekana kuwakusanya ingawa huwezi kuwapata wote ila wengi wanaweza kushiriki. Kila la kheri mkuu mimi ni Nsali Masimbi kama hukujua.tuwasiliane mkuu nsalimasimbi@yahoo.com