Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk. Asha-Rose Migiro akipiga danadana mbele ya mtoto Charles Ssali (12) toka Uganda ambaye ni Balozi maalum wa Muungano dhidi ya Malaria (United Against Malaria) mtoto huyo alipomtembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, leo. Wengine ni Bw. Robert Skinner kutoka taasisi ya Umoja wa Mataifa na Bw. Herve Verhyoosel kutoka Ushirikiano wa Kutokomeza Malaria ( Roll Back Malaria Partnership).

Na Mwandishi Maalum,
New York


Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk Asha-Rose Migiro amesisitiza umuhimu wa matumizi ya vyandarua vyenye dawa kama njia bora na rahisi ya kujikinga na Malaria.

Ameeleza tafiti mbalimbali zimeonyesha katika maeneo ambayo kumekuwa na matumizi makubwa ya vyandarua, sambamba matumizi ya dawa sahihi na utokomezaji wa vyanzo vya mazalia ya mbu, vifo vitokanavyo na malaria vimepungua kwa asilimia kubwa.

Dk. Migiro, ameyasema hayo leo wakati wa mazungumzo yake na Balozi maalum wa Muungano dhidi ya Malaria (United Against Malaria) , Charles Ssali ( 12) kutoka Uganda, wakati mtoto huyo alipomtembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York.

Akabainisha kwamba, licha ya ugonjwa huo kuwa chanzo kikubwa cha vifo hususani kwa watoto chini ya miaka mitano barani afrika, pia umekuwa na athari kubwa kwa nguvu kazi na hivyo kuathiri mapato na uchumi wa n chi zinazoendelea kutoka na nguvu kazi hiyo kutumia muda mwingi kujiuguza.
“ lakini kama hiyo haitoshi, malaria inaadhari nyingine kwa wanamichezo, kwani huadhiri kiwango chao cha uchezaji kwa kujikuta wakiugua malaria mara kwa mara” akasema Dk. Migiro.

Naibu Katibu Mkuu amefafanua kuwa Katibu Mkuu wa UN, Mh. Ban Ki Moon kwa kushirikiana na Muungano huo dhidi ya ugonjwa wa malaria amejiweka malengo ya kuhakikisha kwamba, watu wengi wanalala kwenye vyandarua ifikapo mwaka 2010.

Katika mazungumzo yao, Mtoto Charles, alimweleza Naibu Katibu Mkuu, kwamba yeye ni mpenzi sana wa mchezo wa mpira wa miguu kuliko mchezo mwingine wowote. Na anauchukia ugonjwa wa malaria kupita kiasi.

“ Mimi napenda sana mpira wa miguu, lakini nachukia sana malaria, kwa kadri ninavyokumbuka nimekuwa nikiugua ugonjwa huu tangu nikiwa na miaka minne. Lakini tangu Anti yangu alipoanza kuhakikisha nalala ndani ya chandarua, sijasubuliwa tena na ugonjwa huo”ameeleza Charles.

Akaeleza kuwa, pamoja na kutumia chandarua , Klabu yake anayoichezea imekuwa ikihakikisha kwamba wanameza dawa za kuzuia malaria kila baada ya miezi sita.

Charles katika mazungumzo hayo, alikuwa amefuatana na Bw. Robert Skinner kutoka taasisi ya Umoja wa Mataifa na Bw. Herve Verhyoosel kutoka Ushirikiano wa Kuutokomeza ( Rolls Back Malaria Partnership). Akasema Kupitia ubalozi wake huo, anatoa wito kwa wazazi , watoto na watu wote hususani barani afrika kulala kwenye vyandarua ili kujikinga na ugonjwa huo hatari.

“ kama unataka kucheza mpira wa miguu kama mimi na kushinda kombe la dunia la Ghothia kwa vijana, lala kwenye chandarua uepukane na malaria” akasisitiza Charles.

Baada ya mazumgumzo yao, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Asha- Rose Migiro alikabidhiwa Chandarua kikubwa kama ishara ya kuendeleza kampeni dhidi ya ugonjwa wa malaria na akacheza mpira na mtoto huyo.

Umoja dhidi ya Malaria, ni mpango mkakati wa pamoja ulioanzishwa mwaka 1998 kati ya Ushirikiano dhidi ya Malaria, Shirika la Afya la Umoja wa Mataia(WHO), Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ( UNICEF), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa ( UNDP), Bank ya Dunia na taasisi nyingine zisizo za kiserikali ikiwamo ya Bill na Belinda Gates.

Madhumi ya Umoja huo dhidi ya Malaria ni kuwahamasisha wapenzi wa mpira wa miguu duniani kote kuunga mkono jitihada za kuhakikisha watu wengi wanapata huduma za vyandarua na dawa za kutibu malaria ifikapo mwaka 2010.

Takwimu kuhusu madhara ya ugonjwa huo ambao zimekuwa zikitolewa na wataalam mbalimbali, zinaonyesha katika kila sekunde thelathini mtoto moja hupoteza maisha barani Afrika. Huku zaidi ya watu milioni moja wakipoteza maisha kila mwaka.

Aidha takwimu hizo zinaonyesha pia kuwa duniani kote watu bilioni 3.3 sawa na nusu ya idadi ya watu wote, wamo katika hatari ya kuugua malaria. Huku Asilimia 91 ya vifo vya vitokanavyo na malaria vikitokea Afrika.

Kwa upande wa athari za kiuchumi, ugonjwa huo unachangia katika ongezeko la umaskini na kurudisha nyuma fursa za maendeleo. Wastani wa dola 12 bilioni za kimarekani hupotea kila mwaka kama sehemu ya uzalishaji.
Kama hiyo haitoshi asilimia 40 ya matumizi katika huduma za afya barani afrika huishia kwenye malaria peke yake.

Wataalamu wanaeleza kwamba ugonjwa huo unazuilika na kutibika. Kwa dola tano au kumi unaweza kumlinda mama au mtoto dhidi ya ugonjwa huo kwa kipindi cha miaka mitano, kwa kutumia njia rahisi kama matumizi ya vyandarua, dawa sahihi na kunyunyizia dawa za kutokomeza mazalia ya mbu.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akiwa ameshika chandaru pamoja na mtoto Charles Ssali ambaye ni Balozi maalum wa kampeni dhidi ya ugonjwa huo na maafisa toka taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Ushirikiano wa Kutokomeza Malaria ( Roll Back Malaria Partnership).



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Mama kazi unaijua kha! raha ya kuwa mwembamba

    ReplyDelete
  2. du ukujiunga na yanga simba watafungwa sana, welcom chelsea fc

    ReplyDelete
  3. Du! kumbe Dr. Rose Migiro naye yumo du cjui alipiga ngapi.

    ReplyDelete
  4. CHARLES AMEFUNDISHWA ASEME NINI KWANI TUPO WENGI TUNAOLALA NDANI YA VYANDARUA NA TUNAPATA MALARIA, IWEJE MBU YULEYULE AKIKUUMA NJE YA CHANDARUA UPATE MALARIA, HII NI USANII WA ETI MBU ANAYELETA MALARIA NI YULE ANAYEKUUMA USIKU WA MANANE TU' WATAALAMU TUAMBIENI UKWELI WA BIASHARA HII.

    ReplyDelete
  5. Atia boli bibi huyu kumbe maximo ampe namba ndani ya taifa stars.

    ReplyDelete
  6. kwa wanaopenda kufikiri kuna jambo la kufikirisha katka mchango wa anonymous Nov 13, 12:00. Vyandarua ni danganya toto tu. tutafunte njia sahihi ya kuangamiza mbu sio kumzuia kwa muda. tena mie nadhani ukimzuia mbu kwa muda, muda akikupata ni balaa zaidi.

    jiulize ni kwa nini tunaokwenda hospital kutibiwa malaria wengine wanalala kwenye vyandarua na wengine hawalali kwenye vyandarua?

    jiulize kwa nini ulaya na marekani hakuna mbu. je wameshindwa kutufundisha jinsi ya kuangamiza mbu.

    jiulize kwa nini kiwanda cha dawa mseto ya malaria kiko Brooklyn New York. (kaangalie ganda la dawa hiyo leo.)

    jiulize kwa nini baadhi ya watu walipopendekeza tunyunyize DDT tanzania nzima, kama walivyofanya marekani na kanada miaka ya 1920 ili kuanga miza mbu walipigwa vita na kunyamazishwa.

    dawa za malaria, vyandarua na kadhalika ni mradi wa watu fulani wakubwa nje ya nchi wakishirikiana na viongozi wa humuhumu afrika.

    ReplyDelete
  7. mwee uyu mama kila kitu kabarikiwa
    1.shule/akili ya kufa mtu
    2.kazi swafi
    3.mume bora
    4.pesa juu
    5.kipaji cha mpira duh

    tuna watu wa kujivunia tanzania

    ReplyDelete
  8. Huyo Mtoto "balozi" alichaguliwa lini?

    Halafu shule ana atendi saa ngapi kama kazi yake ndo kuzunguka duniani na kutangaza malalia?

    ReplyDelete
  9. Huyu mama ni mtu mzuri ila ni njia ya Kumpigia Kuwa Raisi hapo baadae akitoka Raisi Kikwete Mie si nipo mtaona wekeni kichwani.

    ReplyDelete
  10. Wapare wako juu!

    ReplyDelete
  11. Mwaipopo...badala ya kuanza kuuliza kwa njia ya kujenga hoja, nibora ungeuliza kwa nia ya kutaka kujuwa.Sababu unachokiuliza kiko nje sana na fani yako...badala yakuonekana unajuwa unaonekana kituko

    1.Kama ilivyokawaida kwamba nzi hupumzika nyakati za usiku lkn huwa kazini nyakati za mchana, ndivyo hivyo hivyo, mbu waleteao malaria huwa hupumzika nyakati za asbh,mchana,jioni hadi usiku mpaka usiku wa manane ndo huanza kazi. Huo ni utaraibu wa maisha yake, kila kiumbe na utaratibu wake wa maisha kutokana na mahitaji yake na mazoea (adaptation) kwanini hushangai bundi kuonekana usiku tu lakini mchana haonekani!

    Kuhusu kutokuepo mbu ulaya na amerika, daah mbona hushangai kwanini zanzibar hakuna simba?
    Kuepo au kutokuepo kwa kiumbe katika sehemu husika inategemea sababu nyingi ikiwemo geographical climate, mbu hawezi kuishi kwenye climate ya baridi kama ya ulaya na amerika, mbu ana ishi vyema kwenye tropical climate kama hiyo ya Tanzania

    Unaposema kwanini kiwanda cha dawa za malaria kipo USA? Duh mbona huulizi kwanini kiwanda cha Benz kipo Ujerumani na si Tanzania? Kuna viwanda vingi tu haviko kwetu but bidhaa zake hutumiwa kwa wingi kwetu. Sababu wenzetu wakombele sana kwa technologia na wana wasomi (wasomao kwa kuelewa na ku apply knowledge) sio wasomaji (wanaosoma kwa kukariri wakaishia kupata credit za masomo tu)

    Mwisho umezungumzia DDT, hii wakati inatumika huko marekani huo mwaka 1920 unaosema, ilikuwa haijafahamika madhara yake kwa viumbe hai, baade ndo wakajuwa matatizo yake kwa viumbe hai ikiwemo ndege na samaki wa baharini, DDT ina dhoofisha gamba la yai, hivyo kumfanya ndege au samaki asiweze kuendeleza kizazi, sijui ulitaka ndege wote na samaki duniani wapotee?? Kwa hiyo kukatazwa kwa DDT si kwa kuionea Tanzania hiyo ni dunia nzima marufuku kutumiwa ni environmental hazard!
    NB:Jifunze kudadisi, na si kukebehi kwa kile usichokujuwa, kila fani ina bwana wake.

    ReplyDelete
  12. Wapare wako juu!! ukabila huo, mama mwenyewe mbona mtu wa Songea huyu.

    ReplyDelete
  13. Ugali si mchezo utafanya kitu chochote ukiambiwa fanya

    ReplyDelete
  14. kwa mwendo huu wa ufisadi kila kona ni heri, ni heri migiro aje kuwa rais wa nchi hii. tumechoka na siasa za uswahiba na kuchekacheka.

    ReplyDelete
  15. Binafsi nimevutiwa na hayo MAHIPS yake akinyanyuwa Boli .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...