Mdau anauza nyumba hii.
Iko Tegeta Salasala jijini Dar.
Mwenye kuhitaji awasiliane naye kwa simu namba zifuatazo:
0754088610
0754303997
0715088610
0787303997




Nyumba ni ya vyumba 2
Master bedroom 1
Library 1
Jiko 1
Choo 2
Sitting room 1
Dinning room 1
Store 1
Tiles nyumba yote
Umeme na maji
Tank 2 za akiba lita 6000
Kisima cha maji ya mvua lita 10,000
Heater na pump ya kupandisha maji
Pevin blocks
Garden
Bati la kisasa na aluminium
Fensi yenye mikuki na ruvazi




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Hivi kwanini linapokuja swala kama hili la nyumba inauzwa.... yaani wabeba box kimyaaaaa kabisa, lakini maswala kama ya kanumba wanakua wa kwanza ku-comment,wabeba box ebu tuonyesheni kwamba huko ni pazuri kwa kununua majumba kama haya, msinitukane wajemeni
    Ni mimi MLA VUMBI.

    ReplyDelete
  2. Shs ngapi? Bilioni mia mbili? Maanake bei za nyumba zinazotangazwa humu kwa michu ziko kwenye karensi ya Zimbabwe.

    ReplyDelete
  3. ka michuzi nyumba ni ya nguvu ila hatuonyeshwi ndani hata kidogo tuone bafu likoje jiko n.k na bei je? wengine hatuishi huko ila tunapenda kujua bei pls tujulishe.

    mdau masachusets

    ReplyDelete
  4. tuonyeshe picha za ndani ya nyumba pia na inayoonekana yote si hivi upande tu.

    ReplyDelete
  5. HII NYUMBA SI ILIKUA INAPANGISHWA JAMANI,SASA IMEKUAJE?

    ReplyDelete
  6. ni nyumba nzuri wenye pesa muwe waangalifu na hati za umiliki haswa kujua kama eneo linakubaliwa ujenzi, sio bondeni, hati hazina ugomvi

    ReplyDelete
  7. WABEBA MABOX TUNANUNUA NYUMBA HUKU NI CHEAP THA TZ. HUKU TZ KAMA HUNA MILLION 300 CASH HUPATI NYUMBA YA MAANA. HUKU POUND 50,000 UNAPATA 2 BED ROOM HOUSE PIA UNAKUWA UNALIPA KWA MWEZI, TZ HATA MORTGAGE HUKU KUPATA SIJUI HATA INA EXIT!

    ReplyDelete
  8. JAMANI PAMOJA NA KUWEKA NAMBA NYINGI ZA SIMU KWA AJILI YA MAWASILIANO! SIO MBAYA KABLA YA KUPIGA SIMU UKAJUA BEI ILI UONE KAMA UNAWEZA KUIMUDU KUNUNUA AU LA! HALAFU IMEPIGWA PICHA ZA KUIBIA,MAANA PICHA ZOTE TATU NI UPANDE MMOJA YAANI LINGEKUWA GARI TUNGESEMA UPANDE MMOJA LITAKUWA LIMEPATA AJALI AU KAMA ANGEKUWA NI DADA WA KIHAYA AU KINYAKYUSA UMEPIGA PICHA INAONYESHA MGONGO TU WALA SURA UIJUI.
    UTOE NA MAELEZO KAMA MAENEO ILIPO LAZIMA UWE NA GARI 4X4 SANA SANA KIPINDI CCHA MVUA ILI UKINUNUA LAZIMA UWE NA AINA GANI YA USAFIRI.

    ReplyDelete
  9. WABEBA BOX TUNAJENGA WENYEWE,KIPI BORA KUJENGA UNAVYOTAKA AU MTU AKUUZIE??VILEVILE NI CHEAP KUJENGA KULIKO KUNUNUA....ITS NOT ROCKET SCIENCE......WENYE HELA NUNUENI

    ReplyDelete
  10. Kutokuweka bei ya nyumba hii ni dalili ya ujanja-ujanja. Kama inauzwa na haina mushkeli kwanini bei haikuwekwa?

    ReplyDelete
  11. KWA NINI WAUZA NYUMBA AU MAGARI WA BONGO HUWA HAWAWEKI BEI ZAKE??

    ReplyDelete
  12. Inatisha utanunua nyumba leo miaka mitano baadaye utasikia serekali inafuatilia nyumba yako maana inahusika na mambo ya ufisadi. Nyumba nyingi za namna hiyo huwa zinajengwa na mafisadi.
    Ndio maana mbeba box atakuwa na wasiwasi kuwekeza hela zake namna hiyo.

    ReplyDelete
  13. wekeni number ya kiwanja na tunataka kuona kwa ndani na nyumber yote kwa ujumla au pia unaweza kutuwekea ramani yake kwa kuiangalia ukiwa juu au plane view

    ReplyDelete
  14. Nyumba nzuri sana, ila ombi kwa muuzaji au agent wake. Next time weka features za nyumba zake kama vile, ukubwa wa hiyo nyumba, idadi ya vyumba vya kulala, idadi ya mabafu, aina ya floor, storage space, jiko, garage ni attached na nyumba au separate. Pia asking price ni muhimu, na ueleze kwamba bei inajumuisha nyumba pekee, au ni + appliances na vitu kama hivyo.
    Phatlorenzo-MN

    ReplyDelete
  15. POLENI SANA WADAU, BEI YA NYUMBA NI MILION 35

    ReplyDelete
  16. Hiyo nyumba haiuzwi wala nini jamaa anaringishia tu. Kama kweli anauza mbona asiweke hata asking price. Wabeba box woote wakiona hujaeka hata teasing price hawaangaiki kuuliza kwa sabu wanaju muuzaji anafanya gelesha tu.

    Huko kwa wabeba box nyumba zinakuwa na bei pale zinapokuwa zinatangazwa kuuzwa, pia huko kwa wabeba box hakuna dalali wa ulongo au nyumba yenye migogoro ya Mirathi au nyumba inayouzwa na mfisadi ambayo itakuletea matatizo baadaye.

    Kwa ivo ukiona wabeba box wamekaa kimya ujue kwanza wamekueshimu, pili hawakointerested na iyo nyumba, tatu wanaogopa kutapeliwa, nne hawana hata hiyo hela, na tano wabeba box kama watu wnagine wana haki ya kusema au kutosema kuhusu kitu chochote kile

    ReplyDelete
  17. ANGALIA HATA BEI YA NYUMBA, KWA BONGO SINUNUI NYUMBA HADI NIHAKIKISHE MWENYEWE...WENGI MATAPELI...NYUMBA NYINGI HASA KAMA HIYO KWA BEI HIYO ILIYOTAJWA BASI KUNA SHAKA...NI KWELI MDAU SISI WABEBA MABOX TUNAJENGA WENYEWE....TUNAFANYA KILA KITU WENYEWE MPAKA TILES TUANATIA WENYEWE. MABOSS WASIOWEZA KUINUA HATA TOFALI NUNUENI...PESA ZA UBWETE ZA MISSADA TUMIENI.....UMESHAONA WAPI MTU ANANUA GARI hata pesa ya mafuta inamshinda? sisi wabeba mabox tunanea uchngu pesa zetu za TAX ZINAVYOTELEKEZWA NA MABOSS WENU...UNANUA NYUMBA KAMA HIYO HALAFU UNAPATIKANA KAMA YALE YA KIGAMBONI......

    ReplyDelete
  18. Two bedroom house unanua kwa £50,000? Wapi huko nije ninunue? Maana huku nyumba zaanza £150,000 tena inakuwa inahitaji renovations kibao, ukitaka nyumba ambayo iko nzuri haihitaji matengenezo basi ununue kuanzia £185,000 na kuendelea. Unless unaongelea kununua kwa mtindo huo wa kukopa ambao ulisababisha uchumi wa US wa kuporomoka, unakopa unalipa karibu maisha yako yote. Ukishindwa kulipa wenyewe wanachukua nyumba yao, sio sawa na kununua inakuwa yako moja kwa moja.

    ReplyDelete
  19. NYUMBA ZA BONGO ZINASHANGAZA UTAKUTA MTU ANAUZA NYUMBA $1000,000.00 HII NI SAWA NA
    TSHS 1,300,000,000.00 HIVI TANZANIA UNAWEZA KUJENGA NYUMBA KWA TSHS 1.3 BILLIONI? LABDA WATAKUJA KUNUNUWA AKINA DAVID BECKHAM. TATIZO WANAFUATISHI EUROPE, WANASHINDWA KUOWANISHA MAMBO YA KIUCHUMI, GHARAMA NI TOFAUTI ZA VITU KATI YA TANZANIA NA ULAYA, KWA MFANO MCHANGA ULAYA UNUNULIWA KWENYE VIFUKO KAMA CEMENT HIVI NA MFUKO MMOJA SOMETIMES UNAPATA KA £3O AMBAYO PENGINE NI SAWA NA TSHS 60,000.00 SASA LORI LA MCHANGA NI VIROBA VINGAPI ILI LIJAE, TUSEMA ELFU MOJA FANYA MAHESABU 30 MARA 1000 = 30,000 AMBAZO NI SAWA NA
    30000X2200=66,000,000.00 HIVI UNAWEZA TANZANIA KUJENGA NYUMBA KWA MCHANGA WA TSHS MILLIONI 66? NDO MAANA ULAYA SODA NI $1 NA BONGO TSHS 500 NA £1 = TSHS 2300

    ReplyDelete
  20. Nyumba nzuri lakini bei unaweza kushangaa na roho yako. Inaweza ikafikia price ya hekalu Wachita, KS...na mishahara ya bongo....havioani kabisa...mtu anataka mark up ya 10000%

    ReplyDelete
  21. Mwenye Nyumba yake Haiuzi alikuwa tuu anataka kuwaringishia, angekuwa anauza angeweka Bei. utatangazaje kuuza kitu bila bei?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...