Home
Unlabelled
from china with love
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Wachina ni wabaguzi sana nashangaa kwanini viongozi wetu wa Afrika wanashupalia uhusiano na Wachina, nafikiri sababu ni moja kwa kuwa wachina wanakumbatia utawala wa kidikteta na viongozi wetu ni madikteta hawataki kutoka madarakani kwa hiari naona wamepata rafiki mwenzao mwenye kufanana na wao kwa sababu Marekani na nchi za Ulaya haziwezi kukubali ubabaishaji wa viongozi wa Afrika kung'ang'ania madaraka na kukumbatia madikteta wenzao kama Mugabe, Kibaki Na Omari Hassan El-bashir kwa hiyo jamaa wanaona heri wakimbilie kwa wachina wasiojali kama wanaua raia zao au la hilo si juu yao wao wanajali biashara tu.
ReplyDeletepropaganda za muamerica hizo, china inakuja juu sana na inamzidi ujanja bara la africa. Wachina wanatoa mikopo bila vikwazo wala masharti ya aina yeyote ile. wazungu wanatupa huku wakitaka watutawale. hiyo news imetoka washinton post unategemea itatoa haki kwa mchina?
ReplyDeleteUkweli ni kwamba mapenzi yako yako kwenye rasilimali na kwa namna uchumi wa kichina unavyokua lazima wavitafute vyanzo vya rasilimali kwa namna yoyote ile. Iwapo vitapatikana kwa kutoa mikopo bila riba, au kwa "kutoingilia" mambo ya ndani na iwe hivyo. Inakadiriwa kuwa ndani ya miaka 10 Uchina itakuwa imeiengua Amerika toka kilele cha uchumi duniani. Kwa maana hiyo, si lengo la mchina (ambaye kiitikadi hapa ni mfanyabiashara) kuanza kutetea haki za kisiasa kitu ambacho kinawweza kumuweka katika mahusiano mabaya na wenye vyanzo vya mali. Ni sisi waafrika wenye kuweza kuamua ni vipi tunakubaliana na mwendo wanaokwenda nao. Tunao uwezo wa kufanya biashara na mataifa ya magharibi, mashariki au hata kuunda kateli zetu wenyewe ndani ya Africa ili tujiimalishe kwenye ushindani na majadiliano ya mikataba. Kwa hakika ningekuwa mfanyabiashara wa kichina - au mwakilishi wake, ningefurahi nikienda Angola niwakute peke yao, nikirudi Gabon niwakute wana matatizo yao na Bongo wana yao. Mwisho, ni lazima tuone kuwa hata hao waamerika wenye kelele kuhusu haki za binadamu inapokuja kujadiliana na Uchina mezani hawalitaji hilo na huo ndo uzuri mmoja wa kuwa mkubwa na mwenye nguvu - kama ilivyo uchina. Kwetu sisi waafrika? Unyonge tunao na hadi hapo tutakapoongea na sauti moja tutaendelea kupigizana kelele.
ReplyDeleteHuu ni wivu tu wa kimaendeleo wa Marekani. Tumekuwa na Urafiki wa miaka mingi na nchi za magharibi, lakini mpaka leo hatuna hata uwezo wakujitegemea kwa maji ya kunywa. Asilimia kubwa tu ya watoto wadogo, akina mama na jamii kwa ujumla wanakufa kwa magonjwa yanayotibika kama Malaria, Viongozi wetu wanaiba mali na kuzificha huko Switzerland, Jersey na kwingineko kwa msaada wa haohao wakubwa. Vita visivyokwisha kila sehemu yenye rasilimali!!
ReplyDeleteWachina ni Mubadala na tuna kila haki ya kuwakumbatia.
Wewe unaongelea ubaguzi china? Hujui historia ya Mwafrika au ya Marekani? Hujui kuna juzi hapa kuna askari wa marekani kagoma kwenda vitani kwa vile haoni uhalali wa Obama kuwa Raisi wa Marekani? Hujui juzi tu hapa majirani walipiga simu polisi na polisi kuja kumkamata prof. akidhaniwa mwizi nyumbani kwake kwa vile ni mtaa maarufu?
China ina historia ndefu na nchi zinazoendelea kuanzia enzi za kupigania uhuru toka kwa hao wazungu wanaotaka kuwachafua wachina sasa hivi. Ni mangapi TZ imefaidika toka uchina baada tu ya uhuru?
ReplyDeleteWanaposema china inataka raslimali tu huku Africa si kingine. Huu ni unafiki at its highest order. Hivi nchi za magharibi hazitaki raslimali za Africa? Vita walivyotupiganisha waafrica (Sudan kusini vs Kaskazini; Angola nk) sababu ni nini?
Tanzania tumegundua uranium mkoani Ruvuma, angalia jinsi Marekani anavyokuja juu kutufanya marafiki wakubwa.
Suala la ubaguzi kila nchi imepitia. Inawezekana wachina ni wabaguzi kwa sababu hawakuwa na interactions sana watu weusi siku za nyuma. Mbona tunawaona hapo kariakoo wakitwanga kiswahili kisawa sawa na wengine hata kuoa wadada wetu.
Ninachochuia nchi za magharibi ni unafiki!!!!
Nipo China mwezi wa pili huu.Kiukweli nimegundua mambo mawili makuu kuhusu perception ya Wachina na ngozi nyeusi.Mosi,ni washamba.Nina maana ya kuwa,hawana uelewa wa kutosha kuhusu General knowledge especially nje ya nchi yao,ukiachia bara la Afrika ambalo mpaka mitaala yao inafundisha Afrika kuna joto la 80 centigrade.Pili hawana reasoning capacity(nazungumzia mtu wa kawaida mchina-aliyesoma na asiyesoma),wao wanadhani waafrika ni maskini wa kutupwa,but hata kwao hapa maskini wa kuomba barabarani wapo (serikali yao tu ndio tajiri).Nawaheshimu kwa uchapakazi na nidhamu(kwa kila kitu).Kudharauliwa kwa ngozi nyeusi ni historia,so ni jambo litakalokwisha as time goes on.
ReplyDeleteEng.Sylva
Propaganda za 'West' hizi;
ReplyDeleteSi bora hawa wanabagua na kusema ukweli kuliko hao wanafiki wanaokuja kuchimba dhahabu yenu kwa 10% huku wakiwahachia mashimo na umasikini mkali.
Heri hawa wanasema wazi kwamba "sipendi black kwa sababu nimesikia ni masikini tangu enzi hizo na mpaka leo bado wako hivyo hivyo". Hachaneni na hizi propaganda, fungueni macho mjue kirusi chenu ni nani!
Nyie watumwa fungueni macho. Ubaguzi ni mbaya ufanywe na mmarekani, Mzungu au Mchina kwamba Wamarekani ni wabaguzi haihalalishi Wachina kuwa wabaguzi. Two wrongs do not make a right. Mwingine anatolea mfano wa Wachina walioko Kariakoo wakati wewe mumatubi ukienda kwao huwezi kufanya biashara za namna hiyo.
ReplyDeleteMtu huru
Check hii quote kutoka kwenye hiyo article.
ReplyDeleteChen Juan, 27, a secretary in an English-language training school in Beijing, regularly uses skin-whitening products and carries an umbrella on summer days. "For me, the whiter, the better. Being white means pretty," she said. "If someone looks too black, I feel they look countrified and like a farmer. . . . Being white is prettier than being black."
"In my impression, black people, especially Africans, are not clean enough," Chen continued. "To be frank, I just feel black people are too black. Definitely, I wouldn't consider having a black guy as my boyfriend even if he were rich."
Kuna watu bado wana mawazo hayo katika dunia hii ya leo, wala sishangai, inasikitisha. Lakini utafanyaje. Waafrika inabidi tuungane, tusisubiri kukubali, kwa sababu kama huyo alivyosema, hata ukiwa na elimu, pesa, ustaarabu bado unaonekana ni kichefuchefu.
Pras wa Fugees aliwahi kusema 'the darker the black man, the better the next man'....
haya sasa waafrika amkeni?
ReplyDeletewachina ni MACORUPT WAKUBWA ACHENI KUWAKUMBATIA
"To be frank, I just feel black people are too black. Definitely, I wouldn't consider having a black guy as my boyfriend even if he were rich."
ReplyDeleteMbona hapa bongo hawa akina dada tunawapata kirahisi tu na hawana matatizo yoyote. Mimi nadhani hiyo article haina ukweli wowote ni propaganda za magharibi.
watanzania acheni kujifanyankila kitu mnajua,haya mambo ya ubaguzi ,yapo kila sehem dunia sio wazungu,wahindi,wachina ,waafrika,kila sehemu ukienda duniani kuna kubaguliwa na kubagua,kuna kipindi dada yetu mmoja mrembo alishinda taji la miss tanzania,lakini cha kushangaza watu wengi walipinga kwa sababu hana asili ya kiasia.,muhimu kusoma ,kuchakarika,kuwa na maendeleo yako safi uone kama mambo eti sijui ,wazungu ,sijui wachina ,sijui wahindi wabaguzi kama yatakuwa na nafasi kwa,hoa mnaosema wabaguzi mbona wengi sisi tunawachukua kama ubua tuu,na wengine tunakutana nao huku mitaa wanatuomba fwedha,shikeni pesa ,pesa ndio boss ulimwenguni sio rangi ya ngozi ukishika pesa hata kama mweusi na ukijikojolea na kumwambia mzungu akufute mikojo yako utapata wa kufanya hivyo.kwa sababu ya pesa.mnaoumia na huo ubaguzi ushauri ndio huo,chakarikeni tuu ,msichunguze mambo mengine.
ReplyDeleteZhou Lin, I challenge you to prove the claim of such unimaginable level of ignorance. I am sure the article or whatever the source was must have referred to Fahrenheit as human life cannot be sustained at 80 degrees celcius! The highest temperature ever recorded (in the world) was 57.8C in Libya and I bet the Chinese know that too.
ReplyDeleteHivi kuna mtu asiyejuwa kuwa wananchi wa china ni masikini?
ReplyDeleteHuu ni wakati wa CHANGE,heshima kwa Waafrika wote.
Kuzuia wale wote wasiolitakia mazuri bara letu.
Tumechoshwa na Afrika kuwa jalala kwa baadhi ya nchi ambazo zinaleta takataka na kupotosha watu kuwa wanasaidia.
Watupatie misaada ya matrekta na mashine za kuvunia mpunga basi:)
Kwanini hawatusaidii mashine za kuvunia mpunga kama wanatupenda?Badala yake wanatuletea mpunga wa kwao ili tununuwe?
kwani mpunga wa Kyela na wa kwao upi mtamu?
ukweli ni kwamba kuna mashine ambazo zinaweza kuvuna na kutenganisha mchanga na mpunga,na kama tukizipata hizo pamoja na matrekta basi shida ya njaa tunaweza kuisahahu.
Haliwi mtu hapo :)
Afrika ilikuwa na heshima yake ,imani yake ambayo ilijengwa kwa upendo wa hali ya juu bila ya ubaguzi wa dini tulizoletewa.
Tuna uwezo wa kisayansi n.k
hapo ndipo ilipoanza busara+Binadamu wa kwanza waiishi hapo, kwa wasomi wa historia wanakubaliana na hili popote pale duniani :)
Siyo kwamba tunaubaguzi,tunawapenda wote wale wanaotupenda na wasiotupenda tunaachana nao.
Wabaguzi hawakaribishwi kabisa Afrika,wakome ....
Afrika ina ardhi nzuri kwa kilimo. n.k .......Kilimo ni uhai
Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania
Al Musoma, ninapokuambia jamaa ni wajinga ( watu wa kawaida) si kwamba nimesikia au nimesoma, nipo huku na najionea.Ukweli ni huo,na hiyo nilitoa kama mfano tu.Hata historia ya nchi yao wanaipindisha(kwenye mitaala yao),taarifa zozote potofu kuhusu nchi yao hazijulikani kwa watu wa huku,ni wasomi tu ndo wenye uwezo wa kutambua ukweli.Hapa nilipo nilifanya kazi ya ziada TV ya chumba changu kuona BBC na CNN, ukimuuliza mwanafunzi wa chuo atakujibu hajui kabisa BBC wala CNN.
ReplyDeleteZhuo Lin
Chinese are racist and not only in China but whenever and wherever their numbers are substantial.
ReplyDeleteThis news is not biased at all against Chinese, during Olympics, restaurants in China were not providing services to black athletes, because they were considered to be, Pimps (Makuwadi), Prostitutes and drug dealers. http://shanghaiist.com/2008/07/18/the_racist_games.php
SO if anyone thinks that, this is Americas propaganda, wake up and smell TAZARA ordeal in Chinese hands. They took a lot more than the 10 billions they are giving back to a whole continent. It is not known, how much of Tanzanias, natural minerals were stolen from Tanzania, during TAZARA railway construction. Many people coming here, were probably not conceived during TAZARA inauguration on 26 October 1970, all they see is, this being a job of imperialists pot, calling a kettle black.
Read further on TAZARA/CHINA issues and learn here [url=http://escholarship.org/uc/item/2037d9f7]TAZARA[/URL]
Chinese, give out rules not to hire black people in their firms simply because they are black, they are also very superstitious and believe, black people will bring bad luck. However, it would stupid to do the same in Africa, but that does not mean an AFrican in Africa will be a manager leading Chinese in African venture.
To connotate, if they are racist, why are they in African Continent, would be saying, if Boers, Afrikaans, are racist why did they end up in South-Africa! Which is lame excuse. You can not generalize concepts, but when a government dictates, or turns a blind eye, then, we have no choice, but to express the true sentiment towards its citizens.
AND currently China is at that stage. China has already surpassed USA economically, no doubt, but in orde for them to emerge victorious, they have to make sure there are no victims. You cant be Chinese first, if you were born in Tanzania, you are Tanzanian of Chinese descent, which is not the case with Chinese, Indians and other Asian countries. You cant bring Arabs into this, because, as much as how racists they can be, they are a majority in African continent. Egypt, Libya, Algeria, Tunisia, Morroco, etc, etc are fellow Africans, who became racist economically, not because there arent Arabs who are black in complexion.
Issa thank you for posting this.
Macho ya kuvimba ooops wachina ni wabaguzi wakubwa hasa hasa kwa waafrika.Ni wakatili kuliko wadosi!!!Sema kama kawaida yetu tutawakaribisha na meno yote nje halafu siku ya siku watafanya yale ya ngamia na tajiri wake jangwani.
ReplyDelete