JK akimfariji Mzee Philipo Pagali mkazi wa kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo ambaye nyumba yake aliyokuwa anaishi iliharibiwa vibaya na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni.Jumla ya nyumba 51 ziliezuliwa mapaa na kuharibiwa mapaa na kusababisha watu zaidi ya 190 kukosa mahali pa kukaa na kulazimika kuhifadhiwa na majirani
JK akukagua baadhi ya nyumba zilizoharibiwa vibaya na mvua kubwa iliyombatana na upepo mkali katika kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo hivi karibuni wakati alipotembelea kijiji hicho leo asubuhi.Jumla ya nyumba51 ziliharibiwa vibaya na mvua hiyo na kusababisha watu zaidi ya 190 kukosa makazi na kuhifadhiwa na majirani. Picha na Freddy Maro.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Maisha bora kwa kila mtanzania au kilimo kwanza??

    ReplyDelete
  2. Nigeria 3 kenya 2, wapopo ndani ya world cup 2010 SA mbona raha !!

    ReplyDelete
  3. Jamani ndugu zangu watanzania hizo ndo nyumba za kustahimili dhoruba kweli? you must be kidding me! Tanzania tunahitaji mapinduzi ya kiuchumi la sivyo watanzania wengi vijijini wataendelea kusahaulika na kwamwe hawatakaa wafaudu matunda ya uhuru. Viongozi wanapaswa kuweka mipango mathubuti ya kumkomboa mwananchi wa hali ya chini kwanza. Now you make me remember Mwalimu Nyerere na azimio la Arusha! Inatia huruma kwa mtanzania anayeendelea kuishi kwenye nyumba kama hiyo iliyozuliwa na upepo na sidhani kama zina hadhi ya kutwa nyumba labda tuite vibanda! Samahani kwa hili lakini ninazungumza kutoka moyoni!

    ReplyDelete
  4. sasa serikali imetoa msaada gani kwa waaithrika?

    ReplyDelete
  5. Wewe Tarehe Sat Nov 14, 09:02:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
    Kwanini Serikali itoe msaada kwa waathirika? Kwani hao waathirika hawakujua kuwa kuna Insurance (bima) kuzikatia hizo nyumba zao? Kama magari tu kama una bima je kwanini utarajie serikali ije ikutengenezee gari yako ukipata ajali?

    ReplyDelete
  6. Yeah Serikali inatakiwa kutoa something for at least 24 hours. Bima itakulisha kwa siku za mwanzoni. Hebu mufikiri kabla hamjaongea. Gari na nyumba ni kitu tofauti.....Natural disasters zikitiokea serikali inatakiwa angalau kuwalisha watu kwa siku mbili...na kama nchi zilizoendelea zinawahifadhi hata kwa miezi 6....

    ReplyDelete
  7. kitu kimoja ninachompendea mhe rais jk, hata kuwepo na maafa kiasi gani yeye anatabasamu na kuweka mikono mfukoni kana kwamba hakuna janga lililotokea. kwa walio karibu naye, kweli huwa ananuna au kuonyesha huzuni?
    ninatoa heshima: maisha bora kwa kila mtanzania! kilimo kwanza!

    ReplyDelete
  8. CNN: Landslides kill 20 in Tanzania.

    ReplyDelete
  9. BIMA YENYEWE HUPATI HADI ULISHE RUSHWAAAA...KWELI INABIDI WAWASAIDIE WAATHIRIKA KWA MUDA...KWANI KWENDA SHULE KOTE HAWAJUI KUNA MFUKO MAALUMU WA KUKABILIANA NA NATURAL DISASTERS...AU MPAKA TUOMBE???/

    ReplyDelete
  10. wewe anony Sun Nov 15, 02:05:00 AM acha kukurupuka. serikali ambayo iko responsible kikweli kweli ilitakiwa kufanya kitu hapo, hiyo ni natural disaster, siyo short ya shirika la kugawa giza nchini (TANESCO). regardless kama una bima au la (unakumbuka katrina? kwa nini bush alipigiwa kelele kwa serikali yake kuchelewa kufanya kitu? wale hawakujua kuwa kuna bima??) acha ujinga. Ila hapa bongo ndo tushazoea.
    Mdau, DSM

    ReplyDelete
  11. we unayedai ati rais huwai anacheka sijui bla bla gani ulitaka alie??

    ReplyDelete
  12. hahahahahaa
    sio la kucheka ila sina mbavu jaman

    eti tabasamu,kilimo kwanza

    hahahaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...