Mlezi wa Klabu ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa Shule ya Sekondari Kingurunyembe, Lawrence Kung’alo ( kulia) akielezea mchiro uliochorwa na mmoja wa msanii wa sanaa ya uchoraji , wakati wa mjadala wa mdahalo uliohusu Kero za Rushwa katika Idara ya Elimu kwa baadhi ya wanafunzi wa klabu za kuzuia na kupambana na Rushwa wa shule za Sekondari ya St Dennis, Kingurunyembe na Morogoro Sekondari, jana ( Nov 14) mjini Morogoro.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Fatma Mwassa, akiongoza msafara kuvuka katika daraja dogo lililojengwa kwa miti katika barabara ya kwenda kitongoji cha Mapangano , Kijiji cha Kanga, ambako msitu wa hifadhi wa asili umahujumiwa na wananchi wa maeneo mbalimbali


Wakazi wa Manispaa ya Morogoro wakiwa katika foleni wakisubiri kujiandikisha kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa macho na wataalamu wa macho kupitia kambi ya Klabu ya Lions ya Dar es Salaam – Mzizima , ambao ulifanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro jana



Askari wa kikosi cha Usalama Barabarani wa Wilaya ya Mvomero, akishiriki kazi ya kujitolea ujenzi wa kiwanda cha kusindika nyanya cha Kijiji cha Kipera, bila kujali aina na mavazi yake akiwa amepokea ndoo iliyojazwa kokoto kwa ajili ya uwekaji zege ( wanne kutoka kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya. Picha na mdau John Nditi.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...