Washiriki wa shindano la umalkia wa Kisura wa Tanzania wakiwa na wasimamizi wao na wapiga picha wa kampuni inayoongoza kwa kazi hiyo ya Sophia Productions wakipozi kwenye magofu ya kale ya karne ya 13 yaliyopo Kaole nje kidogo ya Bagamoyo ikiwa ni mojawapo ya shughuli zao wakiwa kambini kwao hoteli ya Kiromo ambayo imewadhamini kwa mwezi mzima wa kambi. Meneja wa mradi huo Grace Kilembe ameketi wa pili shoto na anayemfuatia ni mshindi wa mwaka jana Emmy ambaye kwa sasa anafanya kazi za umodo sauzi na kaja kusaidia kazi ya kusimamia warembo hawa
warembo wakipozi katika magofu ya Kaole. Chini wakirejea kambini
WASHIRIKI wanaowania umalkia wa Kisura wa Tanzania, ambao waliingia kambini mwanzoni mwa mwezi huu katika hoteli ya Kiromo iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani wanaendelea na mazoezi pamoja na kupata mafunzo ya umodo.

Meneja Mradi wa kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency, Grace Kilembe, anasema washiriki hao walipatikana kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

Aliitaja mikoa iliyofanyiwa usaili na kuwapata washiriki hao kuwa ni Singida, Dodoma, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Arusha, Mara na Dar es Salaam ambapo waliwapata wasichana 20 wenye vigezo vya mashindano hayo.

Aliwataja wasichana hao na mikoa waliyotoka kwenye mabano ni Mwajabu Juma (Mwanza), Lucky Mwakatobe, Resson Soto (Arusha), Jack's Oyombe, Alinda Lema, Violety Mganga, Sharon Silas (Dar es Salaam), Jackline Benson (Arusha) na Gloria Gilbert (Tanga).

Wengine ni Glady Molel, Lightness Mwanga, Mwatatu Francis, Mary Joel, Shamim Babu (Manyara) na Mary Mallya (Dodoma), Asnat Mohammed na Diana Ibrahim (Mara).

Washiriki hao watakaa katika kambi kwa muda wa mwezi mmoja na wiki mbili huku wakitoka mmoja mmoja mpaka watakapobaki 10 ambao wataingia fainali ya mashindano hayo.

Grace alisema visura 10 watakaoingia fainali hiyo watapatikana kwa njia ya kupigiwa kura na watazamaji wa televisheni ya TBC1.

Mashindano ya Kisura wa Tanzania yamedhaminiwa na Serengeti Breweries Limited (SBL), Kiromo Resort, TBC1, Clouds FM, FHI, ATC, Entertainment Masters, Mwananchi Communication, Hugo Domino, Mercy G Parlor Beauty na Bang Magazine.

Grace alisema mwaka huu walijitokeza visura wengi katika hatua za awali tofauti na mwaka jana na kuwapa moyo waandaaji hao kuwa, wengi wameanza kuyaelewa mashindano hayo na manufaa yake.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. washamba sana na hivyo vinguo vyao vya kariakoo vya shs miamia! utafkiri vikahaba vinjiuza! watage of time! mamiss tulikuwa sisi bwana ukiniona kuleeeeee huulizi km ni mrembo au la jibu unalo.. siku hizi bongo hamna kitu, umiss imekua source of income na uchocheaji wa biashara ya ngono!!

    ReplyDelete
  2. wewe Anon 11:02:00 AM
    Jaribu kuwa na mtazamo safi,mtazamo wako wa sasa ni ugonjwa wa roho mbaya,fanya mazoezi kuwa na fikira na mtazamo wa upendo,ndio tiba ya ugonjwa wako wa roho ya kwanini

    ReplyDelete
  3. Anony wa pili umenifurahisha sana sure wewe ni dokta, ndugu akifuata ushauri wako atapona haraka saanaaaa. fanya hima ndugu utakufa bure na kijiba cha roho.

    ReplyDelete
  4. Sasa hao ni washiriki wa kisura wa Tanzania au kisura wa hiyo mikoa kwani sioni mwakilishi toka Lindi au Lindi siyo Tanzania??? kengeeee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...