Tovuti inayohusika na 2011 Diversity Visa Program (DV-2011) ilikuwa na kwikwi kwa muda na kusababisha watu kukwama kutumia Photo Validator na ule ukurasa waku-submit fomu.

Wavuti.com ilijitahidi kuwasiliana na wahusika (unaweza kusoma mtiririko wa mawasiliano hayo kwenye wavuti.com) na hatimaye baada ya danadana ilitua kwenye deski husika, marekebisho yalifanyika na sasa mambo ni mswano.

Mnaotaka kujaribu bahati yenu msikate tamaa.
Napenda kuwafahamisha wale wanaohangaika kutuma picha kuwa tumieni tovuti ya:


itarekebisha picha chapchap na kukuondolea usumbufu!
Picha na maelezo ya ziada kwa anayetaka, vinapatikana katika wavuti.com
Tunakutakieni bahati njema!
Ni hayo tu.
Subi wavuti.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. HII SHIDA ILIKUWA LINI? JUMANNE HII NIMETUMA MAOMBI YANGU, AU ILITEGEMEA NA NCHI ULIYOPO!!!! ALAFU JUU YA PHOTO VALIDATION, UKIWA NA SCAN ZA EPSON ZINAKUJA NA SOFTWARE YAKE YENYE UWEZO WA KUKUREKEBISHIA PICHA YAKO, UKIWA NA MODEL ZIFUATAZO (1) EPSON STYLUS SX205, NA (2) EPSON PERFECTION V350 PHOTO, HIZI ZINAKUJA NA SOFTWARE COOL, PIA KAMA UNAWEZA KUPATA SOFTWARE INAITWA PHOTO IMPRESSION, UNAWEZA KU-RESIZE PICHA ZAKO UKAPATAVIPI VINAVYOTAKIWA VYA GREEN CARD LOTTO.

    ReplyDelete
  2. SASA HIVI CHA MUHIMU NI GREEN CARD YA CHINA....

    ReplyDelete
  3. Dub we anon wa Thu Nov 12, 01:37:00 PM, umeniacha hoi kweli kweli.

    Wakati nyie mnagangania green kadi za uchina na USA wenzio wenu wa nchi zingine inkluding Uchina wanagangania kuja bongo, wakenya ndio usiseme. Haya weee ama kweli penye miti hapana wajenzi.

    ReplyDelete
  4. mkataa kwao...........

    ReplyDelete
  5. HATA mimi nimeshangaa mtoa maelezo anasema jaribu bahati, hii ni bahati kweli?? basi hata watumwa wa karne ya 18 walikuwa na bahati kuuzwa utumwani. Mtizamo tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...