REBEKA GETACHEW-23YEARS (ETHIOPIA)
4. SEFORA MESSELE GHEBREEZGABIHEIR-18 YEARS (ERITREA)

MARRY KIRABO -18 YEARS (UGANDA)

AKAZUBA CYNTHIA -20 Y(L)and MAHORO ANNET-23 Y (R)
(RWANDA)
ALIDA GROLIA KANEZA-19 YEARS (BURUNDI)

QUEEN BELLE MONIQUE-23 YEARS (BURUNDI)

AKAZUBA CYNTHIA-20 YEARS (RWANDA)
SELAMAWIT ZERABRUCK GHEBRESLASSIE -18 YEARS (ERITREA)

Warembo wanaoshiriki mashindano ya kimataifa ya MISS EAST AFRICA 2009 wataanza kuwasiri Nchini tarehe moja mwezi ujao kwa ajili ya mashindano hayo yanayosubiliwa kwa hamu kubwa na watu wengi Barani Afrika.

Wakiwa jijini Dar es salaam, warembo hao watafikia katika hoteli ya kimataifa ya Kunduchi Beach Hotel & Resort ambayo ndiyo hoteli rasmi ya mashindano ya Miss East Africa 2009.

Mashindano ya MISS EAST AFRICA 2009 yanatarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi ujao katika ukumbi wa Mlimani City jijini dare s salaam na yatawashirikisha warembo kutoka Nchi 14 za ukanda wa Afrika mashariki ambazo ni pamoja na wenyeji Tanzania,
Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Nchi zingine zinazoshiriki katika mashindano hayo ni Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Somalia, pamoja na visiwa vya Seychelles, Comoros, Madagascar, Reunion na Mauritius.

Mashindano hayo yanayoandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Limited ya jijini Dar es salaam yanatarajiwa kutizamwa na watu zaidi ya millioni 200 kupitia katika Television barani Afrika.

Mrembo Claudia Niyonzima wa Burundi ndiye anayeshikilia taji la Miss East Africa kwa sasa.

Rena Callist
Chairman
MISS EAST AFRICA PAGEANT











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Jamani huu ni uonevu sasa mbona hamjatuwekea na sisi Miss TANGANYIKA wetu hii si haki

    maria

    ReplyDelete
  2. Wamteue tu mmoja kati ya hao wa eritrea awe mshindi.watoto wameumbika hao duh!

    ReplyDelete
  3. Mimi naona hao wanatosha kwa sababu mshindi tayari anaonekana - SEFORA MESSELE ERITREA).

    ReplyDelete
  4. Ujinga mtupu! MuEthiopia hajioni MuAfrika hata siku moja. WaEthiopia wanatuita Bariah WaAfrika tunaotoka Sub Sahara.

    WaTutsi, WaEthiopia awe MuAhara, MuTigrinya, au MuOromo wabaguzi vibaya sana na hawajioni kwamba ni WaAfrika.

    ReplyDelete
  5. Afrika ni kubwa na siyo tu ya sisi wenye pua kubwa na tu nywele tudogo.Acha roho kutu anony wa Nov 16 05:40 Wake up!!!

    ReplyDelete
  6. Dar patakuwa hapatoshi kama quality yenyewe ndiyo hiyo...nawaonea huruma mademu wetu wa bongo hivi kweli watawashinda hao ??? kwa kweli 1+1=11 habari ndiyo hiyo !

    ReplyDelete
  7. Mdau wamekubagua labda lafizi kigugumizi. Mimi najimwaga Maithopia kwa mwezi mara moja na hukaa over da wikiendi sijbaguliwa hata siku moja. Jamani changeni mjimwage Ethiopia hata mara moja in life time jamani ni wazuri mno.

    Ma wife alilalama mpaka amekubali matokeo. Na mimi ni mbantu tii. Acheni kuwapaka watoto wa watu.

    ReplyDelete
  8. Sukununu, TangaNovember 17, 2009

    Eeh Mola wangu nijaalie namimi nipate angalau nauli ya kunipeleka Ethiopia na Eritrea angalau kwa wiki moja tu nikajirushe na vimwali hivi. Nasikia hawa kwao "kunyima ntu dhambi".

    ReplyDelete
  9. Jamii yoyote iliyojengwa kimatabaka ubaguzi ni lazima utakuwepo. Ethiopia ni jamii iliyojengwa kimatabaka. Ikiwa kama MuAmhara anajisikia ni superior kwa MuOromo au MTgrinya sijui wewe ambaye wanakuita Bariah utakuwa katika strata ipi?

    Siku moja colleague wangu alistuka sana kumsikia dada wa KiEthiopia akimwambia mwalimu "..I am not African.." Mwalimu akamwambia "..But you are from Africa, aren't you?.." Yule dada akajibu "..Yes I am from Africa but I have colour.." Mwalimu akachanganyikiwa. Colleague wangu ambaye ni MuAfrika magharibi alikuwa hajawahi kusikia hayo mambo akastuka akamwambia "..What you mean by sayin' you have colour?.." MuEthipia akakomaa "..I am not black like you I have colour like teacher.." Muwest Africa akaishiwa nguvu akasema "..God help Africa we have too many problems to solve.."

    ReplyDelete
  10. WOW....WATOTO WAKIETHOPIA NA ERITRIA WANAPENDEZESHA BLOGU YA JAMIII DUH....MMATUMBI UMEMPA JIBU LINALOMFAA HUYO ANON.... SIO WAREMBO WAKIBONGO WAKIWA KWENYE BLOGU YA JAMII DUH PODA YAO NI UNGA WA SEMBE HALAF KUKOMAA NDO USISEME...SELAMAWATI NIMSHINDI NO.1 HATA BILA KUWAPAMBANISHA...CANT WAIT TO SEE THEM LIVE.
    PEACE AND LOV

    ReplyDelete
  11. I HAVE MADE UP MY MIND. NAHAMIA ERITREA. VITA KITU GANI BWANA
    Mdau, deslam

    ReplyDelete
  12. Nadhani mashindano haya yanasubiriwa kwa hamu kubwa kuliko mashindano yote ya urembo yaliyowahi kutokea tanzania, hawa watoto si mchezo, Mungu kweli yupo!

    Asmara ni mji mzuri sana, niliwahi kusoma article moja. Wana majengo ya kale waliyoacha waitaliano, hakuna vita huko, ingawa wana mtafaruku mara kwa mara na waethiopia na wamarekani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...