watanzania wenzangu tulokuwa nje ya tanzania. mie ni mtanzania halisi lkn niko nje ya tanzania kwa muda wa miaka 14 kwa sasa lkn kitu kinachonishangaza tanzania unaposhuka uashamaliza kuchukua mizigo yako unakutana na jamaa wamekaa maksudi wanasubiri kupekura mizigo yako!
jamani mie naomba suala hili lifanyiwe kina zaidi sidhani kama wenzangu inawapendeza hali hii manake mtu umetoka safari pengine kwa masaa 10 au zaid unapofika home unataka ukapumzike leo unaambiwa funguwa mabegi yako, hlf unaanza kuulizwa hichi nini na hichi nini.
tabia hii kusema kweli sio nzuri hata kidogo kwa sababu sie tunaotoka ulaya au nchi zenye maendeleo mizogo yote huwa tayari usha scania kitaalam na ndio maana tukawezakutuwa nayo leo wao wanatupekuria kama kutukashif akina mama hatuna stara.
ukitoka tanzania kwenda nje ya nchi mizigo yako wanascan basi hawafunguwi ndani kupekura kuuliza hichi nini wala nini jamani haki iko wapi na ustaarabu uko wapi tunashindwa na watu walokuwa hawana desturi mie naomba nipate msaada jee nikaonanae na nani ili nilkiongelee suala hili manake imekuwa dhiki kwa sasa

mdau maryam said khalfan
london.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. wewe ulitakaje? Kama umeshuka na bwimbwi toka kwa 'Bibi' wasikukague kwa nini?

    ReplyDelete
  2. NAPENDA WATANZANIA WENZANGU TUPUNGUZE MALALAMIKO AU KULALAMIKIA JAMBO AMBALO HULIJUI VIZURI, UKWELI WA MAMBO NI KUWA HAO WANAOFUNGUZA MABEGI NI MAOFISA WA USHURU NA FORODHA LENGO NI KUANGALIA KAMA KUNA KITU CHA KULIPIA KODI, UTARATIBU HUU UKO KILA PAHALA, KWA WALE WASAFIRI UTAKUTA PAHALA NOTHING TO DECLARE OR THINGS TO DECLARE NA PANAPOSHAKA MIZIGO PIA HUFUNGULIWA SI MAREKANI WALA ULAYA NI DUNIA YOOTE. ANKO MICHU HII USIIBANE

    ReplyDelete
  3. we watie mikongoto wakijaribu kufungua mizigo yako, nilimpa jamaa mmoja pale wizi dar airport mkongoto atakaa asahau! aliniuliza kaka ebo fungua mizigo yako nione umebeba nini, kwa hasira nimpa kofi moja safi sana, halafu nikamwambia tewnde mbele ya sheria, akaniomba msamaha mambo yakaisha, si ni mkongoto tu usisubiri sheria wala nini kwani Tz hakuna sheria yeyeto. tahnx

    ReplyDelete
  4. mie nyiew mnaokaa nje ya nchi mnanikera sana. kwahiyo sababu mwingereza ka-scan mizigo yako basi mtanzania asihakikishe kama unavyoingiza ni salama. mama, "halali yako ni haramu ya mwenzio". inawezekana kuna vitu kwa mzungu ni halali lakini kwa mtanzania ni haramu. acheni kasumba. mara ngapi tumeshuhudia jinsi ambavyo wazungu hawajali nchi za dunia ya tatu? wanatuletea vitu ambavyo vimepitwa na wakati na havifai kwa binadamu wala mazingira. ebu ninyamaze manake nachoka na ili tabaka la wanaoishi ughaibuni.

    ReplyDelete
  5. sasa mbona mimi nilipekuliwa Heathrow airport na mizigo yangu ilikuwa imeshakuwa scanned huku? tena nilisharuhusiwa kupita lkn askari mmoja akanihisi kitu na kuniamuru nifungue begi akapekua kweli tena paka chini na akanikuta na bunda 3 za sigara akaniuliza kama zote ni zangu nami nikamjibu ndio na akaniruhusu niondoke kwa kweli begi halikufunga tena maana alipekura haswa, mi nadhani sio suala la kumuona nani wala nani ni utaratibu ambao upo kila mahali.

    ReplyDelete
  6. mdau pole sana kwa kero za wafanyakazi wa airport yetu ya bongo..

    Kwa kweli hata mimi nakareheka sana jinsi wafanyakazi wa airport walivyokuwa na tabia ya kupekua mizigo ya abiria wanaoingia. Mimi nina mfano halisi: mwaka jana nilikuwa nakwenda Tanzania kwenye mazishi ya mama yangu mzazi, tulipotu Dar issue ikaanza vile vile JE UNA MZIGO WA BIASHARA? FUNGUO, OH SIJUI NINI. Nikawaeleza sina mzigo wa biashara isipokuwa nina mashada ya maua ambayo yatatumika kwenye mazishi, lakini hawakuamini mpaka nilipofungua masanduku. muda huo nilikuwa nawaambia kwamba nachelewa kanisani kwani ibada ya mazishi ilikwisha anza lakini bado walisisitiza kutaka kuona kilichoko kwenye masanduku. JAMANI KAMA TAKUKURU WAPO NA WANAFANYA KAZI TAFADHALINI NENDENI AIRPORT YETU MKAJIONEE JINSI MAOFISA WA WANAVYOPOKEA RUSHWA. MBONA ABIRIA WANAOONDOKA HAWAPEKULIWI KIIVYO? Kuweni na ustaarabu kwa wenzenu.

    ReplyDelete
  7. wewe kiazi kweli yaaani unataka upite bila kukaguliwa kisa umetoka ulaya! Wao wana scanner ndio lakini bongo hakuna scanner Mbona wao wanatupekua hand laggage zetu mpaka wanataka kujua umebeba sh ngapi

    ReplyDelete
  8. POLE SANA MDAU, ILA MWAMBIE MICHUZI AKUTAKE RADHI SENTENSI ZAKO HAZIJAKAA VIZURI KIASI KWAMBA NI VIGUMU SANA KUJUA UMEZUNGUMZIA NINI KWA MTU ASIYEJUA KUKISIA. NA HII YOTE NAHISI ATAKUWA MICHUZI NDO AMECHEMSHA SIDHANI KAMA HUKO ULAYA UTAKUWA BADO SOMO LA KUSOMA NA KUANDIKA LINAKUSUMBUA. MAANA HAPA MTU MWINGINE AMBAYE HAJABARIKIWA UJUZI WA KUKISIA MTU ANATAKA KUONGEA NINI, ATAAMBULIA TUU KUJUA KWAMBA WEWE UPO ULAYA.

    MDAU TUKUYU

    ReplyDelete
  9. MIMI NIMESAFIRI NCHI MBALI MBALI MPAKA DEVELOP. ISSUE YA UPEKUZI IKO KILA NCHI NA KWA SABABU MAALUM KAMA VILE KUANGALIA MADAWA YA KULEVYA, KUINGIZA BIDHAA AMBAZO VIMEPIGWA MAARUFUKU KAMA NYAMA HAPA ULAYA, KULIPIA USHURU WA FORODHA N.K.

    KITU MUHIMU TU NI MSAFIRI NA MPEKUZI KUWA WASTAARABU.

    ReplyDelete
  10. yeh nchi za ulaya wanapekura mizigo baada ya kuscan na kuhakikisha kwamba kuna kitu ndani ya mabegi yako lkn tanzania kila mtu wanampekura mabegi hakuna nani wala nani isipokuwa mgeni kama mzungu hawampekuri mzitake kutetea na ukweli upo na mbona tukiondoka wanascan tu mizigo hawapekuri kwa macho kwa kuwa hawana haja na chochote wnajuwa unatoka nchin i lkn ukirudi wao wanapekura inda juzi mtu kaaambiwa toowe zawadi akalipa 10 pound msitetee ni kweli wnataka rushwa tanzania inasifika kwa rushwa dunia nzima wanapekura panapo dharura tufaham jamani tusiteteee kwa kuwa nchi yetu wao wanapekura anaeshuka yoyote yule wao wapekure mbona hatuku piga kelele kuhusu bandarini wao haki yao wapekure njie RUSHWA IMEZIDI NYUMBANI NA UDHALILISHAJI

    ReplyDelete
  11. dunia nzima wanapekura lkn tanzania wanapekura bila dharura wao wanapekura wapate hongo na rushwa sio tabia nzuri jamani

    ReplyDelete
  12. Tabia hiyo inakera sana hasa pale mkaguzi anapotumia ubabe na kutomjali msafiri. Unakuta watu wamekaa kizushi zushi tu hata salam wala maelekezo hakuna wanakuvamia tu.

    Yalinikuta nilikuwa naenda msibani mkoani basi acha nisumbuliwe na nilikuwa na sanduku linanguo za mtoto mdogo, basi wanapekua utadhani wapo dukani wanataka kununua nguo. Hawapo makini kabisa na kazi yao walinikera kweli.

    Watu kibao wanapita bila bila hata kuguswa wao wameshupalia rushwa tu eti tugawane ``zawadi`` Nikawaambia jamani mmemaliza? Maana walishaanza kunikera pale walipoanza kuniuliza hiki nini hiki nini, vilikuwa vi pipi vya mtoto na vimeandikwa ki english na karatasi inaonesha kilichopo ndani. Nikawaambia nawahi msibani wakaanza kunifokea eti ulilazimishwa kuja? Kama vipi usingekuja.

    Halafu hawana sehemu maalum yakukaa, siku hiyo walikuwa wamekaa jirani na sehemu yakuchukulia mizigo, huwezi hata kuaamini kama watu wapo kazini.

    Mnaowatetea hamjafikwa na mkasa huu.

    ReplyDelete
  13. Pole sana mdau kwa yalio kukuta, maana mimi pia yalinikuta hayo pia bora wangenipekua ningejua wako kazini ila walianza kuniuliza nina tokea wapi?? huko niliko nina fanya nini?? na nilifanyaje fanyaje kupata chance ya kwenda ulaya, yaani siku amini nilihisi kama naota vile, sasa sikuelewa wana maana gani na maswali hayo mie najua, ukirudi home hamna usumbufu maana tunapo enda nje hayo maswali yana hitajika,wajue unaingia nchini kwao kufanya nini nasio ukirudi nyumbani.Yaani ni kazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  14. Nahisi hao wanaotetea ni hao hao wala rushwa au jamaa zao na wananufaika kwa namna moja au nyinghine katika udhalilishaji huo, nasema udhalilishaji sababu wanaopekuwa hawapekui kistaarabu wana chambua chambua vitu ovyo, vichupi, visidiria, vipedi vinanyambuliwa mbele ya watu, na kama alivyosema mdau mmoja hata wakimaliza begi halifungiki tena, na mbaya utakuta kigurupu kizima kimemsimamia mtu mmoja wanayemhisi watapata kula wakati abiria wengine wanapita haoo.. yaani utaona tu sura zao si kama wapo kazini sura zao ni njaa njaa tu hamna lingine na wanasubutu kukupangia na bei ya kuwapa kama mmenunua pamoja na wana vijana wao wanaowatuma wakufate nje ili wawapokelee hiyo rushwa!

    ReplyDelete
  15. NDG WADDAU,UKAGUZI(RANDOM/ROUTINE SEARCH)UKO DUNIA NZIMA,MIMI BINAFSI NIMEBAHATIKA TANGU NIANZE KUSAFIRI SIJAWAHI KUSACHIWA TZ,ILA KILA NIKIJA WANANIULIZA UMEBEBA NINI NA UNAFANYA NINI ULAYA,NIKIWAAMBIA TU NASOMA WANANIRUHUSU KUPITA,NAJUA WANAJUA STUDENT CHOKA MBAYA.....LAKINI MARA ZOTE NIKIINGIA HEATHROW NAAMRIWA KUFUNGUA BEGI NA WANAPEKUA HASWA,HAWAWEZI KUTEGEMEA SCANNER KUGUNDUA COCAINE AMBAYO HADI LEO CUSTOMS WANATEGEMEA SIXTH SENSE KUKAMATA WATU...VILE VILE TUNABEBA CHAKULA AMBACHO WAO WAMEPIGA MARUFUKU..KWAHIO TUSIPENDE KULALAMIKA LAZIMA UKAGULIWE DUNIA NZIMA,JUST BE COOPERATIVE AND PATIENT

    ReplyDelete
  16. MAMA NAZANI UJAWAHI KUSAFILI ZAIDI YA UNAPISHI ULAYA KWENDA TANZANIA,KWA KIFUPI SEHEMU YOYOTE DUNIANI KAMA WAKIAMUA KUFUNGUA BEGI LAKO NA KUANGALIA NDANI INAWEZA KUTOKEA NA SIYO DAR TU HATA ULAYA AU MAREKANI,NAZANI OJA YAKO UJAWI TU KUPEKULIWA,TUNAPEKULIWA KILA SIKU VIWANJA VYA ULAYA NA HASA UKIWA MTU MWEUSI NDIYO KABISA....UNASHANGAA KUPEKULIWA DAR?????
    MDAU MONEY UK.

    ReplyDelete
  17. Marekani walininyanganya magimbi yangu. Kisa eti hawaruhusu vyakula kutoka kwetu

    ReplyDelete
  18. alal!! kupekura ni nini??? KUPEKUA full stop

    ReplyDelete
  19. Bwana misupu mimi naungana na mdau mmoja hapo juu. Watanzania tusiwe wepesi wa kulalamika tu bila kujua wanaopekua mizigo hiyo wanapekuwa kwa makusudi gani. Upekuzi wa mizigo haupo tanzania tu. Nilitua schipol pale amsterdam tarehe 29/8/2009. baada tu ya kuchukua mizigo kwenye lango la kutoka nje kuna maofisa pale walikuwa wanafungua mizigo ya watu na kuipekua huku wakiwa wamevaa gloves na hiyo ni ulaya hiyo siyo tanzania sasa nini wabongo kuwa walalamishi tu muda wote. Ifike mahali kabla ya kuanza tu kupiga makelele zifanyie kazi hizo pumba zako kabla ya kuzimwaga

    ReplyDelete
  20. JAMANI TANGAZO KUANZIA SASA ATAKAE ONA KITU CHOCHOTE KINAMSUMBUA,AU KUKERWA TUNAOMBA AMPIGE PICHA AU VIDEO BILA WOGA NA TUI POST KWENYE BLOG PIA PANAPO HUSIKA.WANAPOANZA KUPEKUA WEWE KAA PEMBENI MPIGE PICHA TUITOE KWA MICHUZI NA KUNAKO HUSIKA UKIWA NA USHAHIDI WA KUTOSHA,CAMERA WEKA ON UKISHUKA KWA KUJIANDAA KWA LOLOTE LA GAFLA.HII ITAKOMESHA UONGO NA UBISHI.MTAONGEA SANA LAKINI UKIWA NA USHAIDI TOSHA.

    ReplyDelete
  21. si kila nchi wanapekua, utaratibu wa nchi nyingi nilizoenda huwa hairuhusiwi kufunga begi kwa kufuli mzigo ukifika wenyewe wanascan huko ndani na ikiwezekana wanapekua kabla ya kumfikaia abiria na si kumsimamisha abiria nje
    ndio ustaarabu na hata hao watu inabidi waufuate,
    kama huamini pangilia vitu vyako na weka alama hlf mzigo ukifika uangalie tena mpangilio wa ndani

    ReplyDelete
  22. NYIE MNAOSEMA WAPEKUZI WANATETEWA MNACHEMSHA KWANI DUNIA MZIMA UPEKUZI UPO NA KWA SABABU MAALUM KAMA ALIVYOSEMA MDAU MMOJA HAPA JUU.

    NADHANI TATIZO LETU SISI WATANZANIA MARA NYINGI HATUWAPI WAPEKUZI WA UWANJA WA J.K.NYERERE USHIRIKIANO. KWA MFANO MDAU MMOJA KASEMA ALIKUWA ANAENDE MSIBANI WAKATI JAMAA WANAKAGUA WALIKUWA WANAMUULIZA MASWALI LAKINI YEYE ALIJIBU JEURI. HII MOJA KWA MOJA WAPEKUZI WA DAR WATAONA NI DHARUA NA HAPO LAZIMA KUWE TATIZO. MBONA ULAYA AU US UKIULIZWA HII NI NINI UNAJIBU HARAKA TENA KWA ADABU JIBU HIVYO PIA KWA MTANZANIA MWENZAKO.

    USHAURI WA BURE KAMA UMEBEBA VITU HALALI BASI TOA USHIKIANO KISTARABU BADALA YA KUJIBU MASWALI KWA MKATO KITU AMBACHO KINAWAFANYA WAPEKUZI WAONE NI DHARAU.

    HAKUNA HAJA YA KULALAMIKA BILA SABABU ZA MSINGI JAMANI. JAMAA WAKO KAZINI HAWAJUI KAMA UNA HARAKA AU LA, KWANZA UKISEMA UNA HARAKA WANAKUWA NA MASHAKA ZAIDI NA MZINGO WAKO.

    ReplyDelete
  23. ukweli ni huu mwaka huu, niliplan kuwapeleka wezi kwa pilato ndio maana unaona wamebadili mfumo hapo JNIA, hiyo ni kuhakikisha hakuna mizigo inayoibiwa kwa hiyo msilalamike na pia inawasaidia kuwakumbushia kama imeibiwa wakati wa kupakuliwa.

    ReplyDelete
  24. mswahili bwana.....akikaguliwa na mzungu anaona raha akikaguliwa na mtanzania mwenzake anaona shida .......kuolewa huko.

    ReplyDelete
  25. WAKIKUSIMAMISHA WAKUPEKUE KAMA UNA UBAVU KATA VIBAO TU,

    SUBIRI NISHUKE WANIZUE NAKATA VIBAO TU ALAFU KESI MBELE KWA MBELE

    ReplyDelete
  26. Wanaotetea hili swala hawajasafiri. Wakisafiri watajua inavyouma. Panda ngege uone unavyokereka.

    ReplyDelete
  27. Tatizo la hao wanaolalamika kupekurwa ni kuwa wamezoea kupanda EMIRATES,QATAR ,KENYA AU GULF-AIR,sasa ndege za kishihiri zote ni sawa na muembe ulojaa maembe,maana ndio unaopigwa mawe,lakini ukitua na Swiss au KLM huulizwi kitu,Kupekuliwa mizigo ipo dunia nzima ila ikionekana sim hulipishwi ushuru,lakini Tanzania sim moja elfu hamsini,mkitaka msilipishwe ushuru wa vitu vidogo vidogo basi jipigilie mwenyewe hata simu 50 weka mfuko wa jeans,shati cap na pia nyengine jipigilie mdomoni kama zinaingia NA utaweza kusema,Kwani kabla ya kupekura maofisa hapo wanakuuliza je unasimu,na unatoka wapi,na sio je unakitu cha kudeclare?ulaya unaulizwa umekuja kufanya nini na utakaa wapi tena na immigration ila custom huulizwi hayo ila unaulizwa kama una cha kudeclare,Ukitaka usipekuliwe wewe sema ni mwanafunzi tena serikali ndio imekupeleka,na unatoka urusi au India maana ndio wanajua ushokani na udosini hakuna deal,mi mara kibao nawambia hivyo na napita,lakini baya zaidi kama unaelekea Zanzibar ukifika tena bandarini unapekuliwa tena ijapokuwa mabegi yanaonesha tagi za ndege,mi nilisalimika Airport NIKANASA DOKSI,mwaka 2006

    ReplyDelete
  28. Mimi mwenyewe siku moja nilikuwa nahudhuria mkutano wa Kimataifa nchi moja ya Europe na nilikuwa pamoja na kundi la Waingereza tunatoka Institute moja. Tulipochukua mizigo yetu yule jamaa akaamua kunichagua peke yangu na kunipekua mizigo yangu. Wale wenzangu walijisikia vibaya na wakaamua kunisubiri. Baadae yule Officer alipoona wale wananisubiri ndio akaamua kuacha. Kwa hivo hiyo ya kupekuliwa bila dharura wala nidhamu inatokea kwa wingi huko Ulaya na Amerika.

    ReplyDelete
  29. Yaani kwa kweli unachekesha unasema ulaya hawafungui mizigo?

    wanafungua sana kama mtu anawasi or wanajaribu chance ya kudaka mtu.

    uongo wa scan ni nini?

    tena hapo dar waweke mbwa wanuse mabegi yako

    hata kama umekaa ulaya miaka 14 sasa ndio wakuachie upite? hiyo kitu huwa haitokei ni bahati ya mtu, na wewe kama unaingia kama unawapa wasi basi wanahaki ya kukusearch

    haku babu usalama TZ ni namba moja hata kama wanataka pesa mtu atajiju hapo

    ila usiseme eti ulaya hawafungui mabegi

    mie naona kwenye tv programs nyingi za mchi zilizoendelea

    ReplyDelete
  30. JAMANI MSISITIZO TANZANIA WANAPEKURA KWA KUPENDA KUONA VITU VYA NDANI NA KUTAKA WAGAIWE KIDOGO AU KITU CHOCHOTE NCHI ZA NJE WANA SCAN WAKIONA KITU CHA MASHAKA WANAFUNGUWA BEGI NA WAKIKUHSUKU WANAKUFUNGULKISHA BEGI NI LAZIMA KWA USALAMA WA NCHI LKN TANZANIA WANAFUNGUWA TENA NA MASUALA HAYANA MAANA LETE PASI YAKO UNATOKA WAPI UMEISHI MUDA GANI HUKO WAKATI MAMBO HAYO ANAOPASWA KUKUULIZA WATU WA UHAMIAJI MSIWATETEEEEEE HAWA NI WAPEKUZI TUUU WNAPENDA KUPOTEZA MUDA PALE WAKUULE RUSHWA

    ReplyDelete
  31. Tukitokea nchi za dunia ya tatu kuingia Marekani, Ulaya au Australia 'unaweza' kupekuliwa hata baada ya mzigo kupigwa scan.

    kwa sababu tunabeba vitu kama: Dagaa, Nguru wa kuchoma, Vichwa vya Nguruwe pori n.k ili kuwapelekea jamaa zetu 'chakula cha hamu'. Ila vitu hivyo hudaiwa kuwa vina madhara ya kiafya kwa mifugo yao huko dunia ya kwanza.

    Pia maofisa ushuru/uhamiaji wote dunia ni aina ya 'askari', cheki hata hiyo semina iliyoendeshwa na Ubalozi wa Marekani kuhusu 'money laundrying hapo DSM, washiriki wanatoka TRA,Uhamiaji, Takukuru, Polisi n.k

    Hivyo maofisa wengi ktk viwanja vya ndege duniani ni aina ya 'askari' hivyo usilogwe kumpiga picha au kukataa kupekuliwa utaishia pabaya, jamaa wapo kazi na wanatekeleza majukumu yao ya kikazi.

    Ushauri: wasafiri wa ndege punguzeni jazba, huo ni utaratibu duniani pote, Ila DSM wanapekuwa wengi kutokana na idadi ndogo ya wasafiri. Viwanja vya Ulaya, Marekani n.k abiri mamilioni hivyo huamua kuzukia abiria wachache ili kupunguza foleni na msongamano ktk eapoti zao za dunia ya kwanza.

    Mdau
    Msafiri Kafiri

    ReplyDelete
  32. sasa mheshimiwa hicho ndo kiswahili au kwa sababu uko ulaya. Jifunze lugha alafu uleta malalamiko yako tukuelewe. HICHI, CHILE ni vipi?

    ReplyDelete
  33. kazi kwelikweli.hivyo ukitoka ulaya usikaghuliwe!!waswahili wakikaghuliwa nchi zilizoendelea hawalalamiki,lakini wakikaghulikiwa bongo lawama kibao,hivi udhaibu wa fikra juu wa weupe utawaisha lini waswahili?

    ReplyDelete
  34. WATU HAP[A WANASEMA ETI HATA NCHI ZA ULAYA NA AMERICA HUPEKULIWA HIYO SI KWELI KINACHOFANYIKA NCHI ZA ULAYA NA AMRICA KUNA SCANNER INAYOFANYA KAZI KAMA XRAY HATA KAMA UMEFICHA KITU NDANI YA RADIO AU COMPUTER WATAKIONA NA NA KAMA WANAHISI NI KITU KISICHO CHA KAWAIDA KWANZA KABLA HUJAITWA KIFUNGULIWE HUWA MBWA MKAGUZI HUITWA NA KUNUSA KAMA NI MADAWA YA KULEWA BASI UTAITWA MZIGO UFUNGULIWE MBELE YAKO NA MASWALI YATAANZA, HUWEZI KUCHUKUWA LAPTOP NDANI YA BAG WAKAKUITA KUFUNGUWA HIYO HAIPO, KITU KINGINE NCHI ZA ULAYA HUWA WANAKATAZA KUINGIZA VYAKULA VYA NCHI ZINGINE BILA KIBALI WAKIHISI UMECHUKUWA DAGAA WA KIGOMA WATAKUFUNGULISHA NA KUWATUPA HAWATAKI WADUDU KUINGIA NDANI YA NCHI YAO, HAKUNA KITU CHA KUFUNGULISHA MIZIGO YA WATU BILA SABABU YA MSINGI NIMETEMBEA ULAYA NA AMERICA KWA MUDA WA MIAKA 20 SASA WALA SIJAFUNGULISHWA MSIGO WANGU HATA SSAFARI MOJA, KINACHOFANYIKA AIRPORT TANZANIA NI UPNEZI, RUSHWA NA NJAA, HUWEZI KUMTOZA MTU USHURU AMEBEBA LAPTOP AMBAYO AMENUNUWA ZAIDI YA MWAKA AKISOMEA KAMA KITENDEA KAZI KINGINE CHA MASO AU KAMERA, NI UONEZI NA SHERIA ZIKO WAZI HUWEZI KTOZWA TAX KWENYE LAPTO ULIYONUNUWA ZAIDI YA MWAKA NA UNAKUJA NAYO KAMA PERSONAL EFFECTS.

    ReplyDelete
  35. Sababu kubwa za kupekuliwa uwanja wa ndege:

    1. Madawa ya kulevya.
    2. Fedha haramu (money laundering).
    3. Ukwepaji ushuru

    Nchi za kitajiri hupekuliwi zaidi kwa kuwa kuna wasafiri wengi zaidi. Wakipekua kila mtu basi itachukua miaka kupita katika uwanja wa ndege zao. Wasafiri wao sio wafanyabiashara wanaoleta vitu kwa mabegi ila wanatumia Cargo.

    Nchi masikini kama Tanzania, wasafiri wengi ni wafanyabiashara na wanabeba mizigo mingi bila ya kutaka kulipa ushuru. Ukienda Dubai, utaona jinsi wasafiri wanavyobeba mizigo. Wana jamaa zao na wanaweza kupitisha hata kilo 200 bila ya kulipa ushuru wa uzito wa begi zao. Wengine wanakwenda katika nafasi za First Class kuweka mizigo yao kwa kuw amanma nafasi economy class. Maafisa wa Bongo kama hawatapekuwa basi Serikali itapoteza fedha nyingi.

    Kama wadau wanavyosema, upekuzi uko duniani kote. Ndege za KLM maya nyingi hukaguliwa zaidi kwa kuwa wasafiri wanaokwenda huko wananunua bangi kihalali madukani na kutaka kuleta ulaya. Pia, wafanyabiashara wengi wanakaguliwa kwa kuwa wanaingiza pesa cash, fedha ambazo pengine hawajazilipia kodi kwa kuwa wamezipata kwa njia haramu. Kila mtu anataka kusafiri bila ya shida, lakini umasikini wetu unatufanya tupekue zaidi wasafiri.

    ReplyDelete
  36. nimecheka sana leo hahaaa kwi kwi

    eti KLM wananunua bangi kihalali,mtu mweusi ndo unakua picked ukaguliwe mweee,tushayazoea wengine mbona haya???

    asante

    ReplyDelete
  37. Mimi juzi hapa nimenyang'anywa nguruka wangu na dagaa nilibeba boa nikalipishwa ushuru vinu wakanilipisha ushuru Yani dagaa mpaka uombe kibali serikalini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...