Familia ya Mshana wa Moshi,Kilimanjaro,wanasikitika kutangaza kifo cha mama yao mpenzi Bertha Stafford Mshana kilichotokea leo Novemba 12, 009 katika hospitali ya KCMC,Moshi Kilimanjaro
Sisi tulikupenda lakini mwenyezi Mungu amekupenda zaidi,ukae katika amani mpaka hapo mwenyezi Mungu atakapo tukutanisha tena. Ucheshi,upendo na ukarimu wako daima hautasahaulika.
Sisi tulikupenda lakini mwenyezi Mungu amekupenda zaidi,ukae katika amani mpaka hapo mwenyezi Mungu atakapo tukutanisha tena. Ucheshi,upendo na ukarimu wako daima hautasahaulika.
Familia yote,sisi wanao,Frank,Lilian,Godfrey,Langford,Edington,Magreth,Elias na Ebenezer,Wajukuu,ndugu,jamaa na marafiki,tunakuombea mapunziko mema mwenyezi Mungu aiweke mahala pema peponi roho ya marehemu kipenzi,mama yetu,ni yeye alitoa na yeye ametwaa,jina lake lihimidiwe.
Mipango ya mazishi inaendelea kufanywa na ndugu waliopo Dar es Salaam,Iringa,Moshi,Arusha,Maryland na Rhode Island (USA)
Mipango ya mazishi inaendelea kufanywa na ndugu waliopo Dar es Salaam,Iringa,Moshi,Arusha,Maryland na Rhode Island (USA)
Wafiwa poleni sana.Stafford na Lecturer Ebenezer Mshana(UDSM-Faculty of Law)pole sana.
ReplyDeleteSchool mate wenu.
Ilboru(Arusha) 1994.
Mungu amempenda zaidi, apumzike kwa amani.
ReplyDeleteRIP
ReplyDeleteMungu alimpenda zaidi, apumzike kwa amani. Ebenezer, Judy, Sandra, Ethan na wafiwa wote poleni sana na Mungu awape nguvu kwenye kipindi hiki kigumu
ReplyDeletepole ndugu Elias Mshana pamoja na wafiwa wote, kazi ya Mungu haina makosa, kuwa wenye subira katika kipindi hichi cha msiba mzito wa mama mpendwa.
ReplyDeleteSaleh washington DC
Ni mapenzi ya mwenyezi,kwa huzuni kubwa nawapa pole familia nzima ya mshana pamoja na ndugu,jamaa na marafiki.Mungu watie nguvu katika kipindi hiki kigumu.
ReplyDeleteTunashukuru sana wote wanaotujulia hali kupitia Michuzi blog,Facebook,Michuzi Jr blog,Dj Luke messages etc.Saleh wa DC,Massawe wa Dallas,Ilboru 1994,Bongo Gal,Annon(s) 01:17pm & 03:50,Ney Nyiti,Ghania Mtengeti,Joan Mwakatobe,Sarah Nayeja,Pamela Saleh etc.
ReplyDeleteDidi Vava (Massawe wa DC).