Marehemu Bertha Stafford Mshana

Familia ya Mshana wa Moshi,Kilimanjaro,wanasikitika kutangaza kifo cha mama yao mpenzi Bertha Stafford Mshana kilichotokea leo Novemba 12, 009 katika hospitali ya KCMC,Moshi Kilimanjaro

Sisi tulikupenda lakini mwenyezi Mungu amekupenda zaidi,ukae katika amani mpaka hapo mwenyezi Mungu atakapo tukutanisha tena. Ucheshi,upendo na ukarimu wako daima hautasahaulika.
Familia yote,sisi wanao,Frank,Lilian,Godfrey,Langford,Edington,Magreth,Elias na Ebenezer,Wajukuu,ndugu,jamaa na marafiki,tunakuombea mapunziko mema mwenyezi Mungu aiweke mahala pema peponi roho ya marehemu kipenzi,mama yetu,ni yeye alitoa na yeye ametwaa,jina lake lihimidiwe.

Mipango ya mazishi inaendelea kufanywa na ndugu waliopo Dar es Salaam,Iringa,Moshi,Arusha,Maryland na Rhode Island (USA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Wafiwa poleni sana.Stafford na Lecturer Ebenezer Mshana(UDSM-Faculty of Law)pole sana.
    School mate wenu.
    Ilboru(Arusha) 1994.

    ReplyDelete
  2. Mungu amempenda zaidi, apumzike kwa amani.

    ReplyDelete
  3. Mungu alimpenda zaidi, apumzike kwa amani. Ebenezer, Judy, Sandra, Ethan na wafiwa wote poleni sana na Mungu awape nguvu kwenye kipindi hiki kigumu

    ReplyDelete
  4. pole ndugu Elias Mshana pamoja na wafiwa wote, kazi ya Mungu haina makosa, kuwa wenye subira katika kipindi hichi cha msiba mzito wa mama mpendwa.
    Saleh washington DC

    ReplyDelete
  5. Henry R.Massawe,Dallas,TxNovember 13, 2009

    Ni mapenzi ya mwenyezi,kwa huzuni kubwa nawapa pole familia nzima ya mshana pamoja na ndugu,jamaa na marafiki.Mungu watie nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  6. Tunashukuru sana wote wanaotujulia hali kupitia Michuzi blog,Facebook,Michuzi Jr blog,Dj Luke messages etc.Saleh wa DC,Massawe wa Dallas,Ilboru 1994,Bongo Gal,Annon(s) 01:17pm & 03:50,Ney Nyiti,Ghania Mtengeti,Joan Mwakatobe,Sarah Nayeja,Pamela Saleh etc.
    Didi Vava (Massawe wa DC).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...