Msanii na Mwanamitindo wa kimataifa Naomi Campbell akiwa jukwaani wakati wa onyesho la mavazi lililoandaliwa na Taasisi ya Utepe Mweupe kwa lengo la kusaidia mpango wa uzazi salama kwa wanawake wajawazito lililofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick usiku wa kuamkia leo.Nyuma yake ni Bi. Rose Mlay Mratibu wa Utepe Mweupe Tanzania
Naomi Campbell akiongea na waandishi wa habari mara baada ya onyesho

Mama Salma Kikwete akiwa jukwaani na Balozi wa kimataifa wa Utepe na msanii na mwanamitindo baada ya kuzindua onesho hilo la mavazi. Shoto ni mbunifu Mustafa Hassanali ambaye alimvika Naomi na mamodo wengine
Mke wa Rais mama Salma Kikwete akiongea na Msanii na supa modo wa kimataifa Naomi Campbell wakati wa onesho la mavazi lililoandaliwa na Taasisi ya Utepe Mweupe kwa lengo la kusaidia mpango wa uzazi salama kwa wanawake wajawazito lililofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
Mama Salma Kikwete akiwa na Mke wa rais wa Zambia Thandiwe Banda wakifuatilia onesho hilo. Picha na Aron Msigwa habari na Anna Nkinda-MAELEZO.


SHOO YA NAOMI CAMPBELL YAINGIZA DOLA 10,000


Jumla ya dola za kimarekani 10,000/= zimepatikana kutokana na mnada wa nguo ya kike iliyotolewa na msanii na mwanamitindo wa Kimataifa Naomi Campbell katika maonesho ya mavazi ya Relief Tanzania yaliyofanyika jana usiku katika ukumbi wa Movenpick jijjini Dar es Salaam.


Maonesho hayo yaliandaliwa na Naomi Campbell ambaye ni Balozi wa Kimataifa wa Utepe Mweupe kwa kushirikiana na Mustafa Hassanali ambaye ni mbunifu wa mitindo wa hapa nchini kwa lengo la kukusanya fedha ili kutunisha mfuko wa Mtandao wa Utepe Mweupe (The White Ribbon Alliance).


Akiongea mara baada ya maonesho hayo Campbell alisema lengo la kufanya maonyesho hayo ni kupata fedha ambazo zitatumika katika kampeni ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.


Kuhusu wabunifu wa mavazi na wanamitindo wa hapa Tanzania alisema anaridhishwa na kazi zao na wanajitahidi kufanya kazi nzuri kwa ufasaha mkubwa na kwa kujituma.


Aliendelea kusema kuwa anaipenda nchi ya Tanzania kwa sasabu inavivutio vingi kama vile mbuga za wanyama, visiwa vya Zanzibar, mito, milima, maziwa na Bahari ya Hindi huku akisisitiza kuwa si mara ya kwanza kuja Tanzania na ana wa kuendelelea kuja hapa nchini.


Katika maonyesho hayo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) pamoja na Mke wa Rais wa Zambia Mama Thandiwe Banda walihudhuria.


Mtandao wa Utepe Mweupe (White Ribbon Alliance) wenye takribani nchi wanachama 143 duniani ambao jana uliadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake unafanya kazi kubwa yakuhakikisha kuwa nchi wanachama zinaondokana na vifo vya kina mama wajawazito wakati wa kujifungua.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. hapa..mama yetu atakuwa aliongea kwa luga ipi?

    ReplyDelete
  2. mke wa raisi wa Zambia bado anadai.....

    ReplyDelete
  3. Haya sasa - wako wapi wale wooote waliokuwa wanadai kwamba Anko Mithupu alikuwa anatudanganya kuhusu ujio wa Naomi Campbell huku Bongo???

    Mbona mmekaa kimya sasa?

    ReplyDelete
  4. Mbona pesa kiduchu??

    ReplyDelete
  5. sasa hapo hina ya nini?

    ReplyDelete
  6. wee anon wa kwanza kwani umeambiwa mama maimuna???????ebo!

    ReplyDelete
  7. kaka Mithupu nakuaminia babake! mdau uliyesema uligoogle Naomi yupo Paris umeona? Nimeamini wabongo kwa ubishi! hata km kitu hatukijui sisi ni ubishi tu! Leo kimyaaaaaa!

    ReplyDelete
  8. NAOMBA BW.MICHUZI TUNAOMBA UTUELEZE MAMA YETU WA KWANZA ANAONGEA LUGHA GANI...NINA SABABU YA KUJUA SI KWA MAANA MBAYA.NILIWAHI KUONA PICHA YAKE HAPA COLUMBIA UNIVERSITY AKIHUTUBIA ILA SIKUBAHATIKA KUPATA SPEECH YAKE.NASHUKURU SANA

    ReplyDelete
  9. Wee anony hapo juu mama wa nani lugha siku hizi inapanda mpaka ya kimataifa anasoza french kama mke wa sarkozi kaa mbali nae kabisa!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. simple english...every exposed person speak

    kwani umesikia ni mtihani wa cambridge wee annon #1

    ReplyDelete
  11. wanaouliza HINa...hawajui mwanamke urembooooooooooooooooooooooooooo!

    ReplyDelete
  12. naomba mungu asiwe alita speech kwa lugha ya kikristu uwiiiii

    ReplyDelete
  13. Kingereza kingereza.. acha ufinyu wa akili, kama una lingine sema. hilo sio muhimu.

    ReplyDelete
  14. ...kisichonipendeza ni pale mtu aso maadili - ama mla unga aliyekubuhu na kushindikana, mhalifu au mwenye uelewa mdogo anapotukuzwa na dunia na kufanywa role model. Wapo wengine wengi - kina Pete, senti hamsini na marehemu Jade. Pengine baada ya miaka mingi vizazi vyetu vitakuwa vinashangaa kama wengine wanavyoshangaa leo ilikuwaje Malkia Katarina Mkuu - na tabia zake zote - akatawala himaya kuu ya Kirusi miaka hiyo.

    ReplyDelete
  15. we al musoma una mambo ya kikoloni sana hii kitupeleka kwenye ukoo wenu itawasaidia

    ReplyDelete
  16. MIMI NIMEFUNDISHWA NA SALMA VITU VIFUATAVYO NA KWA UKWELI NILIKUWA SIVIFAHAMU KABISA.
    1.EGG=YAI EGGS=MAYAI
    2.BANANA=NDIZI BANANAS=NDIZI NYINGI
    2.MANGO=EMBE NAKADHALIKA.

    SASA UNAPOSEMA KATUMIA LUGHA GANI HUJUI KWAMBA NAOMI HUWAGA ANASIKIA KIINGILISHI OFUWICHI MAMA SALMA NAMUAMINIA

    ReplyDelete
  17. wewe hapo 16, mmmh , nakuunga mkono na miguu yote miwili, me huyo amama alinifundisha kawe primary tena alikuwa mwl pekee bingwa wa english shule nzima

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...