
SHOO YA NAOMI CAMPBELL YAINGIZA DOLA 10,000
Jumla ya dola za kimarekani 10,000/= zimepatikana kutokana na mnada wa nguo ya kike iliyotolewa na msanii na mwanamitindo wa Kimataifa Naomi Campbell katika maonesho ya mavazi ya Relief Tanzania yaliyofanyika jana usiku katika ukumbi wa Movenpick jijjini Dar es Salaam.
Maonesho hayo yaliandaliwa na Naomi Campbell ambaye ni Balozi wa Kimataifa wa Utepe Mweupe kwa kushirikiana na Mustafa Hassanali ambaye ni mbunifu wa mitindo wa hapa nchini kwa lengo la kukusanya fedha ili kutunisha mfuko wa Mtandao wa Utepe Mweupe (The White Ribbon Alliance).
Akiongea mara baada ya maonesho hayo Campbell alisema lengo la kufanya maonyesho hayo ni kupata fedha ambazo zitatumika katika kampeni ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.
Kuhusu wabunifu wa mavazi na wanamitindo wa hapa Tanzania alisema anaridhishwa na kazi zao na wanajitahidi kufanya kazi nzuri kwa ufasaha mkubwa na kwa kujituma.
Aliendelea kusema kuwa anaipenda nchi ya Tanzania kwa sasabu inavivutio vingi kama vile mbuga za wanyama, visiwa vya Zanzibar, mito, milima, maziwa na Bahari ya Hindi huku akisisitiza kuwa si mara ya kwanza kuja Tanzania na ana wa kuendelelea kuja hapa nchini.
Katika maonyesho hayo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) pamoja na Mke wa Rais wa Zambia Mama Thandiwe Banda walihudhuria.
Mtandao wa Utepe Mweupe (White Ribbon Alliance) wenye takribani nchi wanachama 143 duniani ambao jana uliadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake unafanya kazi kubwa yakuhakikisha kuwa nchi wanachama zinaondokana na vifo vya kina mama wajawazito wakati wa kujifungua.
hapa..mama yetu atakuwa aliongea kwa luga ipi?
ReplyDeletemke wa raisi wa Zambia bado anadai.....
ReplyDeleteHaya sasa - wako wapi wale wooote waliokuwa wanadai kwamba Anko Mithupu alikuwa anatudanganya kuhusu ujio wa Naomi Campbell huku Bongo???
ReplyDeleteMbona mmekaa kimya sasa?
Mbona pesa kiduchu??
ReplyDeletesasa hapo hina ya nini?
ReplyDeletewee anon wa kwanza kwani umeambiwa mama maimuna???????ebo!
ReplyDeletekaka Mithupu nakuaminia babake! mdau uliyesema uligoogle Naomi yupo Paris umeona? Nimeamini wabongo kwa ubishi! hata km kitu hatukijui sisi ni ubishi tu! Leo kimyaaaaaa!
ReplyDeleteNAOMBA BW.MICHUZI TUNAOMBA UTUELEZE MAMA YETU WA KWANZA ANAONGEA LUGHA GANI...NINA SABABU YA KUJUA SI KWA MAANA MBAYA.NILIWAHI KUONA PICHA YAKE HAPA COLUMBIA UNIVERSITY AKIHUTUBIA ILA SIKUBAHATIKA KUPATA SPEECH YAKE.NASHUKURU SANA
ReplyDeleteWee anony hapo juu mama wa nani lugha siku hizi inapanda mpaka ya kimataifa anasoza french kama mke wa sarkozi kaa mbali nae kabisa!!!!!!!
ReplyDeletesimple english...every exposed person speak
ReplyDeletekwani umesikia ni mtihani wa cambridge wee annon #1
wanaouliza HINa...hawajui mwanamke urembooooooooooooooooooooooooooo!
ReplyDeletenaomba mungu asiwe alita speech kwa lugha ya kikristu uwiiiii
ReplyDeleteKingereza kingereza.. acha ufinyu wa akili, kama una lingine sema. hilo sio muhimu.
ReplyDelete...kisichonipendeza ni pale mtu aso maadili - ama mla unga aliyekubuhu na kushindikana, mhalifu au mwenye uelewa mdogo anapotukuzwa na dunia na kufanywa role model. Wapo wengine wengi - kina Pete, senti hamsini na marehemu Jade. Pengine baada ya miaka mingi vizazi vyetu vitakuwa vinashangaa kama wengine wanavyoshangaa leo ilikuwaje Malkia Katarina Mkuu - na tabia zake zote - akatawala himaya kuu ya Kirusi miaka hiyo.
ReplyDeletewe al musoma una mambo ya kikoloni sana hii kitupeleka kwenye ukoo wenu itawasaidia
ReplyDeleteMIMI NIMEFUNDISHWA NA SALMA VITU VIFUATAVYO NA KWA UKWELI NILIKUWA SIVIFAHAMU KABISA.
ReplyDelete1.EGG=YAI EGGS=MAYAI
2.BANANA=NDIZI BANANAS=NDIZI NYINGI
2.MANGO=EMBE NAKADHALIKA.
SASA UNAPOSEMA KATUMIA LUGHA GANI HUJUI KWAMBA NAOMI HUWAGA ANASIKIA KIINGILISHI OFUWICHI MAMA SALMA NAMUAMINIA
wewe hapo 16, mmmh , nakuunga mkono na miguu yote miwili, me huyo amama alinifundisha kawe primary tena alikuwa mwl pekee bingwa wa english shule nzima
ReplyDelete