Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Japani (Tanzanite society) unapenda kuwaarifu kuwa, kutakuwa na mkutano mkuu wa mwisho wa mwaka wa Wanajumuiya wote utakaofanyika:
Tarehe: 6/12/2009
Mahali(Ukumbi) : odasaga plaza (Odakyu sagamihara station)
Muda: Kuanzia saa 12:15 jioni
Agenda za mkutano huu ni kama zifuatazo:
(1)Kupata taarifa mbalimbali za maendeleo ya Jumuiya. (i.e Kuisajili Jumuiya kuwa NGO)
(2)Kujadili na kutathmini zoezi la ulipaji ada za kila mwezi.
(3)Kujadili na kuamua kuhusu kutenga fedha kwa ajili kusaidia wenye shida nyumbani Tanzania. (4)Mengineyo.
Uongozi unapenda kuchukuwa fursa hii kuwakumbusha wanajumiya kuwa, kama tulivyokubaliana katika mkutano uliopita, kwa wale wote watakaochelewa kufika kwenye mkutano au wasiofika bila kutoa taarifa rasmi kwa uongozi watatozwa faini.
Mkutano utaanza rasmi saa 12:15 jioni, tunaomba kuzingatia muda.
Taarifa za kutoweza kufika kwenye mkutano zipelekwe kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya Bw Julluis Mwombwki :
Simu: 09041304754
Email ya simu:jullius57@ docomo.ne.jp
Email:jlmwombekijnr@gmail.com
(NB) Ili kudhibiti nidhamu kwenye mkutano huu, wale wote wasio wanachama(Wanajumui ya)
hawataruhusiwa kuingia kwenye chumba cha mkutano.
Ahsanteni
Uongozi,
Jumuiya ya Watanzania
Wanaoishi Japani( Tanzanite Society)
kifo cha jumuiya tenu kipo karibu, kama mutaiendesha kibabe kama hivyo, waulize wana washington DC, kazi kwenu kila kheri
ReplyDeleteebu nisaidie hapo anony wa kwanza, ubabe uko wapi? inawezekana sikuilewa meseji. Hao wa DC walifanya ubabe gani? fafanua bana acha lolongo
ReplyDeletewewe mwenekiti umekuja kuleta makundi tu huna lolote hayo mafnikio ya kukusanya pesa wala si wewe hiyo ni kazi ya uwataja 2008 wewe endeleza majungu ona mawanyiko wa watanzania sasa yote ni wewe na uongozi wako kutokueleweka na sasa unataka kupeana kula na watu wako kwa fedha zetu etu muanzishe restaurant ili watu wauane sio?watu hawana ajira leo wanataka kuishi kwa pesa za umoja khaa simba tutazaa na nyie sio siri tumekuvumilia mno sasa basi
ReplyDeletetete! toeni majina kabisa basi,si wakati wa uwazi na ukweli..taja jina kabisaa,kuweka wazi unaogopa nini sasa..huku mnakoita Japan mnaonekana ni waongo tu!!
ReplyDeletemdau ukerewe,Rufiji
la kwako liko wapi unaonekana we ndo mungo namba moja kigwagula mkubwa we li
ReplyDeletekweli kabisa anonymous no4 ila naweewe lako liko wapi?toa mfano au ndio walewale?unajifanya haupo jp ?pole sana
ReplyDelete