Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya ( kushoto) akipitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Fatma Mwassa, eneo la msitu wa hifadhi wa asili ulipo katika kijiji cha Mahalaka, Kata ya Doma , Wilaya ya Mvomero kuona uharibifu mkubwa wa uvunaji wa magogo kwa ajili ya mbao na uchomaji wa mkaa kinyume na sheria. Mh. Machibya ameamuru hali hii ithibitiwe haraka na wahalifu wachukuliwe hatua mara moja
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya akiwa katika hali ya kusikitishwa baada ya kujionea uharibifu mkubwa wa uvunaji wa miti toka kwa watu wasiofahamika kwa ajili ya kupata magogo ya mbao na uchomaji wa mkaa ndani ya eneo la msitu wa hifadhi ya asili uliopo katika kijiji cha Mahalaka, Kata ya Doma , Wilaya ya Mvomero na kinyume na sheria.(

sehemu wahalifu hao wanapookea mkaa
Baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mkoa na Wilaya ya Mvomero, wakipia katika moja ya eneo unapochomwa mkaa katika eneo la msitu wa hifadhi wa asili ulipo katika kijiji cha Mahalaka, Kata ya Doma, Wilayani humo na kujionea uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanyw watu waliofahamika kutoka ndani ya Wilaya, Mkoa na nje ya Mkoa. Picha na mdau John Nditi.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. yote hiyo ni khali ngumu ya maisha,kwa ufupi maisha yamekua magumu sana acha wakimbilie kwenye raslimali zilizopo wafaidike pia.

    ReplyDelete
  2. Kwa nini huyo mkuu wa mkoa amesimama juu ya magogo?

    ReplyDelete
  3. umeme hakuna na pesa zikitolewa wanakula na hata uliopo ni bei mbaya sana,gas ipo lakini serikali haifanyi chochote wananchi nao wa chini wafaidike,dawa ni kukimbilia kwenye mikaa tuu na kuni,sasa hapo mnajidai mnashangaa na kuwaita wahalifu,mnataka wapikie nini na kipato watoe wapi?

    ReplyDelete
  4. Huyo Mkuu wa Mkoa hatumii Mkaa? Kupikia Kande na kuchoma nyama? Hebu acheni unafiki. Wapeni wananchi alternative means kabla hamjaanza kusema ni uharibifu wa mazingira. Kuna waharibifu wa mazingira kama hao mawaziri wanaochoma gallons and gallons za mafuta kwa hayo mashangingi? Hebu tupisheni...

    ReplyDelete
  5. Huu ni upuuzi mtupu.
    Wananchi hawana alternative souce of energy (nishati mbadala) halafu wewe unasema tunahifadhi huu msitu mtu asikate mti wala kuchoma mkaa.
    Mimi naona wewe unayetoa amri hiyo ndo mwenye matatizo ya akili.

    Hii ni sawa na kuwa na sahani moja tu ya chakula wakati nikiwa na njaa halafu unaniambia niiweke nitaila wiki ijayo.

    Unamuhifadhia nani?
    Kesho watakuja wageni utawauzia hilo eneo wakate hiyo miti, wananchi wako umewafunga njela.

    Umeme, gesi, jua na vyanzo vingine vya nishati mmekwisha vi-Richmond halafu mnashangaa watu kukata miti. Mnaakili kweli ninyi binadamu?
    Kwani ninyi wenzetu ni wananchi wa nchi gani? Ni Tanzania hii hii tunayoijua sisi? Kwa nini mtufanyie hivi? Umeme mmeuharibu na hata hamkutuletea, gesi mmeharibu na mmejipelekea wenyewe, mtera na kidatu ndo usiseme. Halafu mnaishi kwa kodi zetu tena mkizivuruga mnavyotaka. Mmetunyang'anya kila kitu kilichokuwa chetu. Miti mtukataze tusikate, mnataka tushije? Tule chakula kibichi? Nyama mbichi? wakati hiyo nyama hata hamikagui, si mnataka kutuua kwa magonjwa.
    Tukifa, mkitumaliza mtanyonya nani jamani?
    Hebu kaeni chini mfikiri.

    ReplyDelete
  6. Ninyi serikali ndo mnaotuharibia mazingira na mirichmond yenu. Ufisadi tu mmejaa, pesa ambayo mngelitumia kutupatia nishati mbadala mmenunulia mashangingi na kufanyia umalaya.
    Hamjali tunakula nini? Tunalala wapi, tunaishije. Tunahitaji mkaa na kuni tuweze kupata nishati, hamtaki.

    ReplyDelete
  7. upuzi wa hali ya juu kabisa yani watu wakamatwa kwa jambo hili ,mbona hamuwakamati wauza unga wakubwa wakubwa nao wanajulikana na vigongo wa serikalini,mka muuwa bure amina chipuka/chifuka...kwa sababu ya kujua siri zenu...
    watu wanatafuta riski zao kwa jasho lao nnawakamata,hamuoni hata haya wala aibu,mtumjibu nini mungu wenu kesho mkiwa ndani ya kaburi nafikiri mtaishi milele kuwanyanyasa daima walala hoi nakujishibisha vitambi vyenu kwa jasho la wavuja jasho walala hoi..

    wajanja wa mitaani wenye kula deal na nyinyi ndo wanao ishi na kutuharibia watoto na wajuku zetu..

    tanzania hii leo kuna kila aina ya vitendo vichafu na tamaa mbele..
    lakin mlala hoi mungu yuko na wewe.
    fisadi wakuwa wakuu wa serikalini..

    ReplyDelete
  8. HIYO NI HALI NGUMU YA MAISHA NI SOURCE OF INCOME AND CHEAP ENERGY, YOU CAN NOT AVOID BEFORE SOLVE THE WHOLE BIG PICTURE, CREATE EMPLOYMENT FOR THE PEOPLE, HELP THEM TO FIGHT POVERTY, OTHERWISE THEY WILL CONTINUE TO DECIMTE THE FOREST. VIONGOZI ACHANE UCHOYO SAIDIENI WANANCHI

    ReplyDelete
  9. na tutakata sana hiyo miti mnataka tupikie nini? wakati umeme wenyewe ni wa mgao?? hata nyinyi wabunge mnatumiaga sana mkaa mkitokaga huko dodoma njiani mnapakiaga migunia ya mkaa mnashindilia kwenye hayo mashangingi yenu halafu mnajida bla bla hapa na baadhi yenu kwa kutumia nyadhifa zenu mnakata magogo mnasafirisha nje ya nchi mnajinufaisha wenyewe sasa si bora tufaidi wote??? punguzeni umimi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...