taswira za jiji la dar pamoja na vikwangua anga vipya vilivyomea karibuni na vinbavyoendelea kumea. wasiwasi wa weingi ni kwamba miundo mbinu bado ni ile ile. mifereji ya maji machafu haijaongezwa wala kupanuliwa, sehemu za megesho ya gari ukiondoa chache zilizojengwa kwenda juu, hamna na magari yanaongezeka kila dakika, taa za barabarani haba na zilizopo ni za watts 30 na zinawaka kama mshumaa na kadhalika wadau nisaidieni
hapo ni maeneo ya riddoch motors penye magari ni klabu ya bilicanas



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. uchafu mtupu.

    ReplyDelete
  2. Na wewe Mi-soup bwana. Vikwangua anga wapi? Maana yake ni Sky Scrapers...shida ni kuwa hakuna hata moja bongo. Zinaitwa Sky Scrapers kwavile zinafika mawinguni kama zile World Trade Center 1&2 zilikuwa zinafika mawinguni na hata mvua ikinyesha watu walioko 110 Floor hawajui kama kulikuwa na mvua kwavile walikuwa juu ya mawingu. Sasa usiwadanganye wabongo ati gorofa 15 au 25 ni Vikwangua Anga...hatujafika huko bado...hizo ni Apartment buildings kwa wenzetu..

    ReplyDelete
  3. taswira ya jiji letu pendwa la dar ni kielelezo halisi kama sio kielelezo kuntu cha jinsi wabongo tunavyofikiri na kutenda (worldview) kuanzia mtu binafsi katika kaya yake hadi kaya kuu ya taifa (ikulu)!! ukiwashangaa wafanyayo watawala (na watawaliwa pia)na wao wanakushangaa kwa nini unashangaa!!!!!!!! sote tunaanza kutumbuliana mimacho. ndio bongo hiyo!!!

    ReplyDelete
  4. Hivi kwetu hakuna mipango miji? mji hauwezi kupendeza kama ujenzi haufati ramani za mji?

    usinibanie!!!

    ReplyDelete
  5. Kwa kweli mji unapendeza na hayo majengo mapya, lakini mimi na swali je wanaweka/zingatia sehemu za dharura kama sehemu ya kupita magari ya zima moto? na parking zipo kwa ajili ya wakazi wa hayo majengo? Nashukuru bro Michuzi

    ReplyDelete
  6. jamani nauliza...hivi kipi kinachowashinda wizara kushindwa kuweka mitaro na iweze kutumika...au na hilo tusubiri wahisani??....jamani watanzania tuwe na ule moyo wakufanya jambo taifa lifaidike..

    huwa nasema kila siku.. mungu azizuiya hivyo hivyo hizi mvua kwani hatujiwezi hata kujiinua mguu, na kwa hilo au tutaomba msaada UN tulivyokuwa akili zetu zimejaa ukungu za rushwa...

    ReplyDelete
  7. kwakweli Dar ya zamani si ya leo kwa kweli inangara na kuwika lakin wanafaidi ni wakina nani,wazawa au wazagawa(waliogawiwaa,si wazawa)sina ubaguzi na kabila au rangi ua dini ya mtu ila tuangaliye kwa undani zaidi nani anayefaidika leo hii utasikia tanzania pesa yako kila kitu kipo kama ulaya,je wazazi wetu wasiokwenda skuli hoe hae wanafaidika je mnajua madhara ya majuu pia,kila leo kunaiga mambo ya majuu na tunaona ufahari,pole pole mila na tamaduni zetu tutazisahau na ukarimu na wema wetu wa kitanzania utapotea na hatodhaminiwa mtu isipokuwa pochi...
    kumbekani kwamba dunia tunapita njia,tulivyonavyo hatutakwenda navyo kwenye uzima wa milele isipokuwa matendo yetu mema tuliyoyafanya hapa duniani

    majumba ya kifahari,magari ya kifahari,mavazi ya kifahari,masherehe yakifahari,umaskini kila kona umetuganda,kama mnajenga hayo majumba yetu kuiga majuu sehemu za mitaro mbona hazifanyi kazi mvua zinaponyesha,faida yake nini wenzenu wana plan huku majuu nyinyi kuiga ...

    simuonei wifu alicho nacho kitu isipokuwa kama ana nia njema na matendo mema...
    nimeishi sana majuu europe na marekani na japan na india lakini wenzetu wako tafauti na sisi...

    sikusudi huhubiri lakini...

    kumbukeni kwamba yesu alikuwa mtu wa kawaida sana,very simple na mtume muhammada (S.W.A)naye pia so dini gani sisi tunafuata ufahari wa kidunia...

    bro michu uwamuzi wako ukitaka kuweka comment hii ua laaa..

    ReplyDelete
  8. TATIZO KUBWA VIONGOZI WANASHINDWA KUFANYIA KAZI MAWAZO YA WATAALAM MATOKEO YAKE MAMBO LA KITAALAM YANATATULIWA NA WANASIASA SIKU WAKIAMUA JAMBO LA KITAALAM LIENDESHWE KITAALAMU BASI NAAMINI HARAKA SANA TUTASONGA KUELEKEA HUKO TUNAKOTAKIWA KUELEKEA

    ReplyDelete
  9. NAONA KAMA UCHAFU UNAONGEZEKA BONGO...HAPO HAMNA PLAN KABISA.
    MDAU MONEY UK.

    ReplyDelete
  10. mdau wa kwanza, vikwangua anga sio maendeleo,ila kuimarisha tulichonacho,mazingira,mifereji mjini ndio maendeleo, jamaa zetu wa kenya na matatizo yao yote, bado wametutangulia, hali ya hewa dar miaka ya themanini ilikuwa nzuri, leo mama ntilie na moshi zao kila mahali!!!!

    ReplyDelete
  11. Tusichuzane hapa. Bongo bado ipo nyuma, hata vyoo hamna bado, ukitaka kukojoa inabidi ukimbilie hoteli za kitalii ukajisaidie.

    Huko mtakaa wenyewe, tusichuzane.

    ReplyDelete
  12. Nyie mnaojidai mnaponda bongo na kusifia hizo nchi za wenzenu mnadhani zilijengwa kwa mwaka mmoja ? au mlitaka Dar iwe na nyumba za nyasi ? Acheni kashfa zisizo na msingi, kama hamna vyoo njoo ujenge hivyo vyoo. Hizo nchi za wenzenu kwanza mnaishi ka wakimbizi tu. Kama mna akili njooni muibadilishe nchi yenu kwa faida ya vizazi vyenu vijavyo.
    Roma haikujengwa siku moja.

    ReplyDelete
  13. hatusifii nchi za wenzetu ingawa hazikujengwa siku moja lakini hakuna ufisadi uliokithiri na wala hakuna mgao wa umeme bongo almost miaka hamsini ya uhuru maji tabu umeme ni hadithi ndefu sasa huku kwa wenzetu walichukua miaka 50 kupata maji na umeme?? mbona vi nchi vidogo huko africa vinaishinda bongo?? na hatuishi kama wakimbizi tunakula hewa safi maisha bora kwa kila mtu nguvu zako tu kila kitu utapata ni wewe tu umeme 24/7 maji safiii ya kumwaga no kuchemsha kunywa hata ukiwa cooni no colera usafiri wa bwerere hospitali juu sana sasa miundo mbinu mibovu pia tusiseme kisa ati tuko majuu?tuna akili sana na haturudi kuja kula mgao hapa ili iweje?? tulete vicent vyetu ili mafisadi wavifaidi kama vya kwao?? wakati hata mtu ukirudi kwenu kwa kijivekesheni pale eapoti wanakulamba mali yako ndo tuje tulete maendeleo ya kuja kujenga vyoo ili mkojolee masink sio eeh inauma sana na inavunja moyo tutarudi kuleta maendeleo mkiwa wastaarabu na ufisadi ukiisha kabisa vinginevyo tutabanana na wazungu humuhumu kwa raha zetu na winter hii tunavyon'gaa mtatutaka

    ReplyDelete
  14. Kunaonekana kuchafu na hakuna mpangilio wa majengo wala mitaa.
    Hamna parks hamna bustani hamana zoo hamna movie theaters za kisasa
    hamna shopping Mall kubwa hata moja!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...