Kampuni ya simu za mkoni Tigo leo imekabidhi zawadi kwa washindi wa mchezo wa promosheni ya Tigo Bingwa iliyokuwa ikichezeshwa kwa kipindi mwezi mmoja uliopita
Zawadi zilizokuwa zikishindaniwa katika mchezo huo ni pamoja na 1Plasma TV 26 Inch-LCD mshindi wa Pili ni Laptop DELL na mshindi wa tatu ni Digital camera- SONY.
Washindi waliokabidhiwa zawadi zao wote ni kutoka jijini Dar es Salaam,
akiwataja na kuwakabidhi zawadi washindi hao ni JAMAL JUMBE wa KINONDONI 1 Plasma TV 26 Inch, HASSAN MOHAMED wa MBAGALA Laptop VENACE ALEX MSHOBOZI wa MBAGALAambae aliibuka na Digital camera
Promosheni ya Tigo Bingwa Tilizindua tareh 12/10/09 na kufikia kilele chake tarehe 12/11/09. Promosheni hii ilikuwa ni kwa watanzania wote wanaotumia mtandao wa tigo Tanzania
Ili kuingia kwenye mchezo wa promosheni hiyo Mteja alitakiwa kutuma neno SWALI kwenda 15550 na kisha alianza kupokea maswali mbalimbali kutoka Tigo na alipojibu kwa usahihi alijipatia pointi zilizomfanya awe mshindi kadiri alivyokuwa na pointi nyingi
Sisi tigo tunajisikia fahari sana kuendesha promosheni hii ya kipekee kwa kuwa kila mteja wetu alipoamua kushiriki alikuwa akijiwekea lengo la kushinda zawadi anayotaka kutoka kwetu.
Bado Tigo tunaendelea kuwazawadia watanzania walioamua kutumia mtandao wetu kikamilifu kwa kupitia promosheni nyingine ya KWARUZA inayoendelea hivi sasa. hadi sasa tayari tumeshafikisha zaidi ya washindi 230 walioibuka na zawadi za milioni moja, laki tano na laki tatu
Pia ili kuendelea kuboresha huduma za mtandao wa intaneti sasa tunatoa nusu bei kuanzia muda wa saa tano usiku hadi saa mbili asubuhi. kwa kujiunga na huduma zetu za intanet mteja anatakiwa kutuma neno ALL kwenda namba 15006 na atatumiwa SETTING utakazohifadhi kwenye simu yako na utakuwa umeungwanishwa na mtandao moja kwa moja.
MHH labda iwe niko nyuma ila nijuavyo PLASMA TV size zake zinaanzia 37" na kuendelea. Naa,imi hii itakuwa LCD Tv.
ReplyDeleteKumbe sio peke yangu nilieshangazwa na hilo, nimeona kule kwenye post ya kiota cha bagamoyo LCD TV imeitwa hivyo hivyo plasma TV, nikasema labda ni plasma kweli. Sasa tena kuja hapa na kuona hako nako kameitwa plasma nikawa na wasi wasi muandishi hajui kutofautisha, anahisi kila LCD ni plasma. LCD na plasma ni mbali mbali na zinatengenezwa kwa technology tofauti.
ReplyDeleteNawasilisha.