Kushoto ni Deputy HR Manager (Afisa Rasilimali Watu) wa Tigo Bennett Kakorozya akikabidhi zawadi ya Plasma TV Inch 26 kwa mshindi wa kwanza wa promosheni ya TIGO CHEMSHA BONGO Jamal Jumbe wa KINONDONI, katikati ni Tawonga Mpore Ofisa huduma za ziada Tigo na Afisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando wakishuhudia wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo ofisi za Tigo makao makuu. kushiriki Mteja alitakiwa kutuma neno SWALI kwenda 15550 na kisha alianza kupokea maswali mbalimbali kutoka Tigo kwa mwezi mmoja uliopita.
Kulia ni Deputy HR Manager (Afisa Rasilimali Watu) wa Tigo Bennett Kakorozya akikabidhi zawadi ya Laptop kwa mshindi wa PILI wa promosheni ya TIGO CHEMSHA BONGO Hassan Mohamed wa MBAGALA, katikati ni Tawonga Mpore Ofisa huduma za ziada Tigo na Afisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando wakishuhudia wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo ofisi za Tigo makao makuu. kushiriki Mteja alitakiwa kutuma neno SWALI kwenda 15550 na kisha alianza kupokea maswali mbalimbali kutoka Tigo kwa mwezi mmoja uliopita.

Kampuni ya simu za mkoni Tigo leo imekabidhi zawadi kwa washindi wa mchezo wa promosheni ya Tigo Bingwa iliyokuwa ikichezeshwa kwa kipindi mwezi mmoja uliopita

Zawadi zilizokuwa zikishindaniwa katika mchezo huo ni pamoja na 1Plasma TV 26 Inch-LCD mshindi wa Pili ni Laptop DELL na mshindi wa tatu ni Digital camera- SONY.

Washindi waliokabidhiwa zawadi zao wote ni kutoka jijini Dar es Salaam,

akiwataja na kuwakabidhi zawadi washindi hao ni JAMAL JUMBE wa KINONDONI 1 Plasma TV 26 Inch, HASSAN MOHAMED wa MBAGALA Laptop VENACE ALEX MSHOBOZI wa MBAGALAambae aliibuka na Digital camera

Promosheni ya Tigo Bingwa Tilizindua tareh 12/10/09 na kufikia kilele chake tarehe 12/11/09. Promosheni hii ilikuwa ni kwa watanzania wote wanaotumia mtandao wa tigo Tanzania


Ili kuingia kwenye mchezo wa promosheni hiyo Mteja alitakiwa kutuma neno SWALI kwenda 15550 na kisha alianza kupokea maswali mbalimbali kutoka Tigo na alipojibu kwa usahihi alijipatia pointi zilizomfanya awe mshindi kadiri alivyokuwa na pointi nyingi

Sisi tigo tunajisikia fahari sana kuendesha promosheni hii ya kipekee kwa kuwa kila mteja wetu alipoamua kushiriki alikuwa akijiwekea lengo la kushinda zawadi anayotaka kutoka kwetu.

Bado Tigo tunaendelea kuwazawadia watanzania walioamua kutumia mtandao wetu kikamilifu kwa kupitia promosheni nyingine ya KWARUZA inayoendelea hivi sasa. hadi sasa tayari tumeshafikisha zaidi ya washindi 230 walioibuka na zawadi za milioni moja, laki tano na laki tatu

Pia ili kuendelea kuboresha huduma za mtandao wa intaneti sasa tunatoa nusu bei kuanzia muda wa saa tano usiku hadi saa mbili asubuhi. kwa kujiunga na huduma zetu za intanet mteja anatakiwa kutuma neno ALL kwenda namba 15006 na atatumiwa SETTING utakazohifadhi kwenye simu yako na utakuwa umeungwanishwa na mtandao moja kwa moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. MHH labda iwe niko nyuma ila nijuavyo PLASMA TV size zake zinaanzia 37" na kuendelea. Naa,imi hii itakuwa LCD Tv.

    ReplyDelete
  2. Kumbe sio peke yangu nilieshangazwa na hilo, nimeona kule kwenye post ya kiota cha bagamoyo LCD TV imeitwa hivyo hivyo plasma TV, nikasema labda ni plasma kweli. Sasa tena kuja hapa na kuona hako nako kameitwa plasma nikawa na wasi wasi muandishi hajui kutofautisha, anahisi kila LCD ni plasma. LCD na plasma ni mbali mbali na zinatengenezwa kwa technology tofauti.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...