Watangaji wa mpira wa miguu wanaochipukia kwa sasa hapa nchini ENOCK BWIGANE(kulia aliyevaa uzi wa TAIFA STARS)na AHMED SALUM(kushoto)wote wa shirika la utangazaji Tanzania-TBC wakiwajibika katika kutangaza mpira uwanja mpya wa kisasa wa TAIFA jijini DSM.kweli TBC ni shule inayoibua vipaji vipya na vya ukweli katika utangazaji wa mpira nchini.BIG UP TBC na mkurugenzi TIDO MHANDO. Inatia raha kuona wakifuata nyayo za kina Ahmed Kipozi, Ahmed Jongo, Charles Hilaly, Swedi Mwinyi, Nadhir Mayoka (RIP), Salim Mbonde, Mikidadi Mahmoud na wengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Nadhir Mayoka (RIP) Mwenyezi amuweke sehemu Nzuri. Naomba kuuliza Nadhir ndiye yule alifariki game yake ya Mwisho Alitangaza Yanga na Timu moja kati ya Mbeya au iringan ilikuwa mdogo sana na Umri wa miaka 7. Kama ndio huyo alikuwa kiboko Ahmed Jongo na Charles Hilal walikuwa wanapenda kuongeza Mpya sababu tunasikiliza kwenye Radio Mbao.

    ReplyDelete
  2. unawezaje kuwataja mabest bila kumtaja Domminick Chilambo?(RIP)wa kutoka ccm kirumba,,

    ReplyDelete
  3. Watangazaji wa RTD/TBC walinogesha mechi.

    Zamani enzi zile wakati wa redio moja,tulikuwa tunaanika beteri za radio ili jioni umsikie Anko fadha Ahmedi Jongo, Kipozi, Mshindo Mkeyenge, mikidadi mahmood, Salim mbonde, marehemu Nadhiri Mayoka, Charles Hirary, Dominic Chilambo, Abdul Masood, Sekioni Kitojo, Tido Mhando, Juma Ngondae na wengineo wengi ngoma ilinoga kweli kweli.

    Mpira ulikuwa na shauku kubwa zile lalalalalalala gooooooooo......hapanaa inakuwa nini pale.... watu huko walikuwa wanapiga teke redio zao, kwa sasa sina uhakika na watangazaji wa leo.

    Zamani wakati wa magazeti matatu ambapo mawili yalikuwa ya kiswahili na moja la kiingereza, alikuwepo kaka yangu James Nhende ambaye sasa yuko mwanza. (zile habari za Chama na Mogela, Selamani sanga na Willie Mwaijibe siku hizi hazipo),
    TBC kweli ni chuo kwa sababu sasa yuko Juma Nkamia, Dada Halima Mchuka, Jesse John na chipukizi hawa kiwa Bwigane. Kweli wanajitahidi

    ReplyDelete
  4. Kuna Mdau kanisaidia Nilikuwa nauliza Mtangazaji alifariki Huyu mwengine baada kuweka Jina Domminick Chilambo ndio kumbukumbu imerudi R.I.P kwa Chilambo alikuwa Mtangazaji Mwenye kuvutia utangazaji wa Mpira Vizuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...