Picha na Habari Na Woinde Shizza,
Arusha
Siku mbili baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua hotel ya kitalii ya Snowcrest iliyopo nje kidogo ya manispaa ya Arusha katika eneo la Ngulelo, ukuta wa hotel hiyo umevunjwa leo.
Tukio la kuvunjwa kwa ukuta huo limetokea saa 11.30 alfajiri chini ya usimamizi mkali wa polisi na imeelezwa kuwa sababu ya kuvunjwa kwa ukuta wa hotel hiyo ni kuwa ndani ya eneo la hifadhi ya barabara..
Akizungumza na waandishi wa habari,mkurugenzi wa Snowcrest ,Willfred Tarimo alisema kuwa amepata pigo kubwa juu ya tukio hilo na kwamba limemwathiri kwa kiasi kikubwa kibiashara kutokana na baadhi ya wateja wake zaidi ya 40 waliokuwa wamelala hapo, kuamua kutimuka kwa hofu.
Ameongea kuwa kufanyika kwa tukio hilo kuna chuki za kibiashara na kwa lengo la kumwangusha kibiashara hasa kwa kipindi hiki cha mapumziko,ukizingatia hotel hiyo ni mpya na ima miezi mitatu tangu ianze kutoa huduma.
Tarimo alikiri kupokea barua kutoka Tanroad ikimuelekeza kubomoa ukuta huo ambao inadaiwa ulikuwa ndani ya hifadhi ya eneo la barabara kwa urefu wa mita 10.
Alisema kuwa walishaarifiwa juu ya kuvunjwa kwa ukuta huo, hata hivyo ameeleza kushangazwa kwa uvunjwaji wa ukuta huo ambao umeenda sambamba na ufunguzi wa hotel hiyo uliofanywa na Rais kikwete,hatua ambayo imeelezwa kumwingiza rais katika kashfa ya udhalilishaji.
Alihoji kuwa iweje uvunjwa huo uanzie katika hotel yake ilihali, ujenzi wa barabara haujaanza rasmi huku maeneo mengi ya nyumba katika barabara hiyo yakiwa ndani ya hifadhi pasipo kubomolewa.
Aidha kwa upande wa meneja utawala wa Snowcrest ,Mark Diria alisema kuwa thamani ya uharibifu wa hotel hiyo ni mkubwa hata hivyo wanafanya tathimini ili kujua thamani kamili ya uharibifu.
Hata hivyo akiongea kwa njia ya simu meneja wa tanroads mkoani hapa Deustedit Kakoko alisema kuwa hoteli hiyo ilishaarifiwa kubomolewa kwa ukuta wake lakini uongozi umekuwa ukikaidi na kushindwa kutoa ushirikiano.
Hotel hiyo ya wazawa ilizinduliwa na Rais kikwete, Desemba 18 mwaka huu, huku uzinduzi huo ukienda sanjari na sherehe za kukata na shoka
Hotel hiyo ina vyumba (83) na watumishi (120) imegharimu jumla ya dola za Kimarekani Milioni nane ambapo sehemu kubwa ya fedha hizo ni mkopo kutoka Benki ya Biashara na Maendeleo ya PTA
Ameongea kuwa kufanyika kwa tukio hilo kuna chuki za kibiashara na kwa lengo la kumwangusha kibiashara hasa kwa kipindi hiki cha mapumziko,ukizingatia hotel hiyo ni mpya na ima miezi mitatu tangu ianze kutoa huduma.
Tarimo alikiri kupokea barua kutoka Tanroad ikimuelekeza kubomoa ukuta huo ambao inadaiwa ulikuwa ndani ya hifadhi ya eneo la barabara kwa urefu wa mita 10.
Alisema kuwa walishaarifiwa juu ya kuvunjwa kwa ukuta huo, hata hivyo ameeleza kushangazwa kwa uvunjwaji wa ukuta huo ambao umeenda sambamba na ufunguzi wa hotel hiyo uliofanywa na Rais kikwete,hatua ambayo imeelezwa kumwingiza rais katika kashfa ya udhalilishaji.
Alihoji kuwa iweje uvunjwa huo uanzie katika hotel yake ilihali, ujenzi wa barabara haujaanza rasmi huku maeneo mengi ya nyumba katika barabara hiyo yakiwa ndani ya hifadhi pasipo kubomolewa.
Aidha kwa upande wa meneja utawala wa Snowcrest ,Mark Diria alisema kuwa thamani ya uharibifu wa hotel hiyo ni mkubwa hata hivyo wanafanya tathimini ili kujua thamani kamili ya uharibifu.
Hata hivyo akiongea kwa njia ya simu meneja wa tanroads mkoani hapa Deustedit Kakoko alisema kuwa hoteli hiyo ilishaarifiwa kubomolewa kwa ukuta wake lakini uongozi umekuwa ukikaidi na kushindwa kutoa ushirikiano.
Hotel hiyo ya wazawa ilizinduliwa na Rais kikwete, Desemba 18 mwaka huu, huku uzinduzi huo ukienda sanjari na sherehe za kukata na shoka
Hotel hiyo ina vyumba (83) na watumishi (120) imegharimu jumla ya dola za Kimarekani Milioni nane ambapo sehemu kubwa ya fedha hizo ni mkopo kutoka Benki ya Biashara na Maendeleo ya PTA
Sheria msumeno hata akijanani tena wamekosea ilitakiwa ibomolewe asubuhi ile ya kuja huyo Kikwete, ni wakati sasa watanzania tujirudi na kufuata sheria. Hapo kinachoonekana ni ukaidi na mazingira ya rushwa, inaonekana kuna mtu alishachukua chake mkaamua kujenga mkijua atapiga kifua. Hiyo hotel ni kubwa nyie mkiachiwa watu wato watafanya kama nyie, mlitakiwa kuonyesha mfano kwa watu wa kawaida. Heko TANROADS. Rais ikiwezekana mpe huyu jamaa cheo hasa hapa Dar ili asafishe, wajenzi kama hawa.
ReplyDeleteHongera TANROADS kwa kusimamia sheria. Hakuna aliyejuu ya sheria. Hotel kufunguliwa na Rais haina maana kuwa inafuata sheria.
ReplyDeleteHoja ya barabara bado haijaanza kujengwa inaonyesha jinsi gani huyu mtu asivyofikiria mbali. Ina maana alijenga ukuta iliaje kubomoa wakati barabara itakapokuwa inajengwa? Sheria za ujenzi katika maeneo ya barabara ziko wazi hivyo inabidi tu zifuatwe. Hakuna cha chuki ya biashara hapa.
Kwanza anatakiwa alipelekewe invoice ya kulipia gharama za kubomoa huu ukata ili hela za walipa kodi zilizotumiwa na TANROADS zirudi.
kulikooni tena jamani c juzi juzi hotel ilifunguliwa na rais.
ReplyDeleteEven the president is not above the law. Defaulters should be dealt with accordingly. This hotel should not be where it is.
ReplyDeleteNendeni zenu nyie msilete za kuleta umeambiwa zaidi ya mara tatu kabla na baada ya kujenga huo uzio! sasa Hotel ikiwa ya Wazawa ndo ujenge barabarani? Tukitaka kwenda Hospital tupite wapi? inaonekana ulitaka kutumia siasa katika kuwaogopesha TANROADS kufanya kazi yake! Kila siku tunaskia ati Mrema hivi Mrema vile! Hivi kweli ni Mrema huyu aliyefanya kazi UK indiligency au kuna wanasiasa wanataka kazi yake! Mwacheni afanye kazi yake! Na wana siasa tafadahalini mkinyang'anywa tender zilizowashinda msifanye character assasination!
ReplyDeleteMfano mzuri wa utawala wa sheria. Washauri wa rais na wanainteligensia wake hawafanyi kazi yao kikamilifu! Rais JK ameishafanya ufunguzi rasmi wa vitega uchumi vingi (mahoteli, shule za sekondari, nk) ambavyo vina harufu ya ufisadi! Watu wake walipaswa kujua hilo mapema na kumshauri asiende hapo!!
ReplyDeleteWell done TANROADS!
ReplyDeleteBwana Tarimo nafikiri aliyejenga hiyo hoteli ni msomi na pia kabla hapo ulipewa maelezo ya kuhusu nini cha kufanya kuhusu barabara uwache eneo mita ngapi hapo sasa nini unalalamika kama ulitoa rushwa kwa aliyekuwepo wakati huo kaja mwingine cha kushangaza ni kwamba barua umeletewa na kufanya kiburi na umesema wazi kuwa ulijuwa kwamba uko ndani ya eneo la barabara kwanini ulijenga tanrod cku hizi wa sheria inasema sio lazima wajenge barabar ndio ubomoe hapana bali eneo la barabara linabaki wazi muda wote kama wewe ungeanza wengine wangefutia huo ujinga wako, kuweni wastarabu kwani rais akija hapo ndo kusiwe na makosa rais mambo ya mita za barabara sio kazi yake.
ReplyDeleteunajua kila siku nasoma commets za watu walioko nje ya tanzania zinatia simanzi,kweli nilifiki Tanzania itakombolewa kwa fikara na maendeleo kutoka kwa watanzania wa nje lakini ndio inatia aibu nyinyi mlio kwenye maendeleo mnaogea kama vile watu wa kijijini,hayo TANROAD leo ndio wameona barabara pale au hiyo sheria ya barabara ndio wameijua leo,ukisoma vizuri utaelewa hapo lazima kuna kitu kinafichwa,hata huyo mkurungezi wa Tanroads na yenye hana akili sawa sawa huwezi kwenda kuvunja ukuta saa 11,lazima kunakitu unatafuta zaidi ya kazi
ReplyDeletesawa kabisa, maana kuna maghorofa ya wakubwa yaliyopo barabarani dar, barabara ikijengwa ramani huwa zinapindishwa
ReplyDeleteInabidi hawa jamaa wenye hotel watumiwe invoices, lazima walipie gharama za vunjavunja, tanroad hawafanyi kazi za bure , sisi walipakodi ndo tunawalipa.
ReplyDeletekwahiyo gharama za uvunjaji lazima zilipwe na wenye Hotel.
Kuvunjwa ukuta ni jambo la busara kabisa haswa ukizingatia kuwa Bw. Tarimo mwenyewe anakiri kuwa alipewa taarifa hizo mara kadhaa! Ninaloomba ni kuwa hao washauri wa raisi wawajibishwe kwa kutompa ripoti kamili .. SHAME ON YOU!! You got to do something about this Mr. PRESIDENT, hawa watu wanakuchezea akili sana!
ReplyDeleteWATANZANIA TUNA HULKA MBAYA YA KUTOFUATA SHERIA.MMESHAAMBIWA HOTEL IMEVAMIA SEHEMU YA BARABARA HAMUELEWI BADO MNAENDELEA KUJENGA.MNAPIGA GHARAMA ZA NINI? WAKATI MPO BARABARANI? KWA HIYO WEWE BW. TARIMO UNATAKA BARABARA ISIPANULIWE KWA FAIDA WEWE? UNAFURAHI KUONA KUNA TRAFFIC JAM KWA SABABU YA MANUFAA YAKO! SUALA LA JK KUFUNGUA HOTEL HALIJAHALALISHA WEWE KUVUNJA SHERIA! HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA.
ReplyDeleteSAFI SANA..NA MIKOA MINGINE IFUATE MFUMO MZURI KAMA HUO.
ReplyDeleteTENA NI BORA WAANZE NA MAFISADI
maoni yangu yapo tofauti walipokuwa wanajenga hawo wanaojiita tanroad walikuwa wapi kuanzia mwanzo?? kwani walikuwa hawaoni ikijengwa??? hawo ndio watu wa mzee jk sasa wanakuaibisha mzee unafugua kwa sherehe halafu watu wako wanakuja kubomoa that means uzembe wa kazi
ReplyDeletekitu kingene ni kweli kama kuna rushwa sasa watazania tuamke tuache maneno tuwajibike
Watanzania wenzangu:
ReplyDelete1. Tan Roads walikuwa wapi tangu hotel inajengwa mpaka inakwisha? kwa nini wasibomoe wakati inajengwa pale mwanzoni kabisa??!!
2. Rais Kikwete ameifunguwa hotel then the next day mnavunja hotel?? jamani rais anapokwenda sehemu ni lazima awe na taarifa maalumu na iwe kamili, ili asije akajihusisha na vitu vya ajabu, ajabu, sasa hawa watu wa usalama pamoja na watu wa rais wetu hawakuyajuwa yotee haya??? Aibu iliyoje kwa nchi yetu na kwa rais wetu, mimi nashindwa kuelewa uzembe na aibu anayotiwa rais wetu na viongozi wengine.
Na kwanini hawa Tan Roads wasingetumia busara zaidi.
Mimi huwa nafurahia sana mambo ya Tanzania yetu, wala sitamani kuhama.Hebu fikiria unapata meneja kama wa TANROADS- Arusha anaacha usingizi wake anapanga kwenda kuvunja uzio wa hoteli saa 11.30 alfajiri. Hongera sana pamoja na watendaji waliokuwepo, Nchi inajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye Meno. Naamini wewe ni mmoja wa wale watanzania wachache waliobaki wenye moyo wa kuijenga Tanzania ila unavunjwa moyo na wale walio wengi wanaojipenda wenyewe.
ReplyDeleteSWALI LANGU KUU AMBALO NINA MASHAKA NA HUYU JAMAA(MENEJA) NI KUWA, HIVI ALITOA NOTICE UKUTA UKIWA KABLA,UANZA KUJENGWA AU NI BAADA YA KUJENGA, JE NI KWANINI HAKUSIMAMISHA UJENZI MARA MOJA MPAKA MTU ANAFIKIA KUFUNGUA HOTELI TENA NA KUMWALIKA MKUU WA NCHI, JE HAKUNA SABABU BINAFSI AU CHUKI YA KIBIASHARA AU KUKOMOANA? JE NI NANI ATALIPA HIZO GHARAMA ZA UBOMOAJI? KWANINI WATENDAJI WA SERIKALI TUMEKUWA WAZEMBE KIASI HIKI? KWANINI HATUFIKIRII? UKUTA ULE SIO UYOGA KUWA JAMAA ULIAMKA ASUBUHI UKAKUTA UMEOTA, KWA HARAKA HARAKA UKIFIKIRIA UMECHUKUA ZAIDI YA WIKI MBILI KUJENGWA ACHA KUOTESHA MAJANI NA KUPAVE HILO ENEO.
ANGALIZO:SIMTETEI MWENYE HOTELI KWANI HAKUNA ALIYEKO JUU YA SHERIA UKIVUNJA SHERIA LAZIMA UADHIBIWE, HIVYO MWENYE HOTELI ANASTAHILI ADHABU.
LAKINI HAWA WATENDAJI WANAOSUBIRI NYUMBA ZINAJENGWA HALAFU WANAKUJA KUVUNJA, HUWA WANAKUWA WAPI? NA KWANINI UBOMOAJI HUWA UNAWAKUTA WATU FULANI TU LAKINI WENGINE BARABARA HUWA ZINAWAKWEPA? TANROADS HAO HAO WAMEKUWA WANAWEKA MIPAKA YA BARABARA KWA KUKWEPA NYUMBA ZA WAKUBWA, MFANO HAPA DAR, BARABARA MPYA ILIYOJENGWA KUTOKA KAWE MARINGO MPAKA JESHINI AFRICANA, WAMEWEKA MIPAKA, WALIPOFIKA MAHALI KUNA NYUMBA ZA WAKUBWA NA UZIO UMEPITA WAKAWAKWEPA WAKABANA WALALAHOI, TENA WAKAWEKA MIPAKA NDANI YA VIWANJA VYA WATU. HUO NI UONEVU, SHERIA NI MSUMENO KAMA UMEAMUA KUVUNJA VUNJIA WOTE SIO BAADHI YA WATU.
TANROADS WAMEKUWA NA MAMBO YA AJABU SANA TENA SANA. WAMEKUWA WAKIJIINGIZA KWENYE MALUMBANO NA KUPELEKANA MAHAKAMANI NA WATU NA SIJUI NANI HUWA ANALIPA HIZI GHARAMA ZA MAHAKAMA, WAKATI MAMBO MENGINE WANGEWEZA KUJIHADHARI MAPEMA BADALA YA KULITIA TAIFA HASARA KWA KUTUMIA GHARAMA ZA SERIKALI KUAMKA USIKU KWENDA KUVUNJA STRUCTURE ZILIZOJENGWA KWA GHARAMA KUBWA TENA NYINGINE ZIMELIGHARIMU TAIFA FEDHA ZA KIGENI KUAGIZA HIVYO VIFAA NJE YA NCHI.
MWISHO: NAFIKIRI TANROADS WATAHITAJI KUBADILI MFUMO WA UTENDAJI NA WAACHE UBABE NA UBABAISHAJI.
Kitu cha kuchangaza kabisa ni vipi rais alialikwa kufungua Hoteli ambayo imejengwa kwa kuvunja sheria za nchi? Je wasaidizi wake hawakuwa na taarifa na hili, je huku si kumdhalilisha rais? je Tanroads wamefanya hivyo bahati mbaya au kwa kudhamiria? mimi sielewi kabisa ni nini kimetokea, Haiwezekani kwa muda mrefu hiii hoteli imekuwa ikipigiwa kelele imejengwa kwenye hifadhi ya barabara, leo hii unasikia rais amefungua keshokutwa unasikia imevunjwa,
ReplyDeleteNANI KAMDHALILISHA RAIS?
LAZIMA MTU AU WATU WAWAJIBISHWE HAPA, KUNA UZEMBE MKUBWA TENA SANA. HAIWEZEKANI, HAIWEZEKANI AHAWEZEKANI LAZIMA KUAN UZEMBE MKUBWA, LAZIMA AWAJIBIKE MTU. HUKU NI KUMDHAHILILISHA RAIS. HAPANA NI LAZIMA AWAJIBIKE MTU.
NANI KAZEMBEA HAPA???????????????????
Jamani mie nasema Rais wetu JK ameabishwa yaani kapakwa uchafu! Yaani kumbe kaenda kwa heshima yote kufungua hoteli kumbe kenda kushiriki ufisadi bila hata ya kuonywa na washauri wake, huku ni kumtukanisha rais matusi ya nguoni, hata hao TANROADS wenyewe waliposikia kuwa rais anakwenda kufanya ufunguzi pale huyo Mrema wa TANROADS alipaswa amuonye mzee.
ReplyDeleteJK baba wamekupaka matope machafu.
Halafu uvunjaji wa aina hii ndio jamaa yupo wrong lakini kuna kitu kimejificha kuhusu hili swala zima hapa kuna kukomoana fulani, inaelekea kuna watu tena wakubwa tu serikalini hawajakatiwa chao. mh
This is the cost of engaging stupid designers and planners. Poor Managent!! Go read the TANROADS acT OF 2008.
ReplyDeleteNO DOUBT WATU WANATAKIWA KUWAJIBIKA AU KUWAJIBISHWA.
ReplyDeleteKWA VYOVYOTE TUKIO LA KUBOMOA KITU AMBACHO RAIS AMEZINDUA SIKU CHACHE TU ZILIZOPITA HALIMPI SURA NZURI.
WASHAURI WA RAIS WALIPASWA KUCHUNGUZA KABLA YA KUMRUHUSU RAIS KUFANYA UZINDUZI. DISPUTE YA HOTELI NA TANROADS NI YA MUDA MREFU NA TUMEISIKIA MARA NYINGI KWENYE MEDIA. WASHAURI WALIPASWA KUCHEKI NA TANROADS. HAWAKUPASWA KUMPELEKA RAIS HUKO.
KWANI VIONGOZI WA MKOA NAO WALIKUWA HAWAJUI?? KWA NINI RAIS ADHAALILISHWE KIASI HICHO.
TATIZO NI KUWA MUHESHIMIWA ANAPENDA KUJIPELEKA KILA KONA, HIYO HOTELI TUNAJUA NI YA MSHIKAJI WAKE ( CLOSE FRIENDS) NDO MAANA HAKUJIULIZA MASWALI, ANADHANI TANROADS WANGEMUOGOPA..
ReplyDeleteWELL DONE TANROADS NINGEKUWA NA VIJISENTI NINGEWAFANYIA CONGRATS PARTY
congraturations Mr Mrema u are a real man with balls hakuna kuogopa hata angekuwa mtoto wa JK lazima watanzania mjifunze kufuata sheria nobody is above the law. Nashangaa watu wengine wanalalama kwa nini Tanroads wameamua kubomoa sasa hivi.Kama walishamuonya mwenye hotel na jamaa akaendelea kubisha kwa kufikiria akimualika JK haje afungue hotel basi jamaa wa Tanroads wataogopa nafikiri Tanroads walikuwa na right ya kuja any dayany time kubomoa ukuta na nataka mrema amtumie invoiceya kulipia gharama yakubomoa pamoja na faini ya kuvunja sheria. WELLDONE MR MREMA USIOGOPE MAFISADI WALA NDUGU ZAO
ReplyDeleteNavoiona hii ni kwamba kitu kilikuwa hivi; Tanroads na wenye hotel walikuwa wanavutana ila jamaa hawa wa hotel wakawa wajeuri. Na kugongelea msumari wa mwisho jamaa wa Hotel wakamleta rais kufungua hotel, na baada ya hapo wakaona sasa wao ni untouchables kwa sababu mkuu " kaihalalisha" hotel. Teh teh, jamaa Tanroads wakaona sasa ngoja tukuonyeshe, wakaipiga nyundo after 2 day!! So hapo kuna kisasi pamoja na sheria zimechanganyika,..na uzembe pia. Bongo bana..Naipenda Tanzania
ReplyDelete1. Rais alienda kufungua hoteli na siyo kitu kingine na hoteli ilifunguliwa na inafanya kazi. Nasema Rais hajakashifiwa.
ReplyDelete2. TANROADS walienda kubomoa uzio ambao ulijengwa kwenye Road reserve baada ya kuwa wametoa notice kisheria.Notice haikuwa ya kuvunja hoteli bali uzio. Walichofanya TANROADS ni sahihi. Hawakubomoa hoteli iliyofunguliwa na Rais. Rais hajakashifiwa. Kashfa ni yake mwenye hoteli kwa kukaidi maagizo ya TANROADS.
3. Hoteli bado iko intact. Anachotakiwa kufanya ni kujenga uzio eneo linalokubalika kisheria. Mimi ni mkazi wa Baraa na ninayo nyumba upande huo huo ambako hoteli hiyo ilipo. Nilipokamilisha kujenga nyumba yangu which is 50 metres from the centre of the road, uzio wa ukuta nilikuwa nimejenga ndani ya road reserve kiasi cha mita moja. Nilipewa notice na manispaa wakati huo ya kuuondoa ukuta. Ukuta-mind you- siyo nyumba. Sikubisha. Nilichukua mafundi nikawapa kazi ya ‘kubomoa’ ukuta kwa kutoa tofali moja baada ya nyingine hadi ukuta ukawa haupo tena. Matofali hayo hayo nikajengea ukuta mwingine mita 10 ndani zaidi. Hakuna kilichoharibika. Nilitimiza wajibu wangu kwa kuwa raia mtiifu wa sheria.
4. Sasa swali nauliza. Kashfa kwa Rais hapo iko wapi? Baadhi ya wanasiasa wanataka uongozi wa mkoa uwajibike kwa kumpotosha Rais kweli wako sahihi?
5. Ninakumbuka mwaka 1971 Rais Nyerere alikwenda kufungua jengo la IPS likiwa linamilikiwa na AgaKhan, siku ya pili jengo hilo likataifishwa na serikali iliyokuwa chini ya Nyerere na akapewa Msajili wa Majumba. Nyerere hakukosea. Yeye alialikwa kufungua jengo. Lakini sheria ya Acquistion Buildings Act ya 1971 ikachukua mkondo wake. Mlio watu wazima huenda mnalijua hilo. Sasa JK kaenda kufungua hoteli na hoteli bado inafanya kazi kashfa hapo iko kwa JK au kwa mwen ye hoteli? Jamani let us be objective. Aliekashifiwa hapo ni Bwana Tarimo wala siyo Kikwete.
Dont mess with Arusha!! Hii sio Dar.. In Arusha you dont mess with people or law. Dar people talk too much, Arusha is action.
ReplyDeleteHatufanyi mambo Kienyeji Arusha....msituharibie mji mkaufanya kama Dar...kumekuwa na pany roads...Unajenga kijinga tunabomoa...kazi nzuri sana Tanroads..!! Mtu utajengaje Hoteli mpaka unamuita raisi lakini umevunja sheria? Ujinga huo...!!
ReplyDeletekwa hiyo mwenye hoteli alifanya ubishi muda wote kwa jeuri za kibongo najua atakuwa aliwaambia TANROADS mie najuana na Rais hamuwezi kunifanya chochote, hivo akafanya juu chini kumleta Raisi kufungua ili kuwaonyeshea TNROAD kwamba yeye ni nani! Hivo Tanrd wakasema okee, sasa sisi tutakuonyesha kwamba hata Raisi hayuko juu ya sheria! patamu hapo, and Hongera TNROAD, hamkukubali kutishwa na lolote,
ReplyDeleteWEWE BARAA HUJUI UNACHOONGEA NDUGU YANGU NI BORA UNGEJINYAMAZIA.
ReplyDeleteRAISI HAJAKASHIFIWA ILA AMEDHALILISHWA.
TUNACHOKIONA HAPA NI KWAMBA LABDA AMESHAURIWA VIBAYA NA KINGINE KIKUBWA ZAIDI NI KWAMBA IDARA ZA SERIKALI NA SERIKALI KWA UJUMLA HAWA-COMMUNICATE.
MOJA YA KAZI ZA RAISI NI KUSIMAMIA SHERIA. SASA KWA NINI APELEKWE KUZINDUA HOTELI AMBAYO IMEJENGWA KWA KUKIUKA BAADHI YA SHERIA ZA NCHI??
Wewe Anon wa dec 22, 10:23:00PM. Hujui kiswahili wewe. Utasemaje Rais kadhalilishwa. Kudhalilishwa ingemaanisha kuwa baada ya Rais kufika pale wale wenye hoteli wamesema maneno ya kumuaibisha. Hiyo ndiyo kudhalilishwa.
ReplyDeleteHata hivyo unaniambiaje” NI BORA UNGEJINYAMAZIA,” kwa vile Rais hajakashifiwa. Soma vizuri aisee ni wapi nimeandika kuwa Rais amekashifiwa? Au hujui kusoma kiswahili? Ni dhahiri wewe hujui maudhui ya hoja yangu. So just shut up. Nimesema Rais hajakashifiwa but mwenye hoteli ndiye kajikashifu mwenyewe kutokana na upumbavu wake. Yeye alishaambiwa juu ya uzio kuwa ubomolewe akabisha na upumbavu wake ukamfanya aamini kuwa kwa vile JK kaifungua hoteli ile he will be untouchable. Hayo ndiyo maudhui yangu. Vipi wewe.
BOSS wa TanRoads amenyimwa mshiko/mgao, ndo maana ameamka mapema kuvunja ukuta.
ReplyDeleteWenye hoteli wamejiona wako juu kwa kuamualika Mr.JK, hivyo wakaona hamna haja ya kumpa kitu kidogo mtu wa TanRoads hoping kuwa ataogopa kuvunja ukuta kwa kuwa wakina Diria & Co,wako karibu na System ya nchi.
Please Bro Michu usii bane hii comment:
SWALI: TAnroads walikuwa wapi wakati UKUTa unajengwa?
SWALI 2: Engineer na mkaguzi wa majengo wa manispaa walikuwa wapi wakati ujenzi unakamilika?
ujumbe kwa Mh.JK na Watumishi wa System wa nchi...
Boss wa TanRoad na Afsa Majengo/ujenzi wa mansispaa ya Arusha washughulikiwe na kuwajibishwa ili iwe mfano kwa wengine,kwani waliacha ujenzi ukamilike ile kuweka sawa mazingira ya RUSHWA.