Mixmaster na gwiji wa Old Skul duniani DJ Luke anatoa salamu kwa wadau wote wa Globu ya Jamii, akiwatakia Xmas njema na Heri ya mwaka mpya. Anasema pamoja na kwamba ashkilimu inatesa huko Washington DC aliko lakini Libeneke ni kama kawa na Houston wakae mkao wa kula kwani anakuja kuwashika na vitu vya enzi za kina Dj Kalikali na John Peter Pantalakis, DJ Young Kim (RIP), Choggy Sly (RIP), Super Deo, Pop Juice, Eddy Sally (RIP) Seydou, Fast Eddy, Bonny Luv, Mao Lwangisa na wengine wengi tu.--------------------------------
Globu ya Jamii inapokea salamu hizo kwa niaba ya wadau na kumtakia DJ Luke mafanikio katika kuuaga mwaka na kuukaribisha 2010. Globu hii pia inatoa shukrani za dhati kwa DJ Luke kwa kuwa mtu wetu wa karibu sana na huwa hasiti kutoa msaada wa hali na mali wakati wowote. Asante DJ Luke kwa moyo wako mkunjufu. Wewe ni mfano wa kuigwa kwani tunajua fika wewe ni mojawapo ya nguzo kuu za wabongo waishio DC katika shida na raha.
-Michuzi
John Peter Pantalakis yuko wapi?najua Mao Lwangisa yuko US,nilisoma na kaka yake Kwame pale Mzizima 1978-1981.
ReplyDeleteMtaalam wa Old Skul zetu USA,Luke uko juu,!! Lete ratiba ya mwaka 2010,tunajua Xmas unapiga Houston,TX.
ReplyDeleteDj Luke...maini ya ng'ombe hayazeeki.Zaidi ya miaka 20 ndani ya fani.
ReplyDeleteMichuzi
ReplyDeleteAllow me to personally thank you for maintaining this life line to Tz' I dont think I can thank you enough for lifting many of us with your often sharp, humorous quips,cartoons,or your little stories I can only wish you the best and wish that you are granted what you wish for
Heri ya Noeli na mwaka mpya
Wakatabahu
naomba kukusahihisha Ankal,GWIJI WA OLD SKUL DUNIANI.kwa kipimo gani? hapo tu.otherwise na sisi tunakutakia heri ya Noeli na mwaka mpya
ReplyDeleteKwa ujumla Dj Luke amekuwa kiunganishi kizuri kwa taarifa za waTanzania kwa waTanzania.
ReplyDeleteNasikia ni "mwema" kwenye fani na namtakia kila lililo jema, lakini NAJUA NI MSHIRIKI WA MAMBO MENGI YA WATANZANIA NA HUTUJULISHA HABARI MBALIMBALI ZIHUSUZO WATANZANIA.
Kwa hili NAMSHUKURU NA NAMTAKIA MWISHO MWEMA WA MWAKA NA MAFANIKIO KWA MWAKA UJAO.
Ahsante Dj Luke kwa salamu za Xmas.
ReplyDeleteWadau
Lincoln na Katoke Streets
O'Bay
DJ LUKE HIYO SNOW UMEICHOTA UNAIPELEKA WAPI MAANA NAONA WALK WAY IMESHASAFISHWA AMA!
ReplyDeletedj luke tunajuwa ni mtu mwema lakini akuwi kweli hii kitu .iko kwenye damu. ukimuona mkimya utafikiri kweli ,
ReplyDeletejamani dj luke bado upo umshukuru mungu wengi madj wenzako wameondoka ,unabidi usali sana .usijisahau
ReplyDeleteHarusi ya DJ Luke ni mwaka kesho ?
ReplyDeleteNakutakia kila la heri DJ Luke "Chonchoryo"
ReplyDeleteNi mie mdau wa blog ya jamii na mjumbe wa kikosi kazi cha utundu wa kuthubutu - Urutundura Inc. Tanzania