Nyumba ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesa Benno Ndulu inavyoonekana baada ya kufanyiwa ukarabatiwa mkubwa uliogharimu kiasi cha sh. bilioni moja. Ipo katika mtaa wa Tumbawe, Oysterbay, Dar es Salaam.
picha imepigwa leo na mpiga picha mkuu wa Globu ya Jamii



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 70 mpaka sasa

  1. Ankal, naona mafisadi wameanza kukutumia sasa

    ReplyDelete
  2. UKARABATI WA SH. BILIONI MMOJA,WOW!SHILINGI BILIONI MMOJA NI KAMA US $770,000.NAISHI MAREKANI CALIFORNIA SEHEMU AMBAKO PROPERTIES ARE BELIEVED TO BE SO EXPENSIVE BUT KWA HELA HIYO UNANUNUA A BRAND NEW HOUSE WITH 5 BEDROOMS/5 OR 4.5 BARTHROOMS.KWA MAANA HIYO NYUMBA NI GHALI TZ KULIKO CALIFORNIA KWANI KWA PESA HII TZ NI UKARABATI TU.NAONA KODI ZA WATANZANIA ZINAKUWA ABUSED TO THE EXTENT THAT WILL MAKE SOMEONE WITH A SOUND MIND SICK TO THEIR STOMACH.KILA LA KHERI WADANGANYIKA

    ReplyDelete
  3. kweli ni tambarale kwa bln 1 ni shule ngapi zingekua na madawati? kaka michuzi nina machungu ungetoa hii habari hapo vinginevyo itakua aliye juu mfuate juu.
    mwenye nchi. halafu nina machungu!? BABA WA TAIFA NYERERE UKO WAPI? KWANINI MZIMU WAKO USIWASHUKIE HAWA,

    ReplyDelete
  4. There are things money can't buy. Renovating that house Tshs. 1bn/= TRUST - Priceless...

    ReplyDelete
  5. Mzee Michuzi, mambo kama haya yanatokea Tanzania tu, hakuna kwingine duania mkuu, kusema ukweli hapa nilipo nalia huku naandika kuhusu kodi yangu mkuu.

    Kusema ukweli nakwatwa PAYE nyingi sana halafu yanayofanyika ni UPUUZI KAMA HUU.

    MUDA SI MREFU TUTASHIKIANA ............ TUMECHOKA.

    ReplyDelete
  6. hiviii?...
    samahani ankal, nimesahau sijui nlitaka niandike nini.
    kwaheri tu.

    ReplyDelete
  7. Gharama yake ktk paundi sterling ni kama paundi 700,000 za Kiingereza (Ths Bilioni 1.7 za kitanzania) . Hii ni value for money spent, hakuna cha kushangaa maana hata jijini London huwezi pata jumba ka hilo maeneo ya Kensington, Hydepark, Sloane Square au Marble Arch kwa kina Tony Blair mstaafu au Lady Madona n.k bila kuwa na paundi sterling za Kiingereza milioni 4 na zaidi.

    Kwa kisai hicho cha paundi sterling 700,000 utaishia kupata flat ya vyumba viwili tu na ka-sitting room kaaadogo kabisa.

    Labda umasikini wetu ndiyo maana paundi sterling 600,000 haionekani kuwa vijisenti. Tanzania inatakiwa tuanze kufikiria nchi yetu iwe na GDP ya angalau paundi bilioni 80 za Kiingereza tumzidi Abramovic mwenye utajiri wa paundi za kiingereza bilioni 52.

    Tukipata mind-set za ukubwa wa uchumi kujilinganisha angalau na South Africa basi nchi yetu itapiga hatua, lakini ikiwa vigogo wananunuliwa kwa vijisenti au uchumi wetu tunajisifia kwa vijisenti basi tutaendelea kuwa masikini.

    South Korea, Singapore, Taiwani waliachana na uchumi wa 'vijisenti' miaka ya 1970 na sasa uchumi wao ni mfano wa kuigwa na nchi za kiafrika kama Tanzania.

    Mdau
    Jijini London

    ReplyDelete
  8. HUKU NI KUTOKUWAJIBIKA. UKARABATI WA BILLION MOJA KWA NYUMBA WAKATI MKUU WA MKOA WA DAR ALITANGAZA KILA MWANAFUNZI ANATAKAYE CHAGULIWA KUINGIA KIDATO CHA KWANZA AJE NA DAWATI KISA ETI SERIKALI HAINA UWEZO.

    ReplyDelete
  9. HIVI HII NYUMBA IKIUNZWA NI WATU WANGAPI WATAJITOKEZA KULIPA ZAIDI YA BILION MOJA

    ReplyDelete
  10. HII NI KUITENDEA DHAMBI JAMII YA WATANZANIA WENGI AMBAO NI MASIKINI.

    HIVI HAWA JAMAA HAWAJUI KUWA DUNIA NI MAPITO TU. HIVYO HAKUNA HAJA YA KUWA MLAFI. HUU NI ULAFI TU. DAUD BALALI YUKO WAPI BWANA BENO.

    ReplyDelete
  11. MJOMBA KWANI HUYU NI MEMBER WA CHAMA CHA MAFISADI AU VIPI??

    ReplyDelete
  12. Kaka Michuzi! unajuwa mtu anayekutukana hakuchaguliii tusi,kuhusu ukarabati wa nyumba ya Gavana wa benki kuu kwa gharama hizo ni matusi makubwa kwa watanzania wote na sasa nimeamini ule usemi wa yule askofu wetu aliyesema nchi inatembea bila nguo kuwa ni kweli! Rais wetu yuko wapi kuwabana hawa mafisadi wakubwa! Yeye ndiye mwenye vyombo vyote wa kupambana na hao watu. na tusisahu kuwa hawa jamaa wa benki wana mpango wa kukopesha pesa za kujengea majumba,je kiasi gani cha pesa za walipa kodi kitatumika.
    Watanzania tuamuke na tuanze kukemea vitendo kama hivi.
    Wazalamo ukitoka tuu nje kidogo ya Dar utakuta wanateseka ile mbaya hata maji safi hawana. Hivi kwa nini mungu alitulaani kuwa anatupa viongozi wanaojali maslahi yao tuu na kutojali jamii inaishi je? Nimeandika yote hayo wakati machozi yakinitoka.

    ReplyDelete
  13. dah bro misupu,umeamua kumuanika fisadi nje nje kweuuupee..ahsante sana kama huwa anapitia kijiji hiki basi ujumbe wa wavuja jasho utamfikia.kuna watanzania zaidi ya mil 10 wanakula mlo mmoja kwa siku nini watoto wao kukosa shule.halafu jamaa anakarabati nyumba kwa bil moja! matusi ya nguoni hayo!!hakyanani nikikutana nae hadharani namvaa maungoni..kikwete ammulike huyu nae aonyeshe paysleep yake kama ina mishahara ya kutosha kukarabati hiyo nyumba..mwizi mkubwa huyoo..swali ni kwamba serikali ya jk haimuoni?

    ReplyDelete
  14. only in Tanzania!
    Hata mie mkuu wa Ufisadi hapo nimeumia roho! IT MEANS KUNA MTU AMENIZIDI! WTF!

    ReplyDelete
  15. KAMA HII NYUMBA INGEKUWA NEW BUILT,FOR TSHS 1BIL TUNGESEMA HIO NI KUFURU,SASA RENOVATION FOR TSHS 1BIL PLEASE!!!!THATS DISRESPECT TO MILLIONS OF TANZANIANS INCLUDING ME WHO ARE STRUGGLING TO PUT FOOD ON OUR TABLES.....HOW COME THE BEST PRESIDENT SO FAR COULD ALLOWS THESE SCUMS!!!!IM SURE THIS CAN NOT BE DONE WITHOUT HIS KNOWLEDGE/APPROVAL....AT THE SAME TIME THE EPA SCANDAL IS STILL HOT..

    ReplyDelete
  16. Hii Nchi Hii

    Basi hili nalo litaisha hivihivi tu. Mimi Sioni Dhamira za DHATI za viongozi wetu kuendeleza nchi yetu, nadhani kuna haja sasa ya kubinafsisha Wizara na Idara za Serikali kwa Wawekezaji wa nje.

    Si kwamba tumeshindwa kuendeleza Viwanda vyetu tu, sasa ni dhahiri na nchi imetushinda. Hatuna vipaumbele kabisa, ..na huwezi juwa pengine mwakani utaambiwa Gavana kauziwa hiyo nyumba kwa milioni 120.

    Mbaya zaidi kama kweli ilitumika gharama hiyo, basi zaidi ya asilimia 75% ya hizo pesa zimeenda kununulia bidhaa za nje, hata rangi utaambiwa zimeagizwa toka Afrika Kusini.

    Matukio kama haya yananifanya nizidi kuwadharau viongozi wetu.

    ReplyDelete
  17. TSHS. 1,000,000,000:00 JAMANI NYEE, KWA KWELI UMASIKINI UTAKUWEPO HADI KIZAZI SI HIKI HADI KIJACHO KIPOTEE NDO PENGINE VIONGOZI WA WAKATI HUO WATAJALI WATU WAO, JAMANI NENDENI RWANDA MUKAONE KAGAME ANAVYOJALI WATU WAKE, MIJI NI MISAFI HAKUNA RUSHWA, HAKUNA UFISADI HATA TONE, SASA KATOKA BILALI KAJA BILALI, NI UTAMADUNI AMBAO NI MGUMU KUOKOMESHA SISI WATANZANIA, UBUNAFSI HUMO NDANI YA DAMU YETU HATUJALI WENZETU, VYOMBO VYA UMMA VINATAKIWA KUFANYA MABADILIKO JAMANI. WATANZANIA EBU TULIJADILI HILI KWA KINI IKIWEZEKANA NA WABUNGE WALIULIZIE HILI KANI NI PESA ZETU WALIPA KODI!!!

    ReplyDelete
  18. Na hii ndio sababu Africa ni maskini na tutaendelea kuwa maskini! Bil 1 kama ni mradi wa nyumba za bei nafuu za mil 20, 20 zingejengwa nyumba 50 ambazo famili 50 za wachapa kazi wazalendo wa Kitanzania wangeweza kuishi maskini! Hivi watu kama hawa watakumbukwa kwa lipi jamani?
    Wenzetu hawaendelei kimiujiza!!!!!! Wanachapa kazi na wanawajibika na kuwajibisha! Washikaji si tuingie mtaani angala maandamano tu ya kupinga matumizi mabaya ya pesa za serikali.

    ReplyDelete
  19. DUH HAPO HATA MAWAZIRI WA UK WAKIONA WATATAKA KUHAMIA KWENYE SERIKALI YA TANZANIA, WASHACHOKA VIBANDA VYAO UK VIDOGO WALIJARIBU UFISADI SASA HIVI WANADAIWA WARUDISHE UK WABUNGE, TANZANIA RAHA HUAMBIWI RUDISHA UNAJENGA TU KWA KODI ZA WATU. HARAMBEEEEEEEEEE IRUDISHWE KABLA HATUJAUMIA MANAKE TUSHAUMIA TUNAZIDI KUUMIZWA. MIRAMBO.

    ReplyDelete
  20. JAMANI SI MUMUACHEEEEEEEE KATENGENEZA PESA KASOMA NYIE MNABAKI KUPIGA KELELE HAPA YEYE ANATENGENEZA. KIMARO.

    ReplyDelete
  21. Anko Michuzi tumbo la kuhara limenibana ghafla. Hizi takwimu za kukarabati nyumba kwa Billion moja gholofa mbili????? Hii imekaaje mbona nasikia kizunguzungu???? Si wangejenga hata kagorofa ka watu hata ishirini na tano pale manzese na kupunguza msongomano wa vichochoro??? Uhandisi gani wa bongo huu jamani tunaibiana kimachomacho? Japo kuwa siyo mwanasiasa kama akina Zitto kabwe hapana hii imezidi tena inatia kichefuchefu. Rais wetu Jk kila siku anazunguka kuomba misaada kwa ajili ya watanzania lkn viongozi wachache wanaitumia kwa manufaa yao. Nyumba ya gavana inapokarabatiwa si bodi ya benki kuu inakuwa inapitisha hayo matumizi, Ina maana waheshimiwa pamoja na kwenda shule wanashidwa kuwa waitia hasara serikari???? Maana huu ufanyikao ni uny'ang'anyi kwa mali za umma wa watanzania. Hii Benki kuu nadhani kua jinamizi amablo ukiingia huko lazima uapishwe kuwa mwizi ndiyo uanze kazi hii siyo bure. Watu hawaogopi hata kama kesi zingine za ufisadi hazijaisha mahakamani wao wanachota tuu???? AMA KWELI MAISHA YA BONGO MSWANOOO MWEEEEEE TAMBARARE!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  22. kikwete & PINDA vp?2010? jamani hiii sio sawa kabisa.

    ReplyDelete
  23. ndi maana aliruhusu BoT kuwa benki ya kukopoesha watu binafsi!

    Tanzania walifukuza wafanyakazi....wakajiongezea mishahara badala ya kupunguza mishahara na kuongeza watu kazini!

    Mbunge wa Tanzania analipwa zaidi kuliko mbunge wa Ubelgiji!

    ReplyDelete
  24. My God!Mungu wangu! Aluu! Huo ukkarabati si dhamani ya nyumba mpya sijui ngapi,alfu watanzania wanakufa na njaa,ukosaji wa dawa, maji safi ya kunywa na elimu bora kisa ukosaji wa majengo,madawati na walimu na mishahara kwa walimu hao.Kweli ni haki kwa watanzania jinsi kodi zao zinavyotumika?

    ReplyDelete
  25. The next generation walie tu, kwa sababu nina uhakika hatutawaachia chochote zaidi ya vumbi la umaskini.
    Hizo renovations za dola milioni moja katika nchi ambayo inashika namba nne kutoka mwisho kwa umaskini duniani zinamnufaisha nani?
    Kweli safari yetu bado ndefu.

    ReplyDelete
  26. Angry Intro Said, mate you have got to learn to chill. I bet you moan about how this man could spent those money to refurbrish his bangalow like everybody alse. You went too far. You are too thrilled!!. Time will come Wadanganyika wataelewa ukweli. Hope it's not too late!!
    Mdau Nansio

    ReplyDelete
  27. Nyie watu mnaoishi marekani n.k. hivi mnajua mfuko mmoja wa cement unauzwa shilingi ngapi Bongo? Acheni blah blah.

    ReplyDelete
  28. Daaah 1/=Billion si mchezo , Tax za wananchi ndiyo zimeishia hapo kwenye ukarabati, atleast huku ugaibuni ukikatwa Tax hata barabara tunaziona au hata watoto wa shule wana-mabasi yao ya kuwapeleka shule....lakini bongo ah? Kalagabahooo dah hiyo sijawahi ona! Mdau- - Dallas , Texas

    ReplyDelete
  29. ubepari-uchwara = ufisadi!
    kufuru. ukilalamika unaambiwa 'unataka gavana alale katika kibanda kama cha manzese?' mafisadi wanashindana katika kila kitu: umetumia pesa za walipakodi kiasi gani kukarabati nyumba? umevaa suti ya bei mbaya kutoka wapi? shirika lina mashangingi mangapi? harusi ya kuoza binti yangu haijawahi kutokea hapa duniani!nk zote hizi ni mind-set za ubepari-uchwara.
    wakati huo huo juzi tumeonyehwa hapa hapa watoto wa shule ya msingi vingunguti wakiwa wamekaa sakafuni na wafugaji huko wilaya moja ya arusha wakigombania chakula cha msaada, nk.
    kufuru!!

    ReplyDelete
  30. Afu na wewe anon Wed Dec 23, 11:27:00 PM acha ukuda, au ndo umetumwa? shukuru ni mtandaoni tu(
    hata kama mfuko ungeuzwa 50000, stil kwa renovation haiwezi fika 1 na sifuri tisa mbele(
    But stil I believe, one day they gonna pay the price for all they've done:(:( usiibanie hii michuzi

    ReplyDelete
  31. Jamani mtu anayewasaidia kupangilia mfumo wenu wa kifedha kwenye kiinchi chenu uende vizuri na kuwa sambamba na uchumi wa dunia nzima,bado mnakishambulia kibanda chake mlitaka kiwe cha udongo ndio mfurahi.Waone vile.Mambo ya fikra za nyerere za kimaskini maskini na ufinyu na wivu wa maendeleo ndio hauwafikishi mbali,ila mnabaki hapo hapo mlipo.Kama wewe ni maskini basi unajua la kufanya,lakini sio eti mtu aache kujiendeleza eti kisa watu watamzania ni fisadi.Now akiamua kuwagawia watu sehemu ya alichonacho then its all good kama hataki basi na nyie mtafute vyenu.Si mlitaka kuwa huru ,which means uza chochote unachotaka au nunua chochote unachotaka sasa mnalalamika nini.Nendeni mkatengeneze chai mnunue na chapati mle mfunge midomo,life goes on.My advice to u all wenye wivu,be an innovator,a creator,sell,make profits enjoy na familia yako.Kwaheri.

    Mdau mhangaza wa kanazi
    http://duniayetukubwa.blogspot.com/

    ReplyDelete
  32. NAKWAMBIA KUANZIA AWAMU YA PILI YA URAISI MPAKA YA MISHO WA DUNIA NI MAJAMBAZI. hukuna mwenye nafuu, mwlimu alikua anawaita MANYAN"GAU

    ReplyDelete
  33. mbagala watu walilipuliwa namabomu wengine walipoteza maisha,viungo nahata kuhalibikiwa kwa vitu vyathamani kama nyumba,magari,nk chaajabu hakunahatammoja aliyekarabatiwa au kupewamalipo ya aina yeyote ile!leo mtu anafanyiwa ukarabati 1bln?hivi ni tone ngapi za madawa tungewezakujaza mahospitalini?au wale wanaolala nje wangewezakujengewa japo Hall nawaowakapatakupumzika mbu wa mitaani,mi nazaniumefika wakati sasa watanzani kusimama nakudai haki zetu kwanjia yoyote ile.inabidi tuonyeshe chuki zetu pindi zinapotokea issue kama hizi ikiwezekana tufanye hata maandamano.nakama hali itazidikuwa hizi tuchukue sheria mkononi maana ndio wanavyotaka kwani itandelea hivi mpaka lini?

    ReplyDelete
  34. Jamani haya mambo si yakucheka wala kufanyia utani!this is a big amount ever for renovation!!and all are tax payers money..daah inauma sana sana!
    Hiyo hela unanuna nyumaba mitaa ya kiposh chelsea mtaa mmoja na drogba!
    clik hapa uone bei za flat..
    http://www.zoopla.co.uk/house-prices/london/cheyne-place/ zaidi ya yote hapa uk Gordon brown alirudisha kiasi kidogo tu alichotumia kulipia usafi nyumba yake...daah inauma mno
    mdau uk

    ReplyDelete
  35. acha kutuletea picha leta concrete evidence za hio Billion Moja

    ReplyDelete
  36. INA MAANA AKIJA GAVANA MWINGINE NAYE NYUMBA YAKE ITAKARABATIWA KWA BILIONI NYINGINE?

    KWELI TANZANIA SHAMBA LA BIBI..!!

    NETWORK ENGINEER (NE)
    READING, UK.

    ReplyDelete
  37. WATANZANIA WENGI NI WAONGO NA SI WAAMINIFU PIA.WEWE MDAU UNAYESEMA KUWA UTAJIRI WA ABRAMOVICH NI GBP 56 BIL. UMEPATA WAPI HIYO FIGURE? KWA NYUMBA HIYO KUGHARIMU BILLION MOJA KWA MATENGENEZO NI WIZI WA MCHANA NA KWA VILE WATANZANIA WENGI HATUJUI HAKI ZETU AU HATUJUI KUPIGA KELELE TUTAWANUFAISHA WACHACHE KWA FAIDA YAO NA YA FAMILIA ZAO.TUMESHAIBIWA VYA KUTOSHA KILA KIONGOZI ISIPOKUWA NYERERE WOTE WALIKUWA WEZI NA WALA RUSHWA LAKINI KWA SABABU YA ELIMU ZETU DUNI NA UPOLE WETU TUNAIBIWA WATU WANAONA NI SAWA TU...LAKINI WANGEJUA KWAMBA HUO WIZI UNA EFFECTS KWA UCHUMI WA NCHI WANGELIA KWA UCHUNGU. TANGU UHURU LEO MIAKA 50 HATA BARABARA YA KUUNGANISHA NCHI HAZIPO MPAKA UPITIE JIRANI, KILA KITU KIPO OVYO OVYO TU KIKULIMA KULIMA TU.HATUJALI TUPO TUPO TU.RAIS KIKWETE MWENYEWE KAKIRI KUWA BAJETI YA SERIKALI YA 40% KILA MWAKA ZINAIBIWA NA VIONGOZI HUKO SERIKALINI JE HILO HALITHIBITISHI KUWAPO KWA RUSHWA NA MATUMIZI MABAYA YA PESA ZA UMMA? JE PESA HIZO ZOTE ZINAZOIBIWA NA WAJANJA HUKO SERIKALINI NA KWENYE MASHIRIKA YA UMMA ZINGEPELEKWA KWENYE UJENZI WA BARABARA NA KUPELEKA HUDUMA ZA MAJI NCHI ISINGEKUWA MBALI? WATANZANIA TUKATAE RUSHWA NA TUWE WAKALI TUTAFIKA MBALI SANA KIMAENDELEO LAKINI WANANCHI TUKIWA NA MAWAZO YA KIBANGI BANGI NA KILEVI LEVI TUTABAKIA HAPO TULIPO SIKU ZOTE.

    ReplyDelete
  38. Jamani nyie mnaomlaumu Gavana wa Bank ni kumwonea tu. Yaani mimi nakumbuka wakati tunakaa nyumba ya serikali mzee alihamishwa kwenye cheo kingine ikabidi tuingie kwenye nyumba ingine. Yaani matengenezo tu ilikuwa kama Tsh Million 60 hivi. Mzee alikuja juu sana lakini hakuna kitu ni watu wa Administration ndio wanaopiga panga wanaongezea vijisenti humo humo ili ikizidi ni yao. Mtu anayefanyiwa ukarabati hapati hata senti moja kwa hiyo msimulaumu Gavana buree. Nendeni pale BOT muulizie kwenye Administration dept. Yule Director si ndio ana kesi sasa hivi?

    ReplyDelete
  39. Bahati mbaya kaujamaa bado kapo damuni mwetu ndio maana tunatoa machozi kuhusu gharama kama hio kurekebisha nyumba ya Gavana wa Benki Kuu. Tunalia sana kwa kupoteza vijisenti wakati dunia tunayoikimbilia na kujilingalinisha nayo kila siku hivi ni vitu vidogo.

    Amueni kimoja..twende mbele na tuvikubali hizi gharama kama part and parcel of free market enterprise where Tanzania are new entrants au turudi nyuma kwenye ujamaa wetu maana hapo gharama kama hii kweli ni ya kufokea.

    You cant have it both ways. Chagua moja then ZIP it up.

    ReplyDelete
  40. Nayeweza kuinyoosha nchi hii ni mtu mmoja-US Blogger.

    Mchumi mwandamizi.

    ReplyDelete
  41. safi sana gavana ninyi ndio wenye hati milki ni tanzania na mnajua kuitumia nchi wengine wakipewa t shirt na vitenge na vilemba vya ccm wanashangilia

    ReplyDelete
  42. SIRUDI BONGO NG'O.. HATA NIKIRUDI KUGOMBEA URAIS ETI NITAKUFA GHAFLA...THUBUTU

    ReplyDelete
  43. Mimi naomba sana nimjibu mdau wa London anayesema watanzania tunaogopa hela kubwa kubwa ndo maana tuko nyuma.
    Mimi nafikiri u need to think before u open ur mouth. Kwasababu vile ulivyoandika ni pumba kwa misingi ya kwamba kwanza unalinganisha viazi na njugu....pili kama umeenda shule basi hujaelimika. U think spending big money on something will implicate development not knowing the what will too much money do in the economy with zero production...

    Eti Singapore, angalia hizo nchi zinazalisha nini na kulipa vipi kabla ya kubwabwaja

    ReplyDelete
  44. Mwandishi nadhani kungekuwa na evidence japo ndogo tu ingesaidia zaidi kutoa hoja sahihi.. Kwa jinsi nyumba inavyoonekana nje sawa ni nzuri lakini sidhani kama ukarabati(sio ujenzi) unaweza kuwa wa gharama hiyo (1,000,000,000), labda ingeonekana na ndani...huenda kuna vifaa vya nguvu.... Kuandika tu figure na picha ya nje ya nyumba haitoshi kuwa kama ushahidi maana kwa macho yangu hapo nje sioni kama panaweza kuwa evidence ya billion 1 kutumika kwa kweli.

    ReplyDelete
  45. Jamani! jamani! Mbona mnaisakama sana hiyo billion 1. hebu niambieni Gavana wa Marekani au Uingereza nyumba anayoishi ni ya thamani gani? mlitaka Gavana wa Tanzania akaishi Manzese uwanja wa fisi?

    ReplyDelete
  46. Tatizo lenu ni umasikini mlio nao wa kutokujua na kutokufahamu. Hiyo nyumba siyo ya Beno Ndulu binafsi. Ni nyumba ya Gavana wa BOT ambaye kwa sasa ni Beno Ndulu. Akija mwingine ataingia. Ukarabati huo umefanyika kufuatana na bajeti iliyopitishwa sasa mnalalamika na kushangaa nini. Hiyo Bilioni 1? Kama iko ndani ya bajeti iliyopitishwa so be it. A billion figure is just a relative figure. Kama huna waiona nyingi na kama unazo kama vile BOT it is just an expendable item. Of course ukilinganisha na nyumba yako binafsi ndiyo unahisi kuna ufisadi. Lakini haya majumba yote ya serikali ya mashirika ya umma yanajengwa through tendering process na wanapewa contaractors. Hapo ndipo gharama zinakuwa kubwa. Kwa sababu kuna Main Contractor, Consulting Engineer, Electrical Consultant, Quantity Surveyor na kadhalika. Wote hawa wanatakiwa kulipwa professional fees kufuatana na sheria ya nchi. Sasa ukayajumlisha haya pamoja na gharama za vifaa vya ujenzi utakuta hiyo bilioni moja na kajisenti tu. Kwa hiyo acheni ushabiki wa watu wasioenda shule.

    ReplyDelete
  47. Nadhani wachangiaji wanakosa point. Ni vema kabla hujaanza kupiga kelele kwamba pesa ni nyingi ni vema mkaomba mchanganuo ili mpate hali halisi ilivyokuwa. Vinginevyo hakuna mwenye hoja yenye nguvu.

    ReplyDelete
  48. Michuzi asante kwa kutupa taarifa:

    1. Je hili ni jumba la Gavana wetu au jumba la serikali atakamoishi / anamoishi Gavana wetu?

    2. Je hizo fedha zimetumika kukarabati au kukarafati jumba hilo. Maana wakati ukarabati unafanya matengenezo, ukarafati unaweza bomoa na kubadili muundo kabisa na kutoa kitu kipya.

    3. Kama alivyouliza mdau mwingine, tujue pia samani na vifaa vyote vilivyo ndani ni vipi na vya aina gani maana kuna rafiki yangu juzi aliniambia kuwa amenunua 'akwariamu'- kitunza samaki cha ndani tu kwa thamani ya Ths. Millioni 7. Kisha tuonyeshe na uko uani kama kuwa bwawa n.k

    4. Mwisho tukumbushe kidogo, ni nani kwa mujibu wa muundo wa BOT mwenye mamlaka ya kuhidhinisha matumizi kama haya ya ukarabati au ujenzi wa nyumba za watumishi wake ili kama kuna uwajibikaji basi ndiye tuanze naye.

    Tafadhali hii isibinywe na pia tuwe tunajibiwa hapa ili blogu kuendelea kuwa ya maana katika kuelimishana.

    ReplyDelete
  49. Jamani naomba tusifungwe macho na vyombo vya habari,hivi hakuna sehemu nyingine wanapofuja hizi kodi zetu,huko kwenye barabara vipi,kwenye miradi ya kilimo,miradi ya Tasaf na mengi mengine,unajua tunaweza kukaa tunapiga kelele na hawa BoT kama vile kila kitu ndani ya nchi hii ni BoT,na kama anoy wa mwisho alivyosema kupata picha za nje ya jengo haitoshi kutuhumu mtu na je market price kwa sasa ikoje katika hili,na pia hizo nyumba za serikali kama hii kwani ikumbukwehii si nyumba yake huyo Gavana kama yeye zimejengwa au kukarabatiwa kwa kiasi gani kabla hatujaanza kulaumu maana unaweza kulaumu then baada ya kujua ukweli unabaki aah hatukujua,kwani ni kweli bilioni moja is sound much lakini tumewahi kuuliza kipande cha barabara ya rami kwa urefu wa kilomita moja ni kiasi gani kukijenga.Sitetei kama kuna ubadhilifu ila tusimame kwenye fairness maana huu wimbo wa BoT sasa is too much.

    ReplyDelete
  50. Michuzi naomba uitundike kwenye blog yako hii..

    Kuna jamaa mmoja toka huku Magharibi, aliamua kufanya Research yake kuhusiana na malipo/mishahara ya wafanyakazi wa Tanzania, na matumizi yao ya kawaida.

    Bali alipofika Tanzania, kama kawaida alikwenda kwenye hizi taasisi na kuangalia ni mishahara gani wanapata hawa wafanyakazi. Vile vile alifanya mahojiano nao, kuhusiana na mapato na matumizi.

    Bali kilichomchangaza NI MATUMIZI MAKUBWA KULIKO YALE MAPATO.

    Baada ya mwanko akakamilisha thesis yake, basi serikali ikamwita na ikamuomba atoe findings zake, jibu alilowapa akawaambia nitaitolea Kenya, serikali ikamuuliza kwa nini, akasema nitakupeni jibu lenu next week.

    Yule bwana, kinyemela nyemela akapakia ndege moja kwa moja mpaka Nairobi, akaitisha kikao na waandishi wa habari,

    Na hili ndio jibu na Finding zake akasema "WATANZANIA WOTE WIZI"


    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  51. According to Forbes magazine, as of 11 March 2009, he had a net worth of US$8.5 billion, ranking him as the 51st richest person in the world.[2] Prior to the financial crisis, he was considered to be the second richest person living within the United Kingdom.[3] Early in 2009, The Times estimated that due to the global economic crisis he has lost £3 billion from his £11.7 billion wealth.[4],sasa we figure umeitoa wapI? na usifananishe uk na bongo kiuchumi na wewe unaesema watu wanalipwa kiproffesional hakuna kitu kama hicho ni ujaNjaujanja wa kuongeza figure anyway WIIIIIIIIIZI MTUPUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  52. WE MDAU WA LONDON UKO LONDON AU LONDDON YA MAHENGE NA UNA INTERNET KWEL HAPO LONDON MAANA UNATOA FIGURE ZA UONGO AU NI MMOJA WA WAPAMBE WA MAFISAD WE UNACHEZA NA 52BILL POUNDS?HUYO ABRAMOVICH WAKO (November 4th, 2009. abramovich lunch receipt Roman Abramovichs $52,000 Lunch Bill‎ ... 51st wealthiest person, with a net worth of $8.5 billion dollars. ...HIYO NI US CONVERT KWENYE POUNDS)sasa hizo 45bills pounds kazitengeneza kwa mwezi au kachapisha? au mdau wa london ulichukulia hiyo BILL YA MSOSI ALIOLIPA?WE UKAJUA BILLIONS? jaman wizi bongo sijui utaisha lini

    ReplyDelete
  53. ....NA BADO.....!



    MDAU...LOBOKO LOBII PAPAA

    ReplyDelete
  54. kila mbuzi hula kufuatana na urefu wa kamba yake. hilo najua kila mtu analitambua! wasiwasi wangu ni pale wanaposhindana kati ya yule mbuzi aliyefungwa kamba ziro distance kutoka kwenye mti na yule aliekata kamba!!!

    NONDO

    ReplyDelete
  55. am sure imetumika more than Tsh; 1Billion... kwani wakati ukarabati uneendelea familia ilikaa wapi??? Humo humo ndani ya nyumba??? jibu ni hapana... kwa hiyo walikaa hotelini au walipangishiwa nyumba kwa muda... Je hizo gharama alilipa Gavana?? Jibu ni hapana...Jamani tutafika tunakokwenda????Kuna maswali ya kujibu baada ya maisha mzuri hapa duniani...rejea: maisha ya tajiri na Lazaro masikini kwenye Biblia!!!

    ReplyDelete
  56. nshimimana aka dumisaneDecember 24, 2009

    SIKUJUA KAMA ITAKUWA HIVI.

    ILA TUTAFIKA TU.

    = = =
    Buffalo, (nyumba hapa ni chini ya shillingi billioni moja za kitanzania)
    New York

    ReplyDelete
  57. Kwa umaskini wa Wawatanzania hii ni dhambi kubwa na nina uhakika hata shetani ameficha uso wake kwa aibu na mshangao iweje yeye aliyewafundisha uovu wanadamu wamemzidi kwa kutenda uovu. kwa wasomi wetu, hii ni aibu. Haiingii akilini kwa prof. mzima kuwafanya Watanzania majuha. Hakika haya hayatapita ifikie wakati tuwe na utu. Hivi Beno ni wa ngapi kwenye ukoo wako kama si familia wanateseka kwa kukosa hata lishe bora. ni kwa ufahari gani unaouona kuwa peponi na wakati umezungukwa na wenye dhiki. Yana mwisho na mwisho unakaribia hata kama wewe utakuwa umeiaga dunia, hili sekeseke unawaachia wanao. Akina Pinochet wako wapi. Ninayo mengi lakini naomba niishie hapa.

    ReplyDelete
  58. Mimi nimemwelewa mdau wa jijini London.

    Watanzania tunaona paudi 700,000 ni nyingi sana. Benki kubwa Tanzania ikipata faida ya mwaka ya paundi 700,000 wanapiga kelele nyingi wamefanya vizuri.

    Waziri mzima anatekeleza Sera ya kilimo Kwanza kwa jembe la mkono, badala ya trekta, pia tutamsifia.

    Hospitali za wilaya Temeke, Mwananyamala ikipigwa rangi na kugawiwa vyandarua tunajisifia kwa kelele nyingiii

    Kwa nini tusifikirie mapinduzi ya kimaendeleo makubwa makubwa mfano Mbagala, Chuo Kikuu, Wazo Hill n.k kusiwepo hospitali kubwa kama ya Muhimbili national hospital.

    Kiwanda cha jeshi Nyumbu kwanini kisizalishe makombora, mabehewa ya treni, matrekta n.k

    Viwanda vya sementi vizalishe simenti kwa wingi serikali ijenge barabara za zege kuunganisha mikoa yote Tanzania. Tutumie makaa ya mawe, jua na upepo kuongeza nguvu za umeme, tuzalishe nguo wenyewe kutokana na pamba yetu wenyewe n.k

    Tunatakiwa kufikiria mambo ya kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi kama ilivyokuwa USA ya 1950, USSR ya 1950 na China na India za 1990.

    Ndiyo inawezakana Tanzania ikawa na GDP kubwa kuliko kipato cha Benki ya HSBC(Hong Kong Shangai Banking Corporation)

    Mdau
    Mgodini Mchuchuma

    ReplyDelete
  59. Kweli masikini ni mwingi wa kutoa shukrani hata kama anaibiwa kiaina, soma dataz ya vijisenti.

    According to the Tanzania Chamber of Minerals and Energy (TCME), all mining firms have paid the government USD255,526,893 in taxes in the past ten years, that is USD 25,500,000 annually.

    Tanzania's GDP is estimated at USD10 billion, while the GDP per capita is USD280 and inequitable distribution of income and poverty are still prevalent.

    With tax holiday and capital allowances given by the 1991 generous mining Act, the government has not realized much in corporate tax and royalties which are at a lower rate of 2.7 per cent of net revenue.

    It is reported that despite these allowances the cumulative loss of the sector has been put at over 1trn/-. After recent negotiations with mining companies, some companies such as Barrick, have agreed to pay USD200,000 per year to three districts and the government is to get USD7 million annually paid to the Treasury.

    The Ministry of Energy and Minerals says that the sector has been using over 40 per cent of its revenue in local purchases.

    Tanzania, currently Africa's third largest producer of gold, claims a three per cent mining royalty for most minerals and five per cent for diamonds and gemstones.

    source: ippmedia.com

    ReplyDelete
  60. We mdau wa LONDON wakati unaandika comment ulikuwa umevuta bangi au maisha yanakuzingua london nani kakwambia kwa pound 700,000 upati nyumba uingereza au unatufanya wote wajinga hatujawahi kukaa london tatizo lenu nyie watu mkienda ulaya mnaleta ujuaji sana kana kwamba mnajua kila kitu kumpe pumba tu halafu usilinganishe uchumi wa nchi nyingine na tanzania kama wewe unafikiri kurenovate nyumba kwa shillingi billioni moja ni ujanja basi utakuwa mpumbavu wakati nchi tajiri duniani wanajitahidi kupunguza gharama za matumizi tanzania ndo kwanza tunatoa pesa kwa vitu ambavyo havina maana. ukienda mahospitalini hakuna kitu watu vijijini wanahangaika achilia mbali umeme na maji kupata madawa hospitalini shida.nafikiri watu wengi mnakaa DAR tu nakupiga soga wakati pande zingine za tanzania watu wanaishi katika umaskini wa haajabu jamani maendeleo siyo DAR tu BASIC NEEDS bado ni ishu kwa mtanzania. SASA nikiona wapumbavu wanatetea kukarabati nyumba kwa bilioni moja ni sawa nafikiri si jambo la kufurahia inasikitisha sana kwa jinsi watanzania walivyo wabinafsi. BAADHI ya watu huku ulaya wanajinyima angalau kusaidia AFRICA unakuta wazee hawana chochote lakini watakwambia wanachanga pesa kusaidia africa matokeo yake unasikia story kama hizi za utumiaji mbaya wa pesa.NYERERE JAMANI RUDI

    ReplyDelete
  61. wizi kwa watanzania limekuwa jambo la kawaida kama kenya na Nigeria. Ni ukarabati gani wa nyumba bongo una thamani zaidi ya dollar 850,000. kwa nza kabisa lazi tuelewe nani kapewa kandalasi, contractor, na ni vifaa gani vimenunuliwa na n vya aina gani. tumerudi kwenye enzi za mobutu kupata breakfast Paris on weekends.Lazima hawa viongozi wawajibishwe. huyu governor naye imekuaje akakubali kutia saini malipo kama hayo. please spend money wiselya and again stop buying expensive stuff to government officials. umaskini africa utaendelea iwapo viongozi wataendelea kuangalia matumbo yao.

    ReplyDelete
  62. Wewe mdau unaelinganisha Gavana wa Marekani na wa Tz, jee huyo Gavana wa Marekani aliwahi kuja kuomba msaada wa kufadhiliwa bajeti yake ya matumizi ya mwaka?

    Sisi kila mwaka lazima tutembeze bakuli ndio tuweze kutimiza matumizi ya serikali kwa mwaka, kwa hivo ni halali hizo fedha zitumike sawasawa. Vile vile hiyo tendering process kila stage inakuwa na 10% ukipiga jumla unapata 90%

    ReplyDelete
  63. HAHAHAHAHAHAHAHA BONGO TAMBARARE...WAJINGA NDIO WALIWAO..JIPENI MOYO TU HAPO BONGO LAKINI MIMI BOX SILIWACHI..CHAI YA MAZIWA NA MAYAI KILA ASUBUHI..BOX LINALIPA.....HAKUNA MALARIA WALA VUMBI...BOX LINALIPAAA...HAKUNA KUHONGA DAKTARI..BOX LINALIPAAA...HAKUNA NGOMA KAMA BONGO...BOX LINALIPA...HAKUNA UNYANYASAJI WA POLISI...BOX LINALIPAAA..BARABARA ZA LAMI...BOX LINALIPA..HAKUNA MGAO WA UMEME....BOX LINALIPA..HAHAHAHAHA SIRUDI BONGO HATA MALAIKA WAKISHUKA...BYEBEYEEEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  64. WEWE MDAU WA LONDON UNAYESEMA JE GAVANA WA USA AU UK ANAISHI KWENYE NYUMBA ILIYOKARABATIWA KWA BEI GANI.NAOMBA UELEWE KUWA HAO MAGAVANA WANAISHI KWENYE NYUMBA ZAO AMBAZO WAMENUNUA KWA MORTAGE NA HAKUNA UTARATIBU WA KUPEWA NYUMBA ZA SERIKALI KAMA KWENYE NCHI MASKINI KAMA TANZANIA,HIVYO NYUMBA ZAO ZIKIHARIBIKA AU ZIKIHITAJI MATENGENEZO NI JUU YAO WENYEWE, SERIKALI HAINA HABARI YENYEWE INAKULIPA MSHAHARA TU.HIYO NDIYO MAANA WENZETU WAPO MBALI KWANZA WAKISIKIA KUNA WATU WANAREKEBISHIWA NYUMBA NA SERIKALI WATASHANGAA KAMA SI KUCHEKA. TANZANIA TUNATAKIWA TUISHI NA TUWE NA MATUMIZI YANAYOLINGANA NA UWEZO WETU SIYO KUJILINGANISHA LINGANISHA NA NCHI TAJIRI.

    ReplyDelete
  65. NCHI INANUKA RUSHWA.LAAAAAAAANA.sirudi

    ReplyDelete
  66. SASA NIMEAMINI UKWELI UNAUMA NAJUA MAONI MENGINE NI KWA FAIDA YAKO NI MIMI TENA NILIYETOA MAONI KUHUSU "VIOLATION OF PRIVACY" KAMA MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI UNAELEWA MIPAKA YA KUTOA HABARI KATIKA PICHA, WEWE NI MCHONGANISHI KWA PICHA YA NYUMBA HII NA GHARAMA YAKE NI TOFAUTI KABISA MIMI NI MJENZI NA NINAFANYA SHUGHULI ZANGU USA KWA MAREKANI NYUMBA HIYO INAGHARIMU $MILIONI MOJA NA IKIJENGWA MPYA KUANZIA KWENYE FOUNDATION. KWA BONGO NI PUNGUFU YA HAPO TUKUBALI KWAMBA PESA UNAYOITAJA IMEJENGA NA NYUMBA NYINGINE KAMA HIYO ADDRESS HATUJUI. ILA NDUGU NINAKUONYA UTAJIINGIZA KWENYE CONFLIC OF INTEREST NA HAWA JAMAA NA ITAKULETEA MATATIZO BAADAE UWE MAKINI KWANI UMEMCHONGANISHA GAVANA NDULU ULIMWENGU MZIMA NA KIBAYA ZAIDI UMETOA MAELEZO KWAMBA HIYO NYUMBA IPO ENEO GANI KWA UGAIDI UNAOELENDELEA NI HATARI KWA USALAMA WAKE NA HUKUPASA KUIANIKA ADHARANI MAKAZI YA KIONGOZI MKUBWA WA NCHI! NI MIMI MDAU NILIOTOA MAONI KWENYE PICHA YA PROF. MARK KUHUSU KILIMO KWANZA THAT IS A BULL SHIT! EXCUSE ME FOR MY LANGUAGE. KILIMO CHA MIKONO WALA SIO MFANO WA KUIGWA NA WATANZANIA LABDA KAMA ANGEKUWA ANALIMA BUSTANI HAPO NINGEKUELEWA LAKINI KUTUAMBIA KWAMBA ANALIMA SHAMBA NA AMEAMKA ALFAJIRI NA MAPEMA KULIMA ARE YOU KIDDING ME BRO MITHUPU?
    HEY BRO. I LOVE YOU AS MY BROTHER BUT SOMETIMES YOU PISS ME OFF" BUT I UNDERSTAND BROTHERS FIGHTS SOMETIMES, NINGEKUWA KARIBU NINGEKUTAFUTA TUONGEE LAKINI NIPO MBALI ILA I BELIEVE ONE DAY I WILL MEET YOU BECAUSE I ADMIRE YOUR GREAT JOB! THIS IS YOUR CHRISTMASS. I WISH YOU ALL THE BEST ON YOUR HOLIDAYS
    NI MIMI MDAU WA DAMU WA BLOG YA JAMII. USA

    ReplyDelete
  67. Date::12/24/2009
    Gavana: Tumejenga nyumba mpya si ukarabati

    Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Benno Ndulu.

    Na Ramadhan Semtawa

    GAVANA wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu amekiri benki hiyo kutumia zaidi ya Sh1 bilioni za walipa kodi kwa ajili ya kutengeneza makazi yake.


    Prof Ndulu, ambaye alikuwa akitoa ufafanuzi wa habari iliyochapishwa na Mwananchi kuwa taasisi hiyo kuu ya fedha ilikarabati nyumba hiyo kwa Sh1.4 bilioni, alihusisha taarifa hizo za ubadhirifu huo wa fedha za walipa kodi na mtandao wa wafanyakazi wake ambao alisema una lengo la kumchafua.


    Lakini Ndulu alisema pamoja na kutokuwepo na usahihi kwenye taarifa kwamba nyumba anayoishi ilikarabatiwa kwa kiasi hicho cha fedha, makazi anayoishi yalijengwa upya baada ya nyumba zilizokuwepo awali kubomolewa na akadokeza kuwa gharama zinaweza kuwa kubwa zaidi.


    “Nyumba haijakarabatiwa, imejengwa from the ground (kutoka chini)... ni tofauti kukarabati na kujenga nyumba mpya huu ni upotoshaji wa wazi na kujaribu kuchafua mema,” alilalamika gavana huyo.


    “Napenda taarifa sahihi ambazo hazipotoshi ukweli, kwa maana taarifa kama hizo zinaharibu kila kitu kizuri na kujengwa taswira mbaya kwa wananchi, kitu ambacho si sahihi.


    “Pia si kweli kuhusu hizo gharama kwani hakuna tathmini kamili ambayo imekamilika hadi sasa.”


    Mwananchi iliripoti kuwa nyumba anayoishi sasa gavana huyo ilikarabatiwa kwa takriban Sh1.4 bilioni na kwamba zote zilikuwa kwenye mradi wa kukarabati nyumba za vigogo wanne wa BoT; ya Ndulu na manaibu wake watatu.


    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nyumba nyingine ni pamoja na aliyokuwa akiishi gavana wa zamani, marehemu Daudi Balali ambayo Prof Ndulu alidaiwa kuikataa kwa kuwa haina bwawa la kuogelea.


    “Nashangaa kuambiwa nimekataa kuhamia kwenye nyumba; kisa haina bwawa la kuogelea, huu ni upotoshaji. Kama ni kuogelea, mimi niliogelea hadi kwenye mito, sasa sijui hili linatoka wapi,” alihoji Profesa Ndulu.


    “Kwanza hiyo nyumba wanayosema ilikuwa kwa ajili ya kuishi mimi nikaikataa kwa sababu haina bwawa la kuogelea, ni uongo kwani ile alikuwa akiishi marehemu Ballali na ilikarabatiwa kwa ajili ya (Naibu Gavana Juma) Reli... sasa sijui mimi nimeingiaje,” alihoji.


    Akitoa ufafanuzi wa maeneo halisi ya nyumba hizo, Profesa Ndulu alisema makazi yake hayako karibu na katibu mkuu mstaafu wa CCM na kwamba anayeishi huko ni Naibu Gavana (Taasisi za Fedha na Mabenki) Rila Mkila.


    Alisema Naibu Gavana (Uchumi), Dk Enok Bukuku hajahamia kwenye nyumba yoyote ya BoT na kwamba anaishi kwake hadi sasa.


    Prof Ndulu, ambaye taasisi yake imelalamikiwa kwa kujiidhinishia mamilioni ya fedha za mikopo yenye tofauti kubwa ya viwango baina ya wafanyakazi wa chini na vigogo, alilalamika kuwa taarifa za ufujaji wa fedha katika ukarabati wa nyumba hizo zinamuweka katika kundi la mafisadi na kwamba ni mkakati wa mtandao huo alioutuhumu kuwa unaundwa na watumishi wa BoT na baadhi ya watu walio nje.


    Alidai kuwa miongoni mwa watu walio nje ambao wanaeneza sifa mbaya dhidi yake ni mwanasheria maarufu ambaye anadaiwa kutangaza vita naye baada ya kuzuia mianya ya ufisadi.


    Gavana Ndulu, ambaye aliteuliwa baada ya Balali kuachishwa kazi, alisema kamwe hatasita kutekeleza majukumu yake kwa ajili ya kufurahisha au kuhofu watu wenye dhamira ovu.


    “Najua, kuna watu wanafikiri watanitisha au kunikatisha tamaa. Nasema nitaendelea kushikilia uzi ule ule kusimamia sheria na taratibu katika kuongoza benki na si vinginevyo,” alisema.


    Alilalamika kuwa kuna watu wanataka kuzorotesha juhudi za kujengea nidhamu ndani ya taasisi hiyo na kwamba kwa dhamira zao wanaweza kukaa na kupotosha mambo kwa makusudi.

    Kuhusu tuhuma nyingine kwamba, viwanja hivyo vilinunuliwa, Ndulu alisema vyote vimekuwa mali ya BoT kwa muda mrefu na hakuna hata kimoja kilichonunuliwa karibuni.

    ReplyDelete
  68. PESA NDEFU HIYOOO.HAPO WAKATI WA MWALIMU VIBOKO TU 12-12 KWA WANAOKATA VIJISENTI VYAO.
    MDAU WA 'BOX LINALIPA'KANIFURAHISHA...KWELI LINALIPA.SIRUDI NG'OOO!

    ReplyDelete
  69. jamani nyerere tunaomba urudi

    ReplyDelete
  70. Michuzi umejua kuwasha moto.

    Sasa wadau watagoma kukukaribisha kwenye mabangaloo yao.

    (US Blogger)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...