KWA MUJIBU WA TAARIFA AMBAZO GLOBU YA JAMII IMEZIPATA NI KWAMBA SIMBA WA VITA HAYATI MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA ATAZIKWA SIKU YA JUMAMOSI HUKO NYUMBANI KWAKE MADALE WILAYA YA KINONDONI KWA HESHIMA ZOTE ZA KITAIFA.
VIONGOZI KADHAA WA NCHI ZA NJE WANATARAJIWA KUHUDHURIA MAZISHI YA SHUJAA HUYU AMBAYE ATAKUMBUKWA KWA UADILIFU WAKE NA KUJITOA MUHANGA KATIKA KUGOMBEA UHURU NA PIA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA. HABARI ZAIDI ZITAKUJA KADRI ZITAVYOPATIKANA
Si rahisi kudondosha chozi lakini kwa marehemu Rashid Mfaume Kawawa sikuweza kujizuia.
ReplyDeleteHii ndiyo ada ya kila mja.
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mpe pumziko jema na apate kikao chema katika matumaini mapya.
Amin!
mithupu inatia faraja kumuona mama salma kikwete akijichanganya na wafiwa hapo.pamoja na adamu malima na mbunge wa mafia.
ReplyDeleteTunatoa pole kwa familia yake na Watanzania wote kwa kifo cha huyu mzee wetu shujaa.
ReplyDeleteFaraja kuu itokayo kwa Mola wetu iwe juu yetu sote wakati huu wa msiba.
"PUMZIKA MAHALI PEMA MZEE WETU"
ReplyDeleteMkuu wa blogu ya jamii kwa kidirisha cha "YOU TUBE" umetuweka karibu na msafara wa msiba wa baba na babu wa Taifa letu.
Mwenyenzi Mungu amlaze mahali pema.
Mickey Jones-Denmark
Inna Lillahi wa Inna Ilaihi Raajiun.
ReplyDeletePoleni sana wana familia,mwenyezi Mungu awajaalie subra.
Ameen!
(US Blogger)
Jamani najua tuna uchungu...lakini mbona hakuna utaratibu hapo? sasa nani anafanya nini?
ReplyDelete