anko alipita hapa mwaka 2004 kama inavyoonesha..
anko akiwa na sanamu ya makinuka, mdada aliekimbia nyumbani baada ya kupewa ujauzito akiwa nyumbani. nia yake ilikuwa ajirushe kwenye maporomoko ya kinukamori ili kifo kimuepushe na adhabu ya ukoo wake, ila akasita. lakini alipogeuka na kutaka kurejea nyumbani kutubu, akakumbana uso kwa uso na chui. akataharuki na katika kustuka huko akajikuta anaanguka na kutumbukia kwenye maporomoko. huo ukawa ndio mwisho wa uhai wake. inasemekana adhabu ambayo angeipata yeye na huyo aliyempa mimba ni kutobolewa kwa jiti kubwa kupitia mgongoni kwa aliye juu na kutokea kwa aliye chini wakati wamefungwa kamba wakiwa wamekumbatiana. kisa hiki ambacho inasemekana ni cha kweli ni mojawapo ya vivutio vikubwa hapo kinukamori falls
chui akimnyemelea makinuka...

watalii wa nje na wa ndani hufurika kinukamori. hawa ni vijana toka moshi mjini

anko akipozi na wadau aliowakuta wakitalii maporomoko ya kinukamori falls. kule juu ndiko aliko makinuka akijiandaa kujirusha. hakika mandhari ya hapa utaikuta ndotoni tu...

njia ya kuelekea kwenye maporomoko

sanamu zikonesha hatua mbalimbali za kimila za kichagga

huyu binti katolewa kama kafara ya kuzikwa hai na chifu ambaye amekufa ikiwa ni mojawapo ya mila za enzi hizo za kichaga. msichana alitakiwa awe bikra na asiyetoga ama kukeketwa

majina mbalimbali ya kichagga kwenye ukumbi wa historia ya wachagga katika Kinukamori Falls ambayo iko kilomita kama moja hivi toka stendi ya Marangu Mtoni na ipo wazi kila siku









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. ka michu angalia bwana hayo mambo ya kukumbatia sanamu hilo wifi asije kukutenda muulize mwenzio tiger woods yaliyomkuta tetete

    afu vipi raisi wetu mwinyi mbona humweki tumuone manake ni watu ambao hatuwaoni sana humu hata mkapa hebu leta news zao manake hii ndio cnn yetu ya BONGO.

    good job michuzi

    ReplyDelete
  2. afu mdau ni nini? manake naona unalisema sana hilo mdau, wadau na mpaka shati lako limeandikwa mdau hebu tueleze kwa kirefu..

    wadau, north america

    ReplyDelete
  3. mbony tsapho?

    ReplyDelete
  4. jamnani mimi naitwa Anitha Lyimo, natokea marangu kilema mkyashi, sijawahi kujua kwetu kuna vitu vizuri hivi, kwakweli michuzi tunashukuru, umeniwezesha kulijua hili, and have to go tukienda kuhesabiwa xmas.

    ReplyDelete
  5. very interesting story michu nina asili ya kichanga lakini sijafika huko, decemba hii lazima niende

    ReplyDelete
  6. wadau north america

    Mdau maana yake ni shabiki ndio maana michuzi amevaa mdau no 1, yaani shabiki numba moja wa globu ya jamii ni michuzi, no 2 mimi mashughuli halafu tatu jipe mwenyewe nimejaribu kumsaidia michuzi kwani najau yuko busy na kama nimekosea ruksa kunikosoa

    ReplyDelete
  7. Good Job Michuzi...
    Zidi kutupa vivutio vya Tanzania... Libeneke Aluta Continua...!

    Mithupu is zis ur new fulanazzz??!

    ReplyDelete
  8. Kwa wewe unayeuliza mdau ni nini?Mimi nachukulia kama mteja wa kitu flani,,kwani udau wetu na michuzi ni kupitia hii blog yake tunayochangia kwa kuijenga na kuiimalisha mala kwa mala.Mdau mwingine atusaidie kidogo kwa hili.

    ReplyDelete
  9. The Kinukamori cultural site is good for Chagga culture but seems the site is not well managed. The script board is spoiled by bird droppings and the leopard sculpture is deteriorating. Someone should make donation during Ximass visit for management

    ReplyDelete
  10. hii picha ya mwisho imenshtua kwakweli,vp mr michu jicho ilo??

    asante kwa fulanazzz la mdau #1

    ReplyDelete
  11. michuzi unapendelea sana kwa wakwe zako huko kila siku moshi na arusha mbona kilwa kwetu vipo hivi sijasikia ukienda sijui tumekukosea nini sisi na barabara siku hizi ni ka huko marangu na hai pls michuzi tunakumbo na sisi uende kwetu tumewachoka wachagga humu ndani ukabila mbaka kwenye blog

    ReplyDelete
  12. Michuzi hii sii mila ya kichaga bali ni mila za wa Marangu ,hakuna kitu collectively kinachoitwa wachagga. Wachagga wana mila mbali mbali na lugha zaidi ya thelathini , kwa hiyo hiko kitu hapo ni cha wamarangu

    ReplyDelete
  13. mbunge wa tegeta wananchi wako tunateseka na foleni za magari yatoka Bagamoyo mpaka mwenge?tumekuwa watu wa kuamuka usiku sana na kurudi usiku sana ili kukwepa folen.je umemshauri nini RAIS wetu kuusu barabara hiyo ili 2010 tuwarudishe madaraka nyote wawili?

    ReplyDelete
  14. Tembelea na Tabora, Mbeya, Mtwara, Sumbawanga, Songea n.k

    ReplyDelete
  15. Haya jamani, hizo ndo mila za kiafrika tunazodai zidumishwe. Chifu akifa mpatieni kigori bikira azikwe naye (yaani machifu wenyewe wanajua kuwa kutahiri si dili kwenye mavitus).

    Haya jamani tusifuate mila za kimagharibi wakati za kwetu tunazo.

    ReplyDelete
  16. Kazi nzuri sana Mithupu. Ila nina swali la kizushi wadau, kama huyo msichana alijirusha kwenye hayo maporomoko nani alitoa hiyo habari? Maana inaonekana ilikuwa ni msichana na chui, unless palikuwa na mtu mwingine aliyekuwa ana-osbserve huo mtanange.....anyone out there with an answer pls. Maana hii habari imekaa ki-mitego mitego sana.

    ReplyDelete
  17. jamani mbona mdau wa mwisho una kawivu hivyoooo lol!basi kaka mithupi nendaga na kwao maana mh...! thanx kwa kuona mila za kwetu marangu!

    ReplyDelete
  18. Halafu hapo Kinukamori kuna story ambayo ni ya miaka mingi iliandikwa na Michuzi kwa nini usitumegee (niliona cutting ya hiyo story imebandikwa kaka Michuzi)

    ReplyDelete
  19. kak michuzi vp mbona mkono mfukoni katika picha ya bint huyo wa kichaga

    ReplyDelete
  20. Ukweli wa hiyo story ya binti wa kichaga kutaka kujirusha na hatimae kughairi na kutaka kurudi nyumbani na kukutana na chui amabae alimfanya arudi tena kujirusha kwenye maporomoko hayo na kufa ina utata kuliko hata habari ya babu Seya na wanae. Ina maana kuna mtu alikuwa akishuhudia hayo yote huko kwenye maporomoko na akaja baadae kueleza ilivyotokea au? Mimi siamini hiyo stori

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...