mtarajiwa wakati wa chiken party akiwa na vazi la SmartAfrika la Manju Msita
mtarajiwa na mpambe wake wakati wa send off katika mavazi ya SmartAfrika
mavazi ya SmartAfrika hayaongopi
mtarajiwa na mpambwe wake wakati wa send off
watarajiwa katika send off ndani ya kivazi cha SmartAfrika
wakikata keki wakiwa katika mavazi ya SmartAfrika
wakiingia kanisani
tofauti ni kubwa sana dhidi ya mavazi ya magharibi
alipoamua kustaafu muziki baada ya libeneke la muda mrefu akiwa na Roots & Kulture akiwa na Jah Kimbute, Manju Msita amejikita kikamilifu kwenye ubunifu wa mavazi ya Afrika na sasa yuko katika harakati ya kuleta mabadiliko kwenye mavazi ya wakati wa sherehe kama vile harusi, send off na chicken party. vile vile anawashonea mavazi ya Afrika mastaa wakubwa wakiwemo banana zahir ali, mrisho mpoto na kadhalika. hapa anatumia kompyuta kuhifadhi ubunifu wake na pia kuwasiliana na wadau kwa njia ya kisasa. libeneke lake linaadaliwa pamoja na ripoti kamili. manju, ambaye anatamba na lebo yake ya SmartAfrika, anapatikana Mikono House kona ya Chang'ombe kabla ya VETA jijini Dar. email yake ni manjumsita@yahoo.com na namba ya simu ya ofisini kwake ni +255 655 411 411/ +255 784 411 411











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. 'Big up' Manju tuondolee huo ukoloni mamboleo wa kuiga kila kitu cha Magharibi..huwa wanatushangaa sana tukifanya harusi za magharibi, mavavi nk.

    ReplyDelete
  2. Tatizo hizi nguo ni kama costume , utadhani wako kwenye theatre , kwa kweli sioni kama wamependeza utadhani wanafanya a freak show .

    Angalia hiyo nguo ya sendoff haswa pale inapo buruza utadhani sijui mkia wa nini, ni nguo za kama mtu anafanya imagination , haswa kama vile wamakonde wanavyo chonga zile vyinyago, .

    Hakuna kupendeza hapa, nadhani wabuni nguo zinazo onekana zina valika kuliko kuonekana kama vile wako kwnye fashion show kwenye kipengele cha ubunifu wa hisia.

    ReplyDelete
  3. Vipi Jah Kimbute hivi kaka yako David yupo wapi siku hizi? Mara ya mwisho nilisikia yupo Marekani, mimi nimesoma naye Tanga tulikuwa tunamtania Mzee wa NONDO ama Cheff. Mpe hi nyingi tu mimi niko INDIA

    ReplyDelete
  4. Manju Msita HONGERA sana kwa ubunifu wa hali ya juu. Hii ni njia mojawapo ya ukombozi kutoka makucha kama sio kasumba ya mabeberu wa kiutamaduni (ubeberu ambao huwa umefungamana na ubeberu wa kiuchumi). Sasa nina imani kwa mtaji huu tunaweza hatu kupata suti ya kiafrika inayoshindana na suti ya ulaya. huu ndio ubunifu tunaopigia kelele. nikija bongo nitakutembelea. keep up!!

    ReplyDelete
  5. Wewe unaesema nguo kama wko kwenye theatre pole sana. Tatizo ni kwamba nguo za kizalendo unafikiri ni special kwa sanaa tu, kumbe si hivyo. Badilisha mtazamo hapo awali wengi walichotwa na utamaduni wa wageni siku hizi watu wameshtukia dili kila mtu anathamini cha kwao. Tuondokane na utumwa. MANJU KANDAMIZA KWA SANA WATU WAAMKE. GOODLUCK!!!!

    ReplyDelete
  6. Hi Manju,kuna marekebisho ya hapa na pale ktk nguo zako lakini mbali na hayo kazi nzuri na hata nia yako kama tulivyosoma hapo juu ni nzuri,tafadhali tilia mkazo.
    Kila la heri.
    Mdau Palm Beach,Dar.

    ReplyDelete
  7. kaka michuzi ur spelling inasikitisha is it chicken party ama kitchen party?

    ReplyDelete
  8. Mi sina tatizo na mavazi, ila nina tatizo pale mtu anaposema haya ndio mavazi ya utamaduni wetu. Suruali na 'shati' si utamaduni wetu, kama mnataka mavazi ya utamaduni wetu, turudi nyuma hadi kabla ya ujio wa wageni wa Kizungu na Kiarabu, tuangalie tulikuwa tunavaa nini.. hapo itakuwa sawa. Au?

    ReplyDelete
  9. Hizi ni nguo za kimagharibi ila zina urembo au nakshi za kiAfrika, sasa tubunie zile za kiafrika kama vibwaya, migolole n.k

    ReplyDelete
  10. safi sana
    love it
    nyie haters hapo juu manaosema hawajapendeza acheni hizo, na wewe vaa ya kwako halafu post hapa tukuone, nyooo

    maharusi mmependeza sana msiwasikilize wenye wivu

    peace
    mdau
    Canada

    ReplyDelete
  11. TRULY SOUTH AFRICAN.

    ReplyDelete
  12. Yaani ni nzuri mno, hongera sana kaka haswaaa hizo mavazi ya harusi.

    ReplyDelete
  13. Nilikuwepo kwenye send off ni kitu tofauti na ilipendaza. Lol. Lolah

    ReplyDelete
  14. designs zako nzuri sana kaka, ila kuna siku nilikuja hapo kwa ajili ya nguo ya kitchen party kwakweli CUSTOMER SERVICE yako ni MBOVU! rekebisha hilo mambo yatakuwa safi.

    ReplyDelete
  15. khaaa wee annon 09;43;00am

    hahahaaaa mboni ndo ugonjwa wetu,no mtz ana customer service zuri

    ReplyDelete
  16. Big Up Manju

    Love your work. Mteja sugu lol

    ReplyDelete
  17. Kwakweli nimekubari kuhusu hayo mavazi mnayoyabuni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...