Home
Unlabelled
libeneke la wananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
bro mithupu hii tovuti tumeshauliza maswali kibao lakini cha ajabu hayajibiwi sasa sijui ina kwikwi gani au ndio kama kawaida yao kufungua tovuti ila inakuwa haipo updated!inasikitisha sana maana kila nikiingia naambiwa hoja yako inashughulikiwa mpaka sasa ni mwezi na nusu hoja inashughulikiwa nahisi wahusika waliifungua tu kisha wakaingia mitini!
ReplyDeleteWakiishughulikia hoja yako kupitia kwenye mtandao watapataje pesa za RUSHWA? Eeh hebu nambieni watapataje kitu kidogo, mbali na hiyo watajioneshaje kwako kuwa wao kwa muda huo wewe una matatizo lazima uwasujudie kwa ndio miungu wako?
ReplyDeleteMimi nimeshauliza maswali humo, nimekata rufaa, na kila kinachowezekana ndani ya hiyo tovuti lakini ni zaidi ya mwaka sasa hakuna majibu yoyote niliyopata. Mwisho nilipoenda kuwaona wahusika live, walibaki wakinirusha dana dana, nenda huko nenda kule. hundi yangu ya mirathi imesainiwa hazina tangu Desemba 2007 imepelekwa mahakamani mpaka leo December 2009 inaishia sijaipata. Kila siku faili halionekani, wakae nayo tu mwaka watakaojisikia kunilipa watanilipa kwani haki ya mtu haipotei inacheleweshwa tu.
Wadau wala msijisumbue kutumia hiyo tovuti haina admin, ndio maana haina majibu. Na kama yupo na ndiye aliyepost hilo tangazo baana ya kuona anakaa bure watu hwaitumii hiyo tovuti yake atujibu humu kwenye blogu ya jamii, kazi ya hiyo tovuti ni nini???
hiyo ni campaign tu, kama ni tovuti ya wananchi mbona ina picha ya kikwete?
ReplyDeletezuga tupu! tumeshazoea kupigwa mchanga wa macho, hatuna noma sisi.iwepo isiwepo sawa tu.
The whole thing is bullshit. These guys know that the election is about and now they want to fool people. Hey! can you stop thinking that all Tanzanian people are damn. The government leaders are foolish as they think we’re blind not to see what shit they are doing toward people of TZ. If you are not ready to serve people of Tanzania stop fooling us and go back where you come from. This is madness. Stop it. Almost 98% of Tz leaders they don’t know how to use computer how can they manager this site?
ReplyDeleteHIZI NI PROPAGANDA WATU KIJIANDA NAA UCHAGUZI PRETTY SOON.INASIKITISHA,RAISI AMESHINDWA KUFANYA KAZI,NASHAURI AACHIE NGAZI TU.
ReplyDeleteMimi nafikiri hiki ni kiini macho, Mh. Rais alizindua mtandao huu kwa mbwembwe na akaukikishia umma kuwa watu watakuwa wanajibiwa maswali yao kila waulizapo lakini angalia niliuliza swaali kwenda Wizara ya mambo ya ndani lakini miezi sita sasa lakini sijai kupata majibu
ReplyDeleteIlikuwa ni njia nzuri ya ku-interact na wananchi kujua kero lakini ndo hivyo haikufanya kazi.
nakubaliana na wadau hapo juu,kuwa tanzania imezoea mambo ya viini macho wengine wanaita mchanga wa macho,wakusema maneno kisha vitendo ni sifuri.
ReplyDeletemimi nilidhania nikomwenyewe naye kuta jibu tena kiswahili chake sio sahihi"HOJA YAKO LINASHUGULIKIWA".
swala lenyewe ni juu ya wanavyuo walioko moscow nchini urusi wapatao 15 ambao hadi sasa hawajatumiwa fedha licha ya ubalozi kusaidia kufuatilia ktk bodi ya mikopo,mara bodi idanganye kwamba imetuma fedha kwa watu hao,lakini kati yao wakiamua kufuatilia kwa kutumia ndugu zao walioko karibu na watendaji wa bodi basi fedha inatumwa maramoja wanapata,wakati akina yakhe wanaendelea kula msoto.
sasa hadi serikali inadanganya badala ya kusema kinachoendelea,je wananchi wake wataiamini vipi???
hebu tutoleeni u-%$£28*9# wenu. matatizo ya wananchi kwani hamyaoni hadi muyatake kwa kupitia mtandao. kazi mmeshindwa kuachia nchi wengine waongoze hamtaki kwendeni zenu huko. ndo mana mi ntajibebea box langu kwa bibi hapa wee hadi nakufa, manake mi si raia lakini bibi ananijali kuliko nyie mnavyowajali raia hapo nyumbani
ReplyDeletekulikoni kuutumia huo mtandao kiini macho wa SIRIKALI nibora kuitumia hii blog ya ankal maana utapata jibu ndani ya siku moja au dakika kadhaa au masaa kadhaa:)))
ReplyDeletetunafahamu serikali yetu watu maofisini wengi huenda kupoteza muda wakisubiri muda ufike waondoke tu,nani anamuda wa kushughulikia matatizo ya mtu? matatizo yan watu yanashughulikiwa ktk nchi zingine sio tanzania bwana,tanzania kiswahili kirefu na chenga za mwili nyingi hadi mkono uingie mfukoni ndipo utashugulikiwa au vinginevyo basi undugu na urafiki utumike na sio haki yako kama mwananchi kushughulikiwa,kupewa feedback ya nini kinaendelea na kupewa maximum time ya wewe kusubiri hadi kuwa umeshugulikiwa. hayo wenzetu wanayo sisi sijui tena hilo pia linahitaji.....kama kawaida yetu"sisi ni maskini" yes maskini wa fikra (((:
niliona mfano eti kushughulikia vyeti vya kuzaliwa huko songea,serikali inamtuma mtu anakaa nje ya kituo mwezi mzima huku wanasema tatizo ni picha haziwezi kupigwa. sasa kama sio umaskini wa kufikiri,inamaana serikali inashindwa kununua digital camera,pikipiki,lap top na portable printer kisha imkabidhi mtu mmoja tu kazi hiyo ya kusajiri vyeti kwa mkoa mzima mbona ningeifanya kwa mwezi mmoja tu!!lakini cha ajabu utakuta jambo kama hilo linachukua mwaka au zaidi,na fedha watakayolipwa watumishi kwa kukaa nje ya vituo wakifanya kazi hiyo itakuwa ni x30 ya gharama ambayo ingenunua vitendea kazi hivyo na ku-shorten time.matokeo yake kuna watu watakosa mambo muhimu kwa kutokuwa na vyeti hivyo hadi mwaka uishe((( oops!!serikali makini!!!
FUNGUENI NA CHAT ENGINE ILI TUWE TUNA WASILISHA HOJA ONLINE NA TUWE TUNA CALL PC to PC ILI TUSIDANGANYWE NA AUTOMATED ANSWERING PROGRAM. IKIBIDI MFUNGUE ADRESS ZA ONLINE CHAT KUPITIA MITANDAO MINGINE KAMA YAHOO,HOTMAIL MSN MESSENGER,SKYPE n.k kama kweli lengo ni kurahisisha kushugulikia matatizo yetu wananchi.maana hapo jibu nitalipata hapo hapo na nikiahidiwa najua pia nitajibiwa live hatua gani imefikiwa.lakini sio hii peke yake ya kusubiri miezi nenda na kukuta jibu la unashugulikiwa .
ReplyDeletebado naona kuwa huu ni mwanzo muafaka wa wananchi kuwasiliana na serikali yao, ingawa bado kuna kusua sua katika serikali kujibu. mara zote tulikuwa wala hatuna mlango wa kuwasiliana, huu umefunguka, ingawa majibu hayatoki, nitaratibu haya mambo, mtoto hazaliwi na kutembea leo. na nyie watu wa serikali acheni siasa fanyeni kazi, na kama kazi hamuiwezi wapeni wengine nyie mjiuzulu, na wanasiasa wapige kazi ya siasa maana yaonekana nyie watu wa serikali mmekuwa watu wa kulala.
ReplyDeleteMungu Ibariki Tanzania.