Stars United f.c., inayoundwa na wabongon waishio Marekani, ina mipango ya kuvuka bahari mwezi july mwakani kuelekea Sweden kwa mechi ya kirafiki na timu za huko.
Stars united sasa inatafuta wachezaji wenye uwezo wa kucheza kabumbu wanaoishi Marekani na watakao kuwa tayari kusafiri na timu Sweden na timu itakua chini ya Kocha Juma Maswaya ambae ni kocha wa Houston(Serengeti Boys),tarehe bado haijapangwa lakini ni baada ya mashindano ya soka kombe la dunia kuisha,ambayo yanatarajiwa kumalizika july 11 2010.

Tutakuwa na mechi za kujipima nguvu na timu za mataifa mengine,kuanzia april mwakani,na timu inatarajia kupiga kambi ya pamoja wiki mbili kabla ya kuelekea Sweden,uongozi utawaomba wachezaji watakao kuwa tayari kusafiri kuomba likizo kwa mwajiri wao wakati mmoja ili kuweza kupiga kambi ya pamoja kwa safari hiyo,kwa sasa gharama za usafiri,chakula na malazi ni juu ya mchezaji,lakini mipango bado inafanywa kupata mfadhili atakae punguza au kuondoa makali ya safari kwa wachezaji,timu inatarajiwa kusafiri na wachezaji 16, daktari na kocha.

Kwa mchezaji wa soka Mtanzania anaeishi Marekani mwenye uwezo wa kucheza soka na yupo tayari kusafiri na timu tafadhali wasiliana na Stars United kwa barua pepe starsunited@live.com na uweke jina kamili,state unayoishi na # ya simu utakayo patikana kwa urahisi.

Kama washabiki watakaopenda kusafiri na timu kwa kujigharamia wenyewe wanakaribishwa kwa mikono miwili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. hakuna tabu nyie lipeni nauli pa kulala huku sisi watanzania wenzeni tupo nadhani sio tatizo,zaidi ingieni kilimanjaroclub.com na mtapata namba za wakubwa muwasiliane nao

    ReplyDelete
  2. hivi kwanini wachezaji wa mbele wabong'oe katika picha za pamoja kwanini wasichuchumae....

    ReplyDelete
  3. Timu haina website ?. Mechi ngapi zitachezwa timu ikiwa Sweden ?

    ReplyDelete
  4. Wenye makaratasi ya kutoka hawazidi 8, watasafiri vipi?

    ReplyDelete
  5. Tusio na makaratasi mtatusaidiaje kutoka na kuingia Marekani?

    ReplyDelete
  6. wabongo kwa mbwembwe na misifa!!!ktk hiyo pix wenye makaratasi hawazidi watano(5) sasa mtasafiri vp nje ya USA na kurudi??haha kaaazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  7. pepa mwanangu..hapo ndipo soksi itatoka na kiatu kubaki.

    ReplyDelete
  8. NINYI SASA MNATAKA WATU WAKAOZEE SWEDEN KWANI ISSUE YA PAPERS NI KUBWA,SIZANI KAMA KUNA MTU ATA-RISK KUSAFIRI AKIJUA HIYO NDO BABA JENI BYE-BYE KURUDI STATES

    ReplyDelete
  9. hii ndio website ya timu www.starsunitedfc.webs.com kama kuna swali au maoni yoyote tafadhali ingia kwenye site. Bila kusahau unaweza kujiunga nasi kupata news zaidi.

    ReplyDelete
  10. ..mchezaji hapo ni mwanangu TIFU"peke yake(mwenye dreds.wa pili toka kushoto).kinondoni shamba represent...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...