Ina Sitting room,dinning room na kitchen vyote vya kisasa..
Vyoo na bafu za kisasa na heater.maji ya bomba na reserve tanks.
Bei ni Dola za Kimarekani 150,000 au shilingi milioni 200 za ki-Tanzania
kwa maelezo zaidi piga simu namba
+255 655 303 997
au andika barua pepe
...good stuff...
ReplyDeletecrib iko bomba na bei reasonable
ReplyDeleteMBEBA BOX
Nafikiri kabla ya kukurupuka na kuanza kutangaza bei za nyumba ambazo si practical tujifunze jinsi biashara za nyumba zinavyofanyakazi. Kitu kikubwa ni location, nyumba kama hiyo ukiipeleka Kigoma huwezi kuiuza hata kwa million 15, ila ukiihamishia Oysterbay inafika mpaka milioni 500, na ukiipeleka Tandika basi hata milioni hamsini mtu atakulilia hali sana tu. Hebu tujiulize TEGETA kuna status gani? kwa nyumba kama hii kuuzwa Million 200?. Huyu kama ni muuzaji aachane na madalali aangalie hali halisi ya bei ya nyumba. Mimi ninatafuta nyumba ila kwa bei ya Jamaa kwa Tegeta sio realistic kwa nyumba hii.
ReplyDeleteTujifunze kidogo hapa chini kwenye masuala ya property markets,
1. What is Hedonic Pricing?
A model identifying price factors according to the premise that price is determined both by internal characteristics of the good being sold and external factors affecting it.
Using hedonic Pricing,
The price of a property (residential or commercial) is determined by:-
(a)The characteristics of the house (size, appearance, features, condition) and
(b)The characteristics of the surrounding neighborhood (accessibility to schools and shopping, level of water and value of other homes, etc.)
So lets don't let the clueless brokers who always focusing on 1% commission of the price determine the price of a house. Kama wewe ni muuzaji masuala ya kujiuliza ni haya
1. Kiwanja umenunua kwa Shs ngapi? (Kwa eneo hilo sidhani kama inazidi 10M)
2. Gharama za ujenzi ulizoingia, kwa nyumba hiyo(plus ukitumia vifaa vya China) sidhani kama inazidi 30M, then plus 10% profit nyumba hiyo haitakiwi kuuzwa kwa zaidi Shs 60M kama wewe ni muuzaji kwa bei ya kuanzi lets say $65,000. Hapo utapata wanunuzi. Maana kipindi cha EPA kimepita sasa watu wana hela walizozitolea jasho, bei ni kubwa mno my friend
Wajanja tunajua kuwa imewekwa na bei kamili ili tupimishe na ile ya Gavana! Kwikwi!
ReplyDeleteKwa nje inaonekana ni nzuri, 2oneshe na kwa ndani maana ctaki kuuziwa mbuzi ktk gunia. N,way fahari ya macho haifirisi duka...Kigogo Boiiii
ReplyDeleteKwakweli nyumba ni nzuri, tupe picha za ndani basi.
ReplyDeleteKwa muonekano wa nje tu nyumba ni nzuri hakuna ubishi,ila kama bei za nyumba bongo ndivyo zilivyo basi hakuna haja ya kushangaa nyumba ya Gavana kujengwa kwa 1Bln.
ReplyDeletejamani nyumba ni ndani pia!!mbona unaonyesha njee tuu?
ReplyDeleteKajumba hako ni kazuri na bei yake ni poa kabisa kwa bai hiyo ninakubaliana kwa wadau wenye pesa hivyo ni nyumba ya kuchangamkia hiyo ni bei ya bure kabisa.
ReplyDeleteMdau anaedai yeye ana Property Market expertise inaonekana hujaenda bongo muda mrefu sana, nenda ukajaribu kujenga kule ndio utajua bei halisi za bidhaa. Kiwanja siku hizi maeneo kama hayo ni zaidi ya bei uliyotaja hapo juu. Google search yako inakusaidia lakini sio practical katika uchumi kama wa bongo, remember bongo hakuna market competition kama za nje, pia watu hawataki usumbufu wa ku-deal na mafundi au contractors. My advise ni kwamba nenda bongo uone then ndio utoe comments zako.
ReplyDeleteNakubaliana na Property Market Expert.
ReplyDelete200m is excessive!!
This is second time I see this ad, i can tell frankly, the owner will struggle to get that.
Neighbors not developed you don't know what is gonna come up, why gambling??
Tusipange bei kiswahili expecting kwamba atakayekuja atajigonga kwa kuanza na say half and then aka-end up na 150m, no way!!
I don't see 200m in that house, ni bora hata asingeweka bei - be fair bro.
Property Market Expert huonekani kama unauzoefu wowote katika masuala ya ujenzi wa nyumba Tanzania, otherwise usingesema gharama za kujenga nyumba hiyo ni milioni 30, sielewi hiyo nyumba imejengwa vizuri kiasi gani na ndani imemalizwa ka hatua gani ila kwa mtizamo wa nje naweza kusema thamani yake inakaribia milioni 100 na muuzaji angeweka bei around milioni 150 nisingeshangaa.
ReplyDeleteUshauri wangu kwa mwenye nyumba kama hukueka kumbukumbu za gharama za ujenzi vizuri usije kuuza hiyo nyumba chini ya milioni 100 kwa tamaa utaweza kujenga nyengine na kupata faida, gharama za ujenzi zinapanda kwa kasi kubwa sana Tanzania.
Nawasilisha.
Huyu Propert Markert Expert wa wapi huyo!!
ReplyDeleteMie mzoefu wa hapa bongo nadhani ni fair kusema
-kiwanja ni kama 20mita by 30mita kwa Tegeta itakuwa 20 mil na kama kina hati ni 25 m
-fence, gate na external work ni around 15 m Tsh
-Nyumba kwa nini haonyeshi ndani ??? au kusema ina vyumba vingapi etc??? in any case hilo paa, grills aluminium etc nyumba pekee itakuwa minimum ya 70 mil
Hivyo my conclusion kama hakuna problem ya hati, umiliki, neighbour mkorofiii au kosa kubwa la kiufundi ndani ningemshuri tajiri yangu Masawee anunue kwa 110 m mpaka 130 m.
Naomba kuwasilisha!!
Ndugu zangu mlioko ughaibuni fanyeni hima mjenge home, maana viwanja bei aghali sana, tena sana kwa sasa, dar kariakoo sasa hivi numba inanunuliwa kwa milioni 700 had 800 na sometimes bilioni moja ili ivunjwe na kujengwa nyingine, Bunju wacha tegeta jirani na kwangu kuna kakiwanja kanauzwa milioni 60 na jamaa wamefila nilioni 55 mpaka jana, hii inamaana kwa nilioni 200 tena tegeta ni bei ya kutupwa am sure mapaka mida hii tuosha vinywa yaweza kua imesha uzwa, dar mlo iacha si hii ya leo, rudini ndugu zangu mjenge kupanga hamtaweza mkirudi mikocheni nyumba ya kupanga dola 2000 kwa mwezi mpaka 5000, sasa familia zenu mtaziweka wapi mkirudi au ndo mkapange wa mtogole kweli na nyie mmtoka majuu?? mbona itakua mabadiliko ya aghafla??
ReplyDeleteHuu ni ushauri tu
mzee wa buju
Nakukatalia Property Market Expert unayo yasema yana ukweli kiasi fulani lakini umeandaestmeti sana ile nyumba akiuza milion100 ni rizonable siyo M65, inaonyesha wewe bado upo shule hivyo nadhalia za vitabuni zimekukaa sana umesahau kwamba sehemu kubwa ya nadhalia haziaplai katika mazingira harisi hasa ya kiafrika, Inaonyesha kwanza hujawahi kufanya ujenzi. Kwasababu umeorodhesha magrupu mawili tu ya gharama za ujenzi nayo kwa kukosea bei, kuna vitu vingi umesahau kwa mfano unapo zungumzia kiwanja na vifaa tuu umeashumu ukivifikisha saiti basi yatosha. Mimi mwenyewe najenga Tegeta nyumba ya vyumba vi3 na masterbed room moja, bado hata sijahamia kuna vitu havijakamilika ikiwa ni pamoja na fensi umeme na maji
ReplyDeletei. Uwanja nilinunua Million 21(km2.5 kutoka Stendi) nimenunua mwaka jana sijui market price yake sasa. na hii ilitokana na mimi kuuza uwanja uliokuwa karibu na barabara kwa Million100 kwasasa pamejengwa kituo cha mafuta
ii.Vifaa vyote kuanzia mchanga mpaka kioo imenighalimu Million41 (Kama vipi nenda madukani kafanye windoshopingi ya baadhi ya vifaa vya finishing tuu)include na transport kwa nyakati tofautitofauti
ii. Leba chaji imegawanyika mafungu kibao kwasababu sikuajiri kampuni anzia kusafisha uwanja mpaka kufanya finishing kwa hesabu za harakaharaka naona jumla M11 imeondoka.
ii. Ghalama nyingine ambazo ni kubwa lakini hazijumlishwi kama vile air times, opotyunitikostz nk.
HIVYO PAMOJA NA FAIDA NYUMBA YANGU SIWEZI NIKAIUZA CHINI YA M100.
Nyumba kwa muonekano wa nje ipo safi.
ReplyDeleteMimi nahitaji nyumba kama hii lakini namuomba huyo muuzaji anijibu maswali yafuatayo
1.Kwanini ameamua kuuiza?
2.Je kiwanja ni halali?
3.Viwango vya ujezi uko vipi,Namaanisha je aliweka foundation ya uwiano gani?Tofali zake pia zinauwiano gani?
Pindi nipatapo majibu ya maswali haya ,ndipo tunaweza fanya biashara.
Namba +46735829472
Hii bei si kubwa sana. Ila sio rahisi kupata mtu mwenye hizo hela na ambaye yuko tayari kuinunua.
ReplyDeleteNyumba kujenga ni hela nyingi lakini inachukua muda kujenga hivyo mjenzi huwa hatakiwi kuwa na hela yote kwa mkupuo.
Wewe expert wa properties mchanganuo wako ni wa kwenye vitabu zaidi. Sasa kama kiwanja ni milion 10, nyumba itakuwaje milion 30?
ReplyDeleteSuala la bei na kubaliana na property market expert, bei ni kama mara nne ya gharama halisi ya ujenzi wa nyumba hiyo
ReplyDeletesuala la location siku hizi prpoerty developers huku UK wanasema "Forget location, location,the key to successfully building and selling new homes is presentation,presentation.Site presentation makes the difference" Luluzaan,UK
Anon wa Wed Dec 30, 09:10:00 AM wewe ndiyo muuzaji hasa unaingia kama anon kila baada ya moja (yaani 12.11Am, 1.24AM, 1.54AM, 2.50AM, 7.30AM, and 9.30AM) kwa post za kusifia nyumba wakati nyumba yenyewe ipo TEGETA, Ingekuwa Oysterbay au Mikocheni hiyo bei yako reasonable ila kwa TEGETA Umeenda mbali mno kwa bei hiyo
ReplyDeleteKwa taarifa yako mimi Bongo ni kama wewe unavyoenda kariakoo kila siku kuhemea. Hunidanganyi hata kwa chembe na unajua kuwa niliyoandika ndiyo hali halisi, Sema wewe kwa ufinyu wa uelewa wako unataka kuwaliza wabongo ambao wamejikusanyia vidola vyao na siku nyingi hawajafika bongo.
Inawezekana kweli Google inanisaidia ila kwa kujua kuwa Google inaweza nipatia nini ni dhahiri kuwa ninajua nilichokuwa nakitafuta google. Real estate market ni fani yangu niliyosomea na ninaifanyia kazi huku nilipo na Bongo vilevile, Nimeona niwataarifa watanzania wenzangu wajue kuwa Bongo usanii umezidi!. "CAVEAT EMPTOR"-Let the buyer beware.
"Michuzi" naona ankal umeleta kipande kingine cha malumbano ya nyumba. Naomba kujua market price za kiwanja na nyumba maeneo ya masaki au Oysterbay? Tunalalamikia kifaa cha mheshimiwa gavana kumbe kinaweza kuwa kinalingana na real value ya maeneo hayo. Kikubwa kwa mambo ya serikalini ni cha juu kwa watendaji
ReplyDeleteambacho kinapandisha gharama.
Hiyo nyumba ya ya Tegeta kama wachangiaji wengine waliotanguali wanaopinga, mimi naungana nao kupinga bei, 200ml kwa maeneo hayo bado ni kubwa...labda kama bei ya kuanzia. Ila ni vizuri kama mtu akaweza kutembelea eneo na kujua uimara wa mjengo.Nawakilisha!
mimi ninaomba nimjibu ndugu yangu property market expect.
ReplyDeleteto be honest with you unachozungumza nadhani kina make sense kwenye vitabu lakini sio reality kwenye ground.
mimi at the moment ninajenga nyumba ambayo ina vyumba vitatu.nimedocument kila kitu kwenye excel na mpaka sasa ninavyoandika hii msg kuna mafundi wanahangaika kuweka makabati jikoni, rangi ,kufunga simtank kwa ajili ya maji.bado umeme na sijaweka paving blocks kama za hiyo nyumba hapo juuu.na ninachokwambia mpaka sasa nimeshatumia FEDHA HALALI ZA KITANZANIA MILIONI SABINI (70M). KAKA UKIHITAJI KILA KITU NIAMBIE NIKUTUMIE KWENYE EXCEL ILI TUSHARE WOTE TUWEZE KUJUA GHARAMA ZA UJENZI ZILIVYO JUU.
HIYO NYUMBA KWA HIYO BEI NI SAWA KABISA ILA TATIZO KAMA ALIVYOONGEA NDUGU YANGU MMOJA HAPO JUU SIYO RAHISI KUTOA MILIONI MIA MBILI KWA WAKATI MMOJA.
NAWAKILISHA
Hilo paa lenyewe materials ni kama 14M. Pavings kama 6M. Bado nyumba yenyewe.
ReplyDeletehiyo nyumna inadeserve, tatizo mtu akikaa ulaya anahisi anajua kila kitu, jaribu kujenga uone gharama zinavyoenda, the ahouse is good, ans the place is good to, pia kusema kuwa utapata wapi milioni 200, sio issue, kuna watu wenye hela, we differ alot, kama watu wananunua viwanja kariakoo kwa milioni 5oo atashindwa kununua kwa milioni 200, the house is good, i like it tuache usanii,
ReplyDeleteAnon wa Wed Dec 30, 03:18:00 PM na Wed Dec 30, 03:53:00 PM
ReplyDeleteWewe ni muuza nyumba na bei uliyotoa siyo practical kwa Tegeta na nyumba hiyo. bado nipo palepale kuwa acha usanii weka bei halisi ya nyumba watu wafikirie kuinunua siyo artificial figure.
PROPERTY MARKET WEWE KAA KIMYA TENA NYAMAZA WEWEUTABEBA BOX NA KUSAFISHA MAVI YA WAZUNGU MPAKA LINI NDIYO UINUNUE NYUMBA KAMA HII? HIYO BEI NI POA KABISA PAPA MSOFE AKIIONA ATAINUNUA SASA HIVI NA YEYE YUKO HAPA HAPA BONGO WALA BOX HALIJUWI. LAKINI JITAHIDI PENGINE UNAWEZA UKAPATA MKOPO BANK UKAJIKOMBOA.
ReplyDeletePROPERTY MARKET EXPERT UKO SAWA KABISA kwa 150%,nyumba Tegeta hio bei badoo jamani...Tegeta yenyewe miundo mbinu ni mgogoro leo uje na hio bei yaani nyumba ya kulala tu wala sio ya biashara NOOO hio bei ni too much.Nimefika bongo august nikapewa tenda na my cousin nimuuzie nyumba Magomeni nimeanzia 200m sikupata mnunuzi na nyumba iko sehemu nzuri na haitaji kuvunja kwani niya kisasa ina geti na kila kitu mpaka viyoyozi.Nilishindwa kuiuza pamoja na kwamba tulishusha bei mpaka 150m,niliondoka bongo after a month pasipo na mnunuzi na hapo ni migomigo how about TEGETA???????Hela ya EPA kwishney watu wameishiwa hizo 200m au 150m ni ndoto mtu kubwaga huko tegeta kwenye nyumba tuu..NA MTU WA UGHAIBUNI KWA NINI ANUNUE NYUMBA BONGO KWA BEI HIO WAKATI PESA HIO ATANUNUA HUKU UGHAIBUNI NYUMBA YA MAANA WITH EVERYTHING INNIT.....security,hot/cold tape water,electric ya uhakika,no vibaka/majambawazi,barabara za nguvu hakuna madimbwi ya maji etc.
ReplyDeleteKula tano PROPERTY MARKERT EXPERT.
mdau ughaibuni
gharama ya nyumba ya mhe gavana ni ya ujenzi tu na wala sio thamani ya property yote. kiwanja kilikuwa ni mali ya bot! lakini ninawahakikishieni hiyo nyumba hatimaye atauziwa kwa Tz shs milioni 60! akija gavana mwingine anajengewa mpya. ndivyo nyumba za serikali zinavyojengwa na kuuzwa. aina mpya ya ufisadi!!!
ReplyDeleteInawezekana 200m ni juu mno. Lakini nikiiangalia hiyo picha kwa bei za sasa hiyo kujnga na kila kitu inaweza ikawa 80 to 100m. Fine wale mnaosema Tegeta siyo sawa na Osterbay lakini kwa bei hiyo mimi naona inalingana na Tegeta. Tegeta kama eneo ni hot cake kwa sababu location yake iko barabara kuu na yenye lami. Iko karibu na the growing town of Bagamoyo. Halafu angalieni miaka mitano ijayo na currency yetu inavyoanguka. Yote hayo yatilie maanani. Labda angekuwa amejenga kwa mortgage.
ReplyDeleteOysterbay mwaka jana kiwanja kama cha ekari moja ni almost 700m kikiwa kitupu. Sijui sasa. Maybe 1 bilion??
Nyumba ni nzur, hata location "TEGETA" si pabaya. Inalipa. lakini naomba watangaziwe tenda watu wa BoT nadhani wataichulua. Hiyo price kwao ni kakununua chips.
ReplyDeleteBEI HIYO UNAWEZA KUPATA NYUMBA MBILI NZURI KUPITA HIYO, THE LOCATION IS NOT GOOD FOR THAT PRICE
ReplyDeleteNdugu wa Proerty Market Experty .. nakuomba uende bongo ukanunue kiwanja pale Tegeta halafu ujenge nyumba kama hiyo ndio uje utoe maoni hapa. Naona watu wanaongea bila vitendo humu.. Ndio 200mil ni nyingi na less than 95mil tsh. itakuwa ni ndogo kwa nyumba kama hiyo ukichanganya na bei ya kiwanja kule Tegeta.
ReplyDeleteWewe hapo juu uliyesema nyumba kama hiyo Kigoma haitouzwa zaidi ya 15mil nani aliyekudanganya? Umehesabu idadi ya madirisha ya aluminium ya hiyo nyumba ukajua cost yake huko Kigoma ni sh. ngapi? Siajabu madirisha ya nyumba nzima na grill zake ukute yana cost sio chini ya 7mil. Huo ukuta wa fence wa ukubwa huo, gate na pavement iliyowekwa hapo chini sio chini ya 10mil. Jumla ni 17mil bado nyumba yenyewe kujengwa. Jamani mtu kama huna uzoefu na vifaa vya ujenzi wa nyumba hasa nyumba za kisasa kwa kule Tanzania bora uache kabisa kuchangia mada kama hizi maana utaonekana kichekesho.
Ndio aliyeweka bei ya nyumba hapo ni kubwa lakini huwezi niambia ujenge nyumba kama hii sasa kwa 70mil sh. uone kama utamaliza inavyonekana hiyo hapo... Kama ni mkopo ulichukua bank itabidi ukaongeze tena.
Mdau
UK