MNENGUAJI mahiri nchini Queen Suzy usiku kuamkia leo katangazwa kujiengua rasmi kwenye bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia na kurudi katika Kampuni aliyowahi kuitumikia ya African Stars Entertainment (ASET) ambapo amejiunga rasmi kuanzia sasa.
Utambulisho huo wa Queen Suzy ulifanyika kwenye ukumbi wa Club Bilicanas ambako bendi hiyo ilikuwa ikifanya onyesho lake la kila Jumatano linalofahamika kama ‘Out of Africa Nite’.
Mashabiki walipagawa na kutoamini kile walichokisikia na kukiona kutokana na dada huyo mrembo na mwenye machachari awapo jukwaani alipotambulishwa na kusakata sebene ipasavyo.
Akizungumza na Tanzania Daima mmoja wa wasemaji wa bendi ya Twanga Pepeta Abuu Semhando ‘Baba Diana’ alikiri kwamba Suzy amerudi kwenye Kampuni yake ya wali hivyo hilo siyo jambo geni.
“Ni kweli Suzy karudi nyumbani lakini kwa wale wasiomfahamu ama kujua historia yake watashangazwa lakini ikumbukwe kwamba ASET ndiyo Kampuni yake ya kwanza kumtambulisha kwenye jukwaa la kunengua na kupata jina kubwa” alisema Abuu.
Aidha Abuu aliwataja wacheza shoo wengine wawili kwa jina moja moja waliotambulishwa pamoja na Suzy Club Bilicanas kujiunga na Twanga Pepeta ni Asha na Sabrina.
huyu karudi tu ili ajisogeze kwa kalala jr baba wa mtoto wake
ReplyDeletepatamu hapo kwa huyo mary sijui itakuaje