Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hili, Richard Mwaikenda akimkabidhi Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto (kushoto), zawadi na tuzo alizotunukiwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), baada ya kuibuka Mpigapicha Bora 2009. Picha na Joachim Kanyopa.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts Ltd, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Benny Kisaka (kushoto), akimkabidhi hundi Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hili, Richard Mwaikenda baada ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) kumtunukia tuzo ya Mpiga Picha Bora 2009, katika hafla ya kumpongeza iliyofanyika kwenye chumba cha habari cha Jambo Leo jijini Dar leo.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Jambo Concepts Ltd,inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, wakitakiana heri wakati wa hafla ya kumpongeza Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hili, Richard Mwaikenda baada ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) kumtunukia tuzo ya Mpiga Picha Bora 2009 jumamosi iliyopita.Hafla ya kumpongeza ilifanyika kwenye chumba cha habari cha Jambo Leo jijini Dar leo Picha na Kassim Mbarouk.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. gazeti hili lichukue watalaam wanaojua kazi kama linataka kufika mbali.kuna tatizo la menejimenti kwenye hili gazeti wajifunze umakini wa Mwananchi na Tanzania Daima.

    ReplyDelete
  2. Sorry, gazeti hili! Lipi?

    ReplyDelete
  3. Gazeti la Jambo Leo.linahitaji kusaidiwa kwenye menejiment.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...