Mpiga Picha Bora 2009, Richard Mwaikenda wa gazeti la Jambo Leo, akipongezwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wapiga Picha za Habari Tanzania (PPAT), Juma Dihule, wakati wa hafla ya kuwazawadia waandishi bora 2009, Dar usiku kuamkia leo. Hafla hiyo iliandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT). Jerry Muro wa TBC ndiye aliyeibuka mwandishi bora wa jumla

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hongera sana ndugu yangu Jerry Muro, kwa kweli you deserved for that award. LAkini Tatizo langu na MCT na watoa tuzo wengine ni pale wanapotaka watu wapeleke kazi ili zishindanishwe, badala ya wao MCT kufuatilia kazi za waandishi wa habari na kutafuta mshindi. Kwa mtindo wanaofanya sasa, wanatoa nafasi kwa Opportunists kutengenza habari na vipindi ili wapate award wakati uhalisia wao wa kazi haupo hivyo. Kwa mawazo yangu hii haisadii lengo la kuhimiza uandikaji wa habari za Uchunguzi kwa uendelevu.

    ReplyDelete
  2. Wazo la MCT kutoa award ni bomba sana but unfortunately it is wrongly handled. MCT wawe na timu yao inayochambua kazi za media na sio kusubiri entries kutoka kwa contestants

    ReplyDelete
  3. MCT mbona mliacha social media kama blogs kama hii ya jamii?? Where is your objectivity???????????

    ReplyDelete
  4. Hivi kuna mtu amefanya kazi ya uandishi bora hivi majuzi kama Vicky Ntetema wa BBC aliyeandika jinsi mauaji ya albino yanavyoendeshwa? Sasa ni kwa nini hajaewa award? Au simply kwa sababu kazi yake hakui-submit? MCT acheni usanii. Give credit where it is due.

    ReplyDelete
  5. Kuna columnists bomba sana nchi hii kama vile Jenerali Ulimwengu, Johnson Mbwambo, Anselm Ngurumo na Ayoub Rioba. Mbona na wao hawakufikiriwa na MCT? Au na wao ilibidi wa-submit kazi zao?? MCT amkeni kwa hili

    ReplyDelete
  6. Kuna waandishi wa habari za uchunguzi kama Mbaraka Islam, Charles Kizigha na wao walistahili recognition. Je ni lazima wawasilishe kazi zao??

    ReplyDelete
  7. Kuna watangazaji wazuri wa mpira kama Juma Nkamia, Maulid Kitenge na wengine. Hivi na wao walipaswa waambie MCT wanachokifanya ili wapewe awards?

    ReplyDelete
  8. Kuna sources wa habari wazuri kama vile Askofu Methodius Kilaini wanaokuwa available kwa journalists every time. Hivi na hawa ilibidi wawasilishe majina yao MCT??

    ReplyDelete
  9. Kuna vyombo vya habari vinavyoendeshwa very professionally kuliko vingine. Je navyo ilibidi vitoe majina yao MCT???

    ReplyDelete
  10. Shule za uandishi za mfano je? Kwa nini zisizawadiwe na MCT kwa kuwa mfano bora zaidi???

    ReplyDelete
  11. Mwalimu mzuri katika sekta ya habari je? MCT Hawakumwona?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...