Dada Jackline Twissa ambaye ni mwenyekiti wa Sauti ya Wanawake wa Afrika Ohio. (SWAO) akitoa hotuba ya kuwakaribisha wageni katika sherehe za Uhuru wa Tanzania Huko Columbus Ohio hivi karibuni.

Katika sherehe hizo Chama cha akinamama /kina dada wa Ohio kilifanya sherehe hii kwa mara ya kwanza katika miaka 18. Sherehe hizi zilikuwa zikifanyika mjini hapo na jumuiya ya watanzania katika miaka ya 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90.

Katika hafla hiyo chama hicho kilitoa tuzo mbali mbali ikiwa ni pamoja na ya iliyoitwa ya Mwl. Nyerere, Ubalozi bora, ya utamaduni na michezo na ya kujitoa muhanga kwa wanajumuiya wa Columbus Ohio.

Waliopata tuzo hizo ni pamoja na Sunday Shomari naJohn Sitta-Ubalozi bora.
Oliva Kavishe, Neema Chilewa,Isaac Lyatuu na Harry Layatuu-Uongozi bora (Mwl Nyerere). Kundi la marapper wa Columbus Si Matani -Utamaduni na Michezo.
Kujitoa Muhanga -Gloria Temba,Happy Mwakipesile, Charles Mhuto na Leo Mapunda.

Sunday Simba Shomary akipokea tuzo. Shoto ni mgeni rasmi Bibi Anita Diop kulia ni Jackline Twissa.
Mama Enid Fisher akimpa Jackline Twissa zawadi za wanatuzo huku Bibi Diop akijiandaa kuwapongeza.
Neema Chilewa akipokea tuzo na kulia kwake ni Jackline Twissa na kushoto Bibi Anita Diop mgeni rasmi
Gloria Nangitarame (kati kati) akipokea tuzo yake kulia ni Jackline Twissa na kushoto Bibi Anita Diop .
Happiness Mwakipesile (kati kati) akipokea tuzo kulia kwake ni Jackline Twissa na kushoto Bibi Anita Diop
Kundi zima la Si Matani lenye makao yake Columbus Ohio likipokea tuzo yao kutoka kushoto baada ya Jackline Twissa ni Prodyuza wa kundi hilo Lusungu Msola a.k.a Mtaalam, Boni Makilagi, mama Anita Diop ,Kolumba Mwingira,Paul Kirigiti a.k.a Fat Black na Sam Mfalila.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Natumaini hatujambo na tunaendelea na shughuli mbalimbali zinazotufanya tuishi nchini kwetu TANZANIA kwa upendo.
    Kaka Michuzi, naomba nitoe dukuduku langu na huu mwendelezo wa KUTOZINGATIA ALAMA YA TAIFA LETU (BENDERA).
    IMEKUWA NI MTINDO WA KAWAIDA KUIKUTA BENDERA YA TANZANIA INAPEPEA JUU CHINI KATIKA OFISI NYINGI ZA SERIKALI ZA MITAA, NA KWENYE MAONESHO MBALIMBALI. Nikiangalia bendera iliyopo hapo kimsingi sidhani kama ni ya Tanzania kwani haiko katika mpagilio mwafaka. jamani MSTARI WA BENDERA YA TANZANIA UNATOKA CHINI KUSHOTO NA JUU KULIA. Kwa kweli huwa nasikia vibaya nikiona imegeuzwa, napata mawazo ndio maana vitu hapa nchini vinajiendea kwani hata NEMBO YETU HATUIJUI. just google TANZANIA FLAG upatate kujua bendera inakaaje then endelea kuchunguza bendera utapata kile ninachokiona mimi.
    pole kwa wale niliowagusa wakaona najali sana kitu kidogo.

    ReplyDelete
  2. duh, wenzetu tena mmezidi, kiasi cha kuifanya bendera ya Taifa kuwa kitambaa cha mezani, michuzi hii imekaaje? najua wataitetea kuwa haikuwekwa hapo kitambaa cha meza bali kiwakiishi cha nchi, lakini hata kuwekwa ukutani imeshindikana?

    ReplyDelete
  3. Hakuna kitu muhimu huku nje kama umoja na uongozi imara wa watanzania. Utashangaa sis hapa tuliopo D.C karibu na ubalozi wetu na uongozi wa jumuiya hakuna kilichofanyika. What a shame!!!! Hata uhuru tunashindwa kukodi mahall ya community centers ya bei cheee tukakutana na kusheherekea uhuru wetu na kuonyesha utamaduni wetu?? Excuse me!!!!!! Kama wanavyosema watu wa huku. Michuzi usiibane hii something needs to be changed.

    ReplyDelete
  4. Kama walivyoandika waliotangulia..Inaweza kuwa kutokujua au makosa ya kiplotokali tu,kuhusu Bendera jinsi ilivyogeuzwa (Chini/Juu) na kuwekwa kama Kitambaa cha Mezani(Table mat).Lakini ukiacha tofauti hizo sina budi kuwapongeza wadada wa Columbus na haswa Jackie Twissa kwa kujali Utanzania wetu!

    Huo ni mwanzo msikatishwe tamaa na mwaka ujao jiandaeni vizuri na kutoa mialiko kwa watu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ubalozi wetu...Kuna kila haja ya kurudisha mshikamano wa kitanzania na kufanya mambo kwa kujali asili yetu..Ustaarabu,ukarimu na mapenzi iwe ndio nguzo kuu katika jamii zetu.....kumbukeni huku tuko ugenini tu,tukumbukane na kujumuika kwa pamoja kila tupatapo nafasi kama hizo.

    Mijumuiko hii isaidie kukumbushana maadili mema kwetu pamoja na vijana wetu wanaoishi Nje...kutoa maelezo ya kujenga/kuwekeza na kuendeleza nyumbani,Najua tukielekezana tunaweza.Dada Twissa pamoja na wenzio "wakati ndio Huu" tunawaangalia kama kioo.

    ReplyDelete
  5. Huyo wa bendera ,napenda kukwambia bendera ilikuwepo kama kawaida kwenye kamlingoti kwake ila haikuoneka kushoto ilikuwa ya US na kulia ya TZ. Hiyo ilikuwa ziada tukaona ngoja tupambe. Hivi unajua wenzetu mpaka vilemba chupi n.k za bendera zipo ,kuiweka hapo hivyo unashangaa nini

    ReplyDelete
  6. wewe uliyepeleka hizo picha kwenye michuzi umebagua kuna picha ya mtu mmoja hapo hujaiweka umeweka za wanawake tu pamoja na ya shomari...acha hizo

    ReplyDelete
  7. Hili Kundi la Si Matani mbona kuna members wengine hawapo? Simwoni Babu na Kevin Mkwawa hapo au wamejitoa kwenye hilo Kundi??

    ReplyDelete
  8. Hata km ilikua ya ziada tuiheshimu jamani na usiseme eti wenzetu mpkaka chupi n.k huo si utamaduni wetu, kuiga si vibaya ila tuige yalio mema jamani.
    Kuhusu kusherehekea jamani sio uhuru wa Tanzania, niwakumbushe tu iliyotawaliwa ilikua ni Tanganyika na sio Tanzania mboana mnapotoa Ukweli.
    Mdau Hyderaba.

    ReplyDelete
  9. Imependeza sana sherehe ya Uhuru wa Tanzania. Ningeomba waafrika,msipende kudharau mambo wanaoyafanya waafrika wenzenu.Sio vizuri! Hautakufa,kama ukiona chema hapo kwenye picha,na ukasifia kidogo.Macho yako,yasiangalie mabaya tu! Mazuri je? Acheni utoto,na furahia mema ya wenzenu. Waliojitokeza hapo na kujitahidi kuandaa hiyo tafrija,wametumia muda wao na hela zao ili ushibishe tumbo,na kufurahia muziki wa kiafrika hasa wa kitanzania. Mtu anayebeza mambo ya kiafrika hasa ya kitanzania,sijui anataka aishe sayari gani! Wapeni pongezi hao tafadhari.Ni kama Issa Michuzi,kuweka blog hii;sasa na wewe unaweza kuweka maoni yako ya kukatisha tamaa! Remain positive and eliminate negatives please! I beg!
    Ndugu yenu tena
    Chakubanga
    USA

    ReplyDelete
  10. Itifaki ni Jambo la msingi sana wadau, hili tupendi tusipende, inashangaza eti mtu anajitetea kuwa iikuwa haionekani ndio maana ikafanywa kitambaa cha mezani, kama si kudata ni nini huko? Bora ungechukua hiyo ya u.s.a. ukaifanya kitambaa cha mezani coz umesema wao wameifikisha mpk kuivaa kama nguo ya ndani, lakini si utamaduni wetu, kavae kimino K'koo uone shughuli yake, msitake kujijitea, mnazidi tu kujiumbua, inawezekana hata hapo kwenye mlingoti ilikuwa kichwa chini miguu juu, Itifaki michuzi, nafikiri kuna haja kubwa ya kutoa elimu juu ya hili, "itifaki v/s utamaduni na itikadi zetu

    ReplyDelete
  11. Sunday naona unavyojidai:)

    Hongera zako.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  12. Mnaolalamika mambo ya bendera, hamjui nchi iko juu chini, labda wenzenu wanaelewa hali halisi. Eti itifaki, GTFOH!

    ReplyDelete
  13. Hongera Neema... I'm so proud of you.

    Nas!

    ReplyDelete
  14. Watanzania bwana sisi ni watu wa ajabu. Yaani bendera kuwekwa mezani ndio imeibua zogozogo namna hii. Mambo muhimu yanayowagusa moja kwa moja hamuyazungumzii(umeme, maji, elimu, dawa, hospitali, barabara, umaskini, uhujumu uchumi, ushikaji kila pahali). Kwa namna mambo tunavyoyafanya sisi wabongo sishangai nchi kuwa maskini wa kutupwa 50 years after independence. Kaeni chini muzungumzie mustakabali wa nchi.. acheni poteza mda mwingi kuzungumzia mambo ya vitambaa.. Alaaa!!!

    ReplyDelete
  15. Anon wa kwanza anzisha shule ya upangaji na utmiaji wa bendera yako ya taifa sijakusikia kuzungumzia bendera sinazopepea bongo ktk mijengo ya gov nazimechanika chanika

    ReplyDelete
  16. aya ishoneni chupi,sidiria,leso mtolee mafua basi

    ata wimbo wa taifa tu hamjui,ovyo sana

    nyoooo,,,eti uku USA?so what

    ReplyDelete
  17. yalllllaaaaaaa we, jamani sikuwa namaanisha kuwa wamekosea kutumia hiyo alama, ninachomaanisha mimi ni ile kujua kuwa hiy ni LOGO/NEMBO ambayo inatakiwa ikae kama ilivyoandaliwa, inakuwa yale ya SONY na SONNY, yaani kitu kingine. kweli inabido kuwa serious kwani ilikuwa pale REGENCY hotel bendera zinapeperushwa juu chini tena zilizochakaa, ukiwaambia wanadai mbona ziko sawa, kwa sasa wameshusha kwa lazima. nakumbuka hata wakati Mh. Ras alitembelea Marekani kulikuwa na ile flag ya mezani iko upside-down.
    Mnaotumia please spare us the muwe mnaiwka inavyotakiwa. hebu cheki hiyo ya USA hapo kushoto kwa snaps ilivyotulia hukuti hata siku imegeuka!!! TANANIA NAIPENDA NCHI YANGU (regardless ya yanayoendelea)

    ReplyDelete
  18. Kwa kuongezea na kumsaidia wa juu hapo, mkubali kua hilo ni kosa as they says "long journey started with a single step" now we starts with the flag. jamani hilo kosa rekebisha ama kubali umefanya kosa na kufanya kosa ni kosa kulirudia umeongeza koa. jamani tuwe makini na wawazi muhusika amefanya kosa hapo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...