Mkuu wa Libeneke na Balozi wa nanii....
Naomba msaada tutani kwa sana,kwa wadau tuliokuwa JKT Mafinga Iringa - Rungemba deti.-Operesheni Vyama Vingi 1992- Enzi za Afande Mahili Mlay .kama wakina Nzawisa,Huruma,Idetelo (Mzee wa Apetaiza) ,Mkisi,Mpalanzi,Mayolage,Lute a.k.a TBS ( huyu jamaa alikuwa demo ya afande kwa kulima matuta) ,Bwana shamba,mkama,mpokwa,Habibu aka Mkono spana,Maketwa a.k.a Macho na wengineo wengi ,jamani tutafutane ili tukumbushane siku hizo za Ukuluta hadi Userviceman bila kwata ila kwenda range tu.maana ni muda mrefu ,mie nipo Dar naganga njaa .Jamani ilikuwa sio mchezo tulikuwa mswana ile mbaya kama ndugu mmoja.
Nawatakia Krimasi njema wote pamoja na mwaka mpya 2010.

Ni mie A.k.a - Bingwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Mafinga 1992 - yes, that was ages after I left and how I wish I could roll back the clock and see the bullies (Mpogole Mpilano Nico Kimbunga, Comandoo - D-coy, I understand he is dead now, afande Majota - the King of kunyakua) from a glass shield and holding Medusa's head just in case they came near me. Like slaves in La Bamba during the nights we would sing away our day exhaustions and torments - kanyaga sukuma, siku ziende kuruta we...(by the way it is kuruta as opposed to kuluta - but it doesn't matter, anyway).

    Just in case you are wondering which century all that was - it was when Julius Nyerere ruled the land and Yanga and Simba dominated Tanzanian football - George Orwell's 1984 - a quatre of a century ago!

    ReplyDelete
  2. @ Al Musoma.....Umenifurahisha sana na comments zako.

    Watu mliopitia JKT huwa mko very proud na hiyo kitu. Lakini kila ikitaka kurudishwa mnasema ''it was bullshit''!

    Tukuchukue lipi?

    ReplyDelete
  3. weacha tu umenikumbusha matunda fulani tulikula sana njiani kwenda idetelo,yanaitwa mikusu.pia ulanzi ule mkangafu unauchanganya na konyagi we achatu sikuhiyo mbona kikosini watakukoma,hasa mad....e...lakini mimibinafsi jkt kwangu nliipenda,inafundisha,kwa watoto waliotoka mjini kuwa washamba,na kijijini kuwa wamnjini yaani wajanja,mimi ndo nilivyoona.pia lisilowezekana uraiani jkt linawezekana tena bila mjadala safisana.nililima sana ,nlijenga sana ile shule mpya.nakuangusha miti,bila kusahau kuzima moto.nilikuwa A,coy najamaa wengi tu.

    ReplyDelete
  4. Kijana wa zamaniDecember 16, 2009

    JKT ni muhimu ikarudishwa. Inajenga moyo wa uzalendo na kujituma bila ya kudeka. Pia mtandao wenu unakuwa mkubwa na udumu. Sisi wengine tulipita zamani kidogo miaka ya 1972. Operation TUMAINI. Nilikuwa Makutopora. Niliingia nikiwa mwembaba na kilo 50. Nilipotoka nilikuwa na kilo 65. Kisa? Wakati naingia nilikuwa bwege lakini wakati ninamaliza nilikuwa mjanja nikijua mbinu zote za kukabiliana na mazingira magumu pale kambini. Nilikuwa smart kuhakikisha ninapangiwa zamu ya kupika jikoni au kwenda kuchunga mabanda ya kuku. Kila kazi ilikuwa na marupurupu yake. Pale kwenye jiko onja onja ilikuwa ni sehemu ya job description. Kwenye kuku mayai tulikuwa hatuibi ila tulikuwa tunasogeza tu. Utaacha kunenepa. Wala huna haja ya kuwaza. Maafande were thinking on our behalf. enzi zile mkuu wetu wa Kambi Brigadier General Adam C J Mwakanjuki. Very smart Mkuu wa kambi.

    Kuna kituko kimoja siwezi kukisahau. Afande wa mashamba ya mizabibu akiitwa Lenard. Mzee yule akipenda kutuhenyesha kisawasawa. Alipoona mawingu na mvua inakaribia kunyesha. Akapiga filimbi ya foleni na kuwaagiza mafande huku akisema "Leader!!Peleka kuruta hawa wakamwagile mizabibu kabla mvua haijanyesha" Sounds funny and stupid. Lakini kwa JKT haikushangaza. Hayo ndiyo yalikuwa maisha. Hata mimi na uzee wangu nayakumbuka sana maisha yale.

    ReplyDelete
  5. Kweli ,Bingwa umenikumbusha mbali sana,kwa jinsi tulivyokuwa kunakaa Rungemba kweli ilikuwa raha sana.Nakumbuka tulikiuwa tunatembea kilometa zipatazo 15 mara 2 kila siku kwenda Kijijini,kwenye ulanzi,ukipita ulanzi inakuja komoni,baada ya komoni inakuja kiambule vyote hivyo ukiwa jkt aina budi utumie hili siku ziende.Lakini kubwa tulikuwa tunafundishwa uvumilivu sana .Nakumbuka nilipotoka jkt nilikuwa natembea Mwenge mpaka posta kwa mguu kila siku,na kuona kuwa ni jambo la kawaida kabisa.
    Natamani sana jkt irudishwe.Mie pia nilikuwa Rungemba deti- A coy kwa afande Waziri.
    Wadau toeni mikwara zaidi ya jkt,nakumbuka nilikaa wiki moja bila kuoga mara baada ya kuripoti mafinga - baridi,baadae nikazoea sana,pia kitendo cha kutembea na mestini kila sehemu hata msalani ndicho kiliniacha hoi,kwani ukiwa huna mestini jkt kula ni kwa bahati sana.

    Jamani,irudi vijana siku hizi legelege sana.

    ReplyDelete
  6. Uzuri mwengine Jkt hata ufanye kosa gani,hakuna kufukuzwa bali utapigwa bogi tu Mafinga - Bulombola.Maisha yanakwenda hakuna kufikiri.Bingwa nakumbuka alikuwa mjanja sana kwa mbinu pale deti.
    a.k.a TBS

    ReplyDelete
  7. Safi sana kukumbuka wenzako huna moyo mswano kweli.JKT watu lazima muwe ndugu kabisa.
    Nilikuwa B coy kwa afande mwenye mkwara wa juu staff sajenti Adam.anakwambia staff sajenti ni cheo chake na sio jina lake,sasa hole wako umuite Adam,utajuta kuwa coy B.

    ReplyDelete
  8. jamani mie namtafuta peter chambi wa coy c makutupora jkt (1992-93). alikuwa akitokea shinyanga. kwa yeyote mwenye habari zake, naomba anitumie email: info@tzuk.com ili nimshukuru.

    ReplyDelete
  9. since we r talking JKT i might as well chip in too. JKT Makutupora Operesheni vyama vingi,duh ilikua poa sana kwa kweli mimi experiensi yangu ya kuwa mvumilivu huku ughaibuni ni matunda ya JKT. Na marafiki zangu niliofamaiana nao JKT ni kama ndugu zangu hadi leo, hatujapotezana,.
    coy B au wabeba magogo, watani wetu wa jadi walikua A coy wabeba nyanya LOL. CO alikuwa afande Rajabu Mzenji mkubwa kama Pepe Kale, kuna afande mmoja alikua anapenda sifa huyo, afande Matondo, hana meno ya mbele inasemekana kwa masifa yake alikamata kuruta wamejificha msituni akawapiga extra drill kuruta wakapiga mahesabu ni wavulana kadhaa na kina dada, kwanini tusimpe kibano huy mtu mmoja anatushinda nini? basi nasikia walimpa kibano cha nguvu han hamu kimbele mbele chote kwisha mbaya zaidi alivofanikiwa kurudi kambini hoi akaminya kwa Noma!lol aseme achekwe! Kimbelembele hakuacha ila alijifunza where to use it.
    story ni nyingi sana hiyo ni moja tu naona niandike kitabu cha hadithi za JKT,,,
    NB: Tall wa B coy bonge la msanii hakupiga kwata kwa kisingizio hana size ya buti! lol, bonge ya comedian nikimkumbuka tu naanza kucheka kwa nguvu sana. ha ha ha ha

    ReplyDelete
  10. Something goes unmentioned. JKT was characterised by institutional bullying and raping - both high level crimes which went unpunished. If I had to do it again, I surely wouldn't...

    ReplyDelete
  11. we al-musoma ulienda jeshini kweli? bullying yes but raping no. usichanganye mapenzi na kubakwa kisa binti `msomi' kuhusiana kimapenzi na koplo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...