Marehemu Mzee Ronald Zakaria Mliga
Familia ya Mliga, inapenda kuwashukuru nyote kwa upendo wenu na kushirikiana nao tangu mlipopokea taarifa ya kifo cha mpendwa wao, baba, babu, mjomba Mzee Ronald Zakaria Mliga kilichotokea nyumbani Ada Estate jioni ya tarehe 18 Novemba 2009 na kuzikwa katika Kijiji cha Mamboya, Wilayani Kilosa tarehe 22 Novemba 2009.
Tunawashukuru kwa kutukimbilia nyubani na kutoa salamu zenu za rambirambi, na kushiriki kwa hali na mali katika maandalizi na mazishi yake. Tulihitaji sana msaada wenu katika kipindi hicho kigumu sana, msaada ambao ulipatikana papo hapo kwa kiwango cha hali ya juu pasipo matarajio.

Tunapenda kumshukuru kila mtu na kumtambua binafsi, lakini tunashindwa kufanya hivyo kwa kuwa si rahisi kutokana na udhaifu wa kibinaadam. Hata maneno ya kuelezea vya kutosha jinsi tulivyoguswa na upendo wenu nyonyoni mwetu hatuna.
Tunachoweza kusema ni AHSANTE.

Tunamshukuru Dr. Kaushik Ramaiya na wafanyakazi wote wa Hospitali ya Shree Hindu Mandal, Uongozi wote na wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Viongozi na wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Air Tanzania, Mheshimiwa Askofu Getrude Rwakatare, Mchungaji Chegere wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Mikocheni, Askofu Oscar Mnung’a wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Newala, Cannon wa Mtwara, wajumbe wa halmashauri ya mtaa, kwaya za El Shadai na Upendo Kanisa Anglikana la Kristo Mfalme Kinondoni.
Tunawashukuru Bw. Na Bibi George Lauwo na familia yao, majirani zetu wa Ada Estate na Sea View na Kijijini Mamboya, ndugu jamaa na marafiki zetu wote ambao ,mlishiriki nasi kikamilifu katika kuomboleza, kuanzdaa na kushiriki katika kufanikisha sherehe ya mazishi yake hapa Dar-es-Salaam na kijijini Mamboya. Tulifarijika sana na upendo wenu na kushiriki nasi katika kipiondi hicho kigumu tulichopiotia. Mungu awabariki nyote.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya
Marehemu Robnald Zakaria Mliga mahali pema peponi,
Amin.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Amina Mungu ailaze roho ya marehemu babu yetu mpendwa mahala pema peponi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...