Msondo Music band wakiwa jukwaaniBendi kongwe ya muziki wa dansi nchini Msondo Music Band siku ya jumanne hii watafanya utambulisho wa albam yao mpya ya 'Huna Shukrani' kwa staili ambayo haijawai kufanyika nchini, imefahamika.
Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kwamba utambulisho huo utafanyika katika ukumbi wao wa Amana uliopo Ilala.
Alisema katika uzinduzi huo bendi ya African Star wana wa 'Twanga Pepeta' yenye mashabiki lukuki nchini watawasindikiza ndugu zao wa Msondo.
Mhamila alisema licha ya kusindikizwa na bendi hiyo pia wamejipanga kutoa zawadi kwa mashabiki wao, ambapo kila mpenzi atakaekata tiketi ya kuingia ukumbini atapewa zawadi ya albam yao mpya.
Alisema nyimbo zitakazotambulishwa siku hiyo ni pamoja na wimbo uliobeba albam hiyo, 'Huna shukrani' uliotungwa na Saidi Mabera, 'Kiapo' (Hussein jumbe) 'Haki yangu ipo wapi' (Huluka Uvuluge) 'Mama Cos', uliotungwa na marehemu Josephe Main, 'Albino' (Juma Katundu) 'Machimbo' (Isihaka Kitima dj papa upanga) na 'Cheo ni Dhamana' (Eddo Sanga).
Aidha aliwataja wanenguaji watakaokuwa wanatoa burudani katika safu hiyo kuwa ni Amina Said 'queen Emmy' Nacho Mpendu 'mama Nzawisa' na Amiri Saidi 'Dongo'
Pia rapa wa bendi hiyo Romani Mng'ande 'Romario' atawachenguwa mashabiki watakaofika katika onesho hilo wakiongonzwa na mkurugenzi wa bendi hiyo Muhidini Gurumo na Band Master Saidi Mabera.


Hivi hao wafadhili hawana uwezo wa kuwapa nguo za maana hao wanamuziki? Kila siku hiyo mi-tshirt, wapenzi wao wanaridhika? Enyi watu wa Safari, kuweni wabunifu zaidi, muitangaze biashara yenu na wanamuziki muwapendezeshe pia!!
ReplyDeletekampuni kubwa wabunifu wa matangazo mbumbumbu na maboss wao hawalioni hilo..tshirt zina quality ya chini mno wakati msondo ni baaaaaaab kubwa
ReplyDelete